Kauli ya JK Kuipongeza Marekani kufuatia kifo cha Osama yaja? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli ya JK Kuipongeza Marekani kufuatia kifo cha Osama yaja?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 3, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 3, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Hii ni sehemu ya bango ambalo lilitolewa na FBI kuhusu "kutafutwa" kwa Osama Bin Laden. (Msisitizo wa rangi nyekundu wakwangu)

  [​IMG]

  Murder of U.S. Nationals Outside the United States; Conspiracy to Murder U.S. Nationals Outside the United States; Attack on a Federal Facility Resulting in Death


  USAMA BIN LADEN
  [​IMG]  Date of Photograph Unknown


  Multimedia: Images
  Aliases:

  Usama Bin Muhammad Bin Ladin, Shaykh Usama Bin Ladin, the Prince, the Emir, Abu Abdallah, Mujahid Shaykh, Hajj, the Director
  DESCRIPTION

  Date(s) of Birth Used: 1957

  Place of Birth: Saudi Arabia

  Height: 6' 4" to 6' 6"

  Weight: Approximately 160 pounds

  Build: Thin

  Occupation:Unknown

  Hair: Brown

  Eyes: Brown

  Complexion: Olive

  Sex: Male

  Nationality:
  Saudi Arabian

  Scars and Marks: None known

  Remarks:


  Bin Laden is the leader of a terrorist organization known as Al-Qaeda, "The Base". He is left-handed and walks with a cane.

  CAUTION

  Usama Bin Laden is wanted in connection with the August 7, 1998, bombings of the United States Embassies in Dar es Salaam, Tanzania, and Nairobi, Kenya. These attacks killed over 200 people. In addition, Bin Laden is a suspect in other terrorist attacks throughout the world.
  REWARD

  The Rewards For Justice Program, United States Department of State, is offering a reward of up to $25 million for information leading directly to the apprehension or conviction of Usama Bin Laden. An additional $2 million is being offered through a program developed and funded by the Airline Pilots Association and the Air Transport Association.

  CONSIDERED ARMED AND EXTREMELY DANGEROUS


  If you have any information concerning this person, please contact your local FBI office or the nearest American Embassy or Consulate.
  Field Office: New York
  June 1999
  Poster Revised November 2001

  Poster Classification: Ten Most Wanted Fugitives


  My Take:
  Sijui kama tumechelewa au bado tunafikiria tutoe kauli ya namna gani. Kwa ufupi ingetakiwa tuwe miongoni mwa watu wa kwanza kutoa pongezi kwani mhusika wa uhalifu ulioua Watanzania 11 hatimaye hayupo tena baada ya kukutwa na kile ambacho kwa miaka mingi alikuwa akiwalazimisha kwa kutumia mafundisho na sera zake kiwakute wengine.

  Ni matumaini yangu Rais atatoa kauli yeye mwenyewe kuelezea furaha ya Watanzania kuwa mhalifu nambari duniani amekutwa na haki. Haitaji kusema mengi au kuyapamba sana bali machache yenye kuonesha kuwa tunajalii kilichotokea.
   
 2. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,839
  Likes Received: 11,959
  Trophy Points: 280
  Mbona Kikwete tayari ameshatoa tamko ila anasema anaisikitikia familia yake.
  Kauli hii kwa tafsiri yangu ni kama Kikwete amesikitika sana lakini basi afanyeje.
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ameshatoa kauli
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  May 3, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  acha utani bwana!!!
   
 5. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
   
 6. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,839
  Likes Received: 11,959
  Trophy Points: 280
  Siku hizi yuko makini nafikiri kikombe cha babu kinatibu.

  Kikwete: Kifo cha Osama ahueni vita ya ugaidi
  (HabariLeo)
  RAIS Jakaya Kikwete amesema, ingawa mauaji ya kiongozi wa Mtandao wa kigaidi wa Al- Qaeda, Osama bin Laden si jambo la kufurahia, lakini yametoa ahueni katika vita dhidi ya ugaidi.

  "Huwezi kufurahia kifo cha mtu kwa kuwa tumefundishwa kupenda hata maadui zetu, lakini naweza kusema kutakuwa na ahueni," alisema Rais Kikwete.

  Akijibu swali juu ya mauaji hayo katika mkutano wa waandishi wa habari uliohusu maazimio ya Tume ya Umoja wa Mataifa ya Habari na Uwajibikaji wa Afya ya Wanawake na Watoto, Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alisisitiza kuwa alitarajia Osama akamatwe na kushitakiwa ili haki itendeke.

  "Mtu aliyekuwa akitafutwa ili ashitakiwe nimeambiwa hayupo tena ndiyo hivyo," alisema Rais Kikwete.

  Alikumbushia kuwa Agosti 7, 1998 Ubalozi wa Marekani nchini ulilipuliwa na Watanzania 11 wakauawa na siku hiyo hiyo karibu muda sawa, Ubalozi wa Marekani nchini Kenya nao ulilipuliwa.

  Kutokana na milipuko hiyo, Tanzania ilianzisha uchunguzi ambao Rais Kikwete alisema baadhi ya watu walihisiwa kuhusika, lakini mshukiwa mkuu alikuwa Osama.

  Katika uchunguzi huo kwa mujibu wa Rais Kikwete, mmoja wa watuhumiwa ambaye ni Mtanzania, alikamatwa nchini Pakistani na kufungwa katika Gereza la Guantanamo Bay nchini Cuba.

  Baadaye Mtanzania huyo, Mohamed Ghailani, alifikishwa mahakamani nchini Marekani ambako Rais Kikwete alisema haki ilitendeka.

  Jumatatu , Rais Barack Obama wa Marekani alitangaza kifo cha Osama, ikiwa ni takribani miaka 10 baada ya shambulizi la ugaidi lilitokea Septemba 11, mwaka huu Marekani na kuua zaidi ya watu 3,000.

  Kutokana na taarifa hiyo ya kushtukiza viongozi mbalimbali duniani wamempongeza Obama kwa ushindi na kifo cha kiongozi huyo na kuuita ushindi huo kuwa ni wa kihistoria.

  Katika hotuba yake aliyoