Je, kampuni Kemexon ya Ubelgiji ndiyo inayoiba mafuta na Gesi ya Mtwara?

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Salaam wakuu,

Hivi karibuni tumeshuhudia Meli zikianza kubeba Makaa ya Mawe kutoka Mtwara. Watu wakadai Makaa ya Mawe Tanzania inayauza kwa kila tani moja ni Elfu sitini za kitanzania huku Soko la dunia kila tani ni Dola 300 zaidi ya laki saba za Kitanzania. Hivyo ikaonekana huu mkataba ni wa kifisadi.

Hivi Karibuni rais Samia Alitembelea Ubelgiji ambapo ndo Makao Makuu ya Kampuni inayohusika na Kununua Makaa ya Mawe ya Huko Ruvuma na Mtwara.

Je, Gesi yetu ya Mtwara na Mafuta ya Mtwara, hii Kampuni inahusika pia? Kipindi cha Nyumba Dr. Slaa na Magufuli kwa Wakati Tofauti walisema kwamba Mafuta na Gesi kutoka Mtwara hatuna Chetu kwani Mabomba yajengwa Baharini kuelekea Ulaya.

Kampuni inayomilikiwa na Ubelgiji iliyosajiliwa Hong Kong inayofanya biashara zaidi ya mafuta ya petroli, nishati na bidhaa za madini, Kemexon, inasimamia mauzo ya makaa ya mawe kutoka Ruvuma Coal, kusini magharibi mwa Tanzania, hadi Ulaya na Asia.

Tungependa Serikali iseme inavyouza Makaa ya Mawe kama Wanavyotaja bei ya Bamba, Kahawa na Alizeti. Mikataba inafichwa sana.. Ukilalamika wanasema leta mkataba sababu wanajua huwezi kuupata.

Pia, soma:

Thread 'Meli nyingine iliyobeba makaa ya mawe yaondoka kutokea Mtwara kwenda Ulaya' Meli nyingine iliyobeba makaa ya mawe yaondoka kutokea Mtwara kwenda Ulaya

Issue ya Gas kitambo sana tulipigwa...bunge la mwisho la Mzee wa msoga waziri akiwa Simba-Cha-*** walipitisha miswada ya gas kwa hati ya dharura, walijua ajae ni mtu wa aina gani. Hi ndo sababu ht yeye hakua na muda nayo.
Ss km bei ya soko ni dola 300 na sisi huku ni elfu 60 then kuna tatzo.
 
Hata samaki wa baharini pia wameshauzwa wote na hii awamu, Wanzanzibari na Waislamu wenzake wanalia huko kupelekewa Kambale.

Haijawahi kutokea tangia binadamu aanze kuishi kisiwani Zanzibar wakalishwa kambale wa mtoni!
 
Mleta mada ni mpumbavu!

Si ni wewe ulikuwa unasifia royo tuwa hapa
 
Biashara ya gas ya mtwara iliuzwa kwa bei ya kutupa wakati wa utawala wa awamu ya 4!
Kumbukeni mikataba ya dharura iliyopitishwa na wabunge wa ccm tena kwa rushwa za waziwazi kabisa!
 
Wabongo bwana.

Kuna wakati tujipe muda wa kusoma mambo na kupata uelewa kidogo kabla ya kuanzisha sensitive discusions.

Gas au madini hayajiotei tu ardhini ukaanza kuchukua ni vitu ambavyo vina process zake kujua kwanza uwepo wake na kuchimba.

Ili uchimbe gas au madini lazima kwanza ujue yapo kiasi gani mahala hapo na utayachimba kwa muda gani na gharama zake ni kiasi gani kuanzia kuyatafuta na kuyachimba.

Ukijua madini au gas chini ipo kiasi gani na taarifa zoote za kitalaam zitanazokubalika kimataifa ndio zinakupa uwezo wa kupata fund ta kuyachimba.

Makampuni mengi kama sio yoote unayoyaona makubwa ya utafutaji madini na gas sio kampuni la mtu mmoja bali ni shares za watu zimewekwa humo na mengi yako listed kwenye International stock exchanges.

Utafutaji na uchimbaji wa madini na gas ni gharama sana na uwekezaji wake inahitaji hela nyingi saana kiasi kwamba ni tatizo kwa nchi masikini hasa Africa Tanzania ikiwemo, Hela, Technolojia na skills hivi vyote hatuna na hapa ndio shida inapoanzia kudeal na mabepari.

Investors ni mfanyabiashara kama mfanyabiashara mwingine lazima ajiwekee mazingira ya kupata faida tena kubwa ikiwezekana na hapa lazima apambane kila negotition iwe upande wake na yeye apige hela kampuno iwepo na iendelee kuwa giant.

Makampuni mengi yenye uwezo wa kufanya hizi kazi kwa maana ya technolojia, mitaji na skills ni mali ya wazungu na ndani yake ina mikono mirefu ya mashirika ya kijasusi kutoka nchi hizo kwa manufaa ya nchi zao.

NJIA PEKEE KWA AFRICA KUWA HURU NI KUJITEGEMEA NA KUWA NA UWEZO WA KITEKNOLOJIA, KIUCHUMI NA WATALAAM, KUIFIKIA STAGE HII KUNAHITAJI SACRIFICE YA VIZAZI KADHAA, JE TUKO TAYARI KUJISACRIFICE KWA MATESO MAKALI ILI VIZAZI MBELENI VIPATE UNAFUU?
 
