Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 1,408
- 3,575
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, amekanusha vikali kauli ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, inayodai kuwa vyama vyote vya siasa, ikiwemo CHADEMA, vilishirikishwa na kukubaliana na taratibu za uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji.
Mnyika ameeleza kuwa kauli hiyo ni ya uongo na upotoshaji, ikilenga kuonyesha kuwa CHADEMA ilikubaliana na taratibu ambazo chama hicho kinaamini zina upungufu mkubwa, ukiukwaji wa haki, na udanganyifu katika mchakato wa uchaguzi huo.
Aidha, Mnyika amesisitiza kuwa CHADEMA haijakubaliana na taratibu zinazokiuka katiba na haki za wapiga kura, na kwamba chama hicho kinaendelea kupinga ufisadi na uovu unaoendelea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Hata hivyo, Waziri Mchengerwa amekuwa akisisitiza kuwa uchaguzi huo utakuwa wa haki na uwazi, akieleza kuwa jumla ya wapiga kura 31,282,331 wamejiandikisha, sawa na asilimia 94.83 ya lengo la uandikishaji .
Pamoja na hayo, vyama vya upinzani vimeendelea kulalamikia kuenguliwa kwa wagombea wao katika kinyang’anyiro hicho, huku Waziri Mchengerwa akivitaka kutumia siku mbili zilizowekwa kuwasilisha malalamiko yao badala ya kulalamika pembeni .
Soma: TAMISEMI yasema CCM imefanikiwa kuweka Wagombea Mitaa yote, upinzani wameweka Wagombea 30,977 katika nafasi 80,430