Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,232
- 113,610
Usisahau kuwa ugaiidi wa siku za nyuma iulikuwa ni wa maslahi zaidi kuliko religious ideology. Osama ndiye ameingiza hili akitaka kuungwa mkono na kwa bahati mbaya tunaona mnavyomuunga mkono hata kwenye udhalimu usio na chembe za imani.
Kwa nini unanihusisha na wanaomuunga mkono Osama? Nini kimekufanya unihusishe na huyo muuaji? Kama maswali yangu yamekufanya unidhanie hivyo utakuwa umekosea sana.
Kama aliyekumbwa ni baba au mama yako, kaka au dada usingetamka haya.
Mimi nimeona nikiwa kazini Aug 1998, nimesikia kishindo na nimebeba majeruhi ndani ya hospitali. Inaniwia vigumu na napata uchungu sana kwa maneno yako. Ungemuona yule bibi aliyekuja kuchukua maiti ya kijana wake au yule mama aliyeaachwa na watoto mayatima, neno bahati mbaya ungeliona tusi.
Unanihukumu kimakosa sana. Maneno yangu yepi hayo yanayokupa uchungu? Daaah haya bana.