Vitalu vya makaa ya mawe vinamilikiwa na makampuni binafsi kwa serikali kuwapa maeneo ya uchimbaji maeneo mbalimbali hasa Songea.

Kampuni hizi zipo Za wazawa na za wageni pia, zote zimepewa vitalu sehemu mbalimbali kufanya exploration na kuchimba ambavyo vyote vinahitaji hela sio hizi za mboga bali bilions, na makampuni haya mengi hasa ya kigeni ni shared with different investors.

Coal kwa sasa inademand kubwa Europe kutokana na crisis ya Russia vs Ukraine, wenye vitalu Songea with their own wakiwemo Ruvuma coal wametafuta wateja na kumanage kuexport kuuza hiyo coal.

Ukisoma hapo juu, utaona, anayeuza coal sio Serikali ya TZ ni wamiliki wa vitalu vya coal ambao wameweka hela zao, Serikali inalipwa kodi, mrahaba nk ambavyo ni serikali kupitia bunge ndio wameviweka, kwa hiyo kama hao wachimbaji na wasafirishaji wanavibali na kulipa hizo kodi na mirahaba hakuna shida.
 
Sasa kwanini tuuze kwa bei ya kutupa hivyo?
Yanaendelea kuoza ndiyo maana tunaharakisha mzigo uishe ili tusikose Bara na Pwani.
Mwl.Nyerere hakufikiri sawa sawa kukataa mgao wa >75% baina ya Serikali ya Tanganyika na Wawekezaji wa miaka yake.
 
Yanaendelea kuoza ndiyo maana tunaharakisha mzigo uishe ili tusikose Bara na Pwani.
Mwl.Nyerere hakufikiri sawa sawa kukataa mgao wa >75% baina ya Serikali ya Tanganyika na Wawekezaji wa miaka yake.
Makaa ya Mawe yanaoza? Au sio
 
Makaa ya Mawe yanaoza? Au sio
CCM hawafahamu bei ya Coal na hawana hasara hata ikichukuliwa na wajanja watoa Rushwa za kampeni zao.Mwalimu Nyerere alizilinda hizi raslimali zetu lakini CCM mpya hawana nia hiyo.
Wanachowaza ni kubaki madarakani bila kujali wanachohitaji wananchi.
Bila Katiba Mpya nchi hii haiwezi kutoka hapa ilikokwama.
 
Salaam wakuu,

Hivi karibuni tumeshuhudia Meli zikianza kubeba Makaa ya Mawe kutoka Mtwara. Watu wakadai Makaa ya Mawe Tanzania inayauza kwa kila tani moja ni Elfu sitini za kitanzania huku Soko la dunia kila tani ni Dola 300 zaidi ya laki saba za Kitanzania. Hivyo ikaonekana huu mkataba ni wa kifisadi.

Hivi Karibuni rais Samia Alitembelea Ubelgiji ambapo ndo Makao Makuu ya Kampuni inayohusika na Kununua Makaa ya Mawe ya Huko Ruvuma na Mtwara.

Je, Gesi yetu ya Mtwara na Mafuta ya Mtwara, hii Kampuni inahusika pia? Kipindi cha Nyumba Dr. Slaa na Magufuli kwa Wakati Tofauti walisema kwamba Mafuta na Gesi kutoka Mtwara hatuna Chetu kwani Mabomba yajengwa Baharini kuelekea Ulaya.

Kampuni inayomilikiwa na Ubelgiji iliyosajiliwa Hong Kong inayofanya biashara zaidi ya mafuta ya petroli, nishati na bidhaa za madini, Kemexon, inasimamia mauzo ya makaa ya mawe kutoka Ruvuma Coal, kusini magharibi mwa Tanzania, hadi Ulaya na Asia.

Tungependa Serikali iseme inavyouza Makaa ya Mawe kama Wanavyotaja bei ya Bamba, Kahawa na Alizeti. Mikataba inafichwa sana.. Ukilalamika wanasema leta mkataba sababu wanajua huwezi kuupata.

Pia, soma:

Thread 'Meli nyingine iliyobeba makaa ya mawe yaondoka kutokea Mtwara kwenda Ulaya' Meli nyingine iliyobeba makaa ya mawe yaondoka kutokea Mtwara kwenda Ulaya

Wasilisho lake ni la mtu asiye na uelewa kabisa.

1) Tangu lini Tanzania imekuwa inachimba mafuta? Unadhani mafuta yanachimbwa kama unavyochimba kifusi cha kujaza barabarani?

2) Ni ujinga mkubwa tena unaoelekea kwenye upumbavu kuamini kuwa eti kunaweza kuwa na mabomba chini ya bahari yanasafirisha mafuta (ambayo hatuchimbi) kupeeleka Ulaya. Au unadhani mafuta ni kama hayo maji ya bahari?

3) Bidhaa nyingi hupanda bei maradufu baada ya kupitia hatua fulani. Hizo hatua za kati ndizo zinazoongeza thamani. Wewe unafahamu coal inauzwa katika quality ipi,na hiyo unayosema inauzwa kwa dola 300 ni ya quality ipi?

Mwombe Dr. Matarajio au kijana wake mmoja akupe hata ile elementary kniwledge ya mafuta,nina hakika utajiona mjinga wa ajabu, na utataka hii thread yako usiwepo hapa. Msiwe mnaleta habari za vichochoroni JF.
 
Back
Top Bottom