Kauli ya Mnyika, Inakatisha tamaa...

Kauli ya Mnyika, Inakatisha tamaa...

mbona imekaa vizuri tu hiyo,nilidhani amesema kuingia ikulu kwa namna na mbinu yeyote watafanya,kama mkwere,ila hiyo hapo juu mbona iko shega tu,naona kweli magamba yameshikwa pabaya yanafuatilia hotuba na kampeni za UKAWA kwa karibu kuliko hata UKAWA wenyewe, lol
 
Yaweza kuwa hukuelewa au huelewi kazi za mbunge. Kazi kubwa ya mbunge ni kuisimamia serikali....Hata kama ni serikali ya chama chako lazima isimamiwe. Kwa hali hiyo wakiingia bungeni wataisimamia vizuri serikali yao chini ya CDM kwa mwamvuli wa UKAWA hivyo kuleta ufanisi

Umemjibu vizuri sana. Sijui kwanini watu hawaelewi jinsi gani serikali inaendeshwa. Very basic knowledge lakini watu hawanayo kabisa.

Kweli "ujinga" bado ni adui mkubwa wa maendeleo.
 
Hata serikali ya ukawa inahitaji kutikiswa inapolegalega, hajakosea

mkuu, kwa u potential walio nao kina Mnyika na Kubenea, possibly hawawezi kukosekana kwenye baraza la mawaziri.
Hapo watajikosoaje?
 
kwa hiyo ulitaka wasiionye serikali hata kama ikikosea????
ACHANA NA UCHAMA MKUU WEKA UZALENDO MBELE

Hapo uelewe ni gamba limemwelemea tu vinginevyo tunajuta kuufungua uzi huu na kuusoma umetupotezea muda.
 
Mnatowa na vyeo vya uwaziri! Mmekosa ya kuandika kweli! Nawasihi kwamba muwe kama mimi kwamba Matokeo yeyote yale niko Tayari kukubaliana nayo kwa Amani ya nchi yangu. Ila naona wengine muandako ni mbali na mna jiandaa kukataa matokeo ya kuwa angusha.
 
kwani hamkumsikia kwenye kipimajoto itv akisema naomba wananchi wachague wabunge na madiwani wengi wa ukawa.... kuhusu rais hakugusa kabisa nadhani anajua hawawezi kupata
 
Huwezi kuitoa ccm madarakani hata siku moja

Mmm! Ww tz nchi ya vyama vingi so chama chochote kinahaki ya kuchukua dola ukiendelea na msimamo huo wakutokukubali hali halisi ni sawa na kujionea ww mwenyewe fikra zako na maendeleo yako so usirudi nyuma nenda mbele hii ndo democrasia ya sasa kuwa na mawazo huru
 
Kazi ya mbunge sio kutetea serikali Bali wananchi.Mnyika yupo vizuri.anajua fika ccm imeshaondoka,kilichobaki ni kuapishwa serikali mpya ya mh Edward LOWASA.
 
Mbunge makini haingii bungeni kwa "Kuunga mkono hoja kwa asilimia mia" wala kuiimbia serikali Aleluya, bali huitikisa serikali hata kama ni ya chama chake kwani huwa yuko bungeni kwa ajili ya kutunga sheria na kuwatetea na kuwaletea maendeleo wapiga kura wake.
 
Rabboni

Kisha Mnyika inaonekana hadi sasa hivi moyo unamsuta, anashindwa kumuangalia Lowassa usoni, ndio hivyo hana pa

kwenda ila kuna vitu inaonekana wazi hajavifurahia jinsi vinavyokwenda.

Huyu ni mtu makini aliyekuwa anajitahidi sana kupambana na ufisadi.
 
Last edited by a moderator:
Rabboni

Unajua kazi ya mbunge?kazi ya bunge ni kuisimamia serikali,iwe serikali ya ukawa iwe serikali ya ccm!
Mmezoea mibunge yenu ya ccm kujigeuza serikali ndio maana hujamuelewa Mnyika
 
Last edited by a moderator:
Rabboni

kazi ya wabunge ni kuisimamia serikali bila kujali ni ya chama gani, hvy hata lowasa akishinda,bado wajibu wa wabunge ni kuisimamia serikali ya ukawa, POLE, UNGEKUWA UMESOMA SEKONDARI HADI KIDATO CHA PILI KUNA MADA NDOGO INAYOITWA ORGAN OF THE STATE.NDANI YAKE NDO KUNA PARLIAMENT,EXCUTIVE AND JUDICIARY.
 
Last edited by a moderator:
Alijisahau tu !. Ni ubinadamu kutokana na uzoefu na mazingira yake !

Kwa sababu amekuwa mpinzani kwa muda na hayuko katika serikali inayotawala, mara nyingine unconsciously mtu unaweza kujikuta unaongea katika present tense (ambapo yeye bado ni mpinzani) badala ya future tense ambapo yeye anategemea kuwa chama tawala......Hata wewe (au mimi) ungeweza kuchanganya na kufanya kama alivyofanya !

Hata Lowassa kuna siku alijichanganya akasema CCM hoyeee na hii ni kwa sababu ya kuwa katika CCM kwa zaidi ya miongo mitatu na kuna vitu unakuta unavifanya unconsciously kwa sababu umezoea sana kufanya hivyo.....

Lakini hata hivyo mbunge kazi yake ni kusimamia serikali kwa hiyo kwa namna nyingine whether alipitiwa kama nilivyosema hapo juu au alimaanisha, bado anakuwa sahihi, kwa sababu kwa kufanya hivyo anakuwa anatimiza wajibu wake kama mbunge.....

Rabboni
 
Last edited by a moderator:
John Mnyika, Mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema jana alitoa kauli ambayo kidogo ilitufanya wachache tufikirie tofauti na dhamira kuu ya UKAWA kuwaondoa CCM.

Mnyika alisema, wananchi wa Ubungo na Kibamba wafikirie juu ya uwepo wake na Kubenea ndani ya bunge utakavyoitikisa serikali...
Kwa kauli hii inamaanisha kuwa Mnyika haamini kama Ukawa watachukua nchi!!
Au alimaanisha wataitikisa serikali yao wenyewe watakaoiunda?

It means hawaamini kama Serikali ya CCM itatoka madarakani, wakati sisi wananchi wa kawaida tushaliona anguko kubwa la Chama cha Mapinduzi.

Kwamba wakiingia bungeni ni kutetea wananchi wanaowawakilisha kwa serikali. Haina maana kuwa wakishinda basi kila kitu cha serikali hata kama ni ya kwao iwe ndiyo kama ilivyo kwa ccm. Ndio maana wao wanaamini kutenganisha serikali na bunge. Vinginevyo, watakuwa hawana tofauti na ccm!
 
ahahahhaaa Mnyika ameusoma upepo akaona hawawezi kuingia Ikulu hata iweje maana wanajua CCM ni shina la mbuyu huwezi kuukata. .
Ila ananishangaza amesahau kuwa hata yeye Ubunge jimbo la kibamba hachukui hata kubenea pia hachukui Huu Mwaka CCM wamejipanga aisee ni nooma ukawa waliewalie tu
 
Back
Top Bottom