Ibrah
JF-Expert Member
- Mar 22, 2007
- 2,729
- 528
Juzi Rais JK akiwa ziarani Mtwara, alinukuliwa na vyombo vya habari akiwataka wakazi wa Mtwara wajiandae kupokea uchumi mkubwa kwa kuwa Mtwara kuna hazina kubwa ya gesi na Mafuta. Hadi sasa sijajua mantiki ya kauli ya Mh Rais, maana tunajua kuwa kuna gesi Kilwa (Songosongo Island) na pia mwaka juzi tulitangaziwa kugunduliwa kwa gesi nyingi Mkuranga. Nijuzeni Wana wa jambi; Je, Mafuta yameshagundulika Tanzania?