Kauli ya Murugo siikubabali

ligendayika

JF-Expert Member
Aug 31, 2012
1,183
198
Namsikiliza Mh Murugo anasema kuwa kazi ya chama cha upinzani ni kupinga mipango ya maendeleo ya chaa tawala. kwa mujibu wa Murugo hiyo ni kazi ya wapinzani duniani kote. Kwangu mimi hiikauri si ya kweli. Ebh wenye akili wa JF ichambueni hii.
 
Kazi ya upinzani ni kuikosoa serikali na kuifanya ifanye kazi kama inavyopaswa. It is to make the government accountable.


Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Huyo jamaa bila shaka ndie wa Tanzania ni muungano wa Zanzibar na Zimbabwe! Ndio tafsiri wanazo waambia wapiga kura wao ili wajenge chuki kwa opposition parties yet ni Waziri tena katika Elimu
 
Hajui tofauti ya kupinga na kukosoa

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Huyu hafikiri kabisa yeye anajibu tu. Hata waziri mwenye dhamana anawapongeza watu wengi mpaka Spika ameamua kumkumbusha kuwa hakuna muda wa kufanya hivyo.
 
Tangu aliposema muungano umetokana na Tanganyika na Zimbabwe nilishamfuta kwenye listi ya mawaziri pamoja na kuwa jk anamkumbatia!
 
Labda imempasa kurejelea kusudio la uanzishwaji wa Vyama vya Upinzani mwanzoni mwa miaka ya 90
 
Mzee wa Zimbabwe na Tanganyika hehehhe hili lijamaaa hivi halikuona aibu?
 
Watz ndo zetu kupinga kila jambo pasipo kuthnk. Upinzani unapaswa kukosoa pale gvt inapokosea but wapinzani wa tz wanapinga hata maendeleo ya nchi kwa maslahi ya vyama. Taifa kwanzaaaa.
 
Kwanza kabisa mleta mada hii una tatizo kama la huyo waziri wako, yani wewe na Mulugo hamjui tofauti ya matumizi ya R na L. wewe umesema KAURI, neno sahihi ni KAULI. Huyo waziri wako ndiyo kabisaaaa hata nashindwa kuhesabu ni maneno mangapi kayakosea ktk hotuba yake wkt anajibu hoja za wabunge. natoa mifano michache ninayoikumbuka. mf alisema, elimu BOLA, badala ya BORA, TABOLA badala ya TABORA, NAZANI basala ya NADHANI, yaani mpaka nashangaa huyu bwana taaluma yake ni nini na mbona kapewa wizara nyeti lkn hata matumizi ya maneno na herufi hajui. kapataje uwaziri huyu wkt hana ufasaha?????????
 
Si Mawaziri wala Wabunge wa CCM wakuwaamini kwasasa hasa juu ya kauli zao.Leo Bungeni,Mbunge mmoja wa CCM alisema kwa nia ya kutamba: ' Mimi nilisoma PCM na nikapata Division One ya Hesabu'. Chama changu kimefikishwa hapa na upinzani ambao haukuwahi kuwepo tangu Uhuru. Sasa,mtusikilize kwa makini ndugu zangu watanzania. Kiukweli,hatuko poa!
 
Yaani kila waziri ni kituko,tumsaidie bure,upinzani ni "watchdog".Ohoo sijui kama atanielewa hapa.
 
One Nineteen Sixty One (1,1961)
Ila leo Hamim alikuwa na hofu sana
pia bajeti imewatoa jasho hasa Cdm
walipowabana kuhusu uongo wao
kwenye matokeo ya kidato cha 4.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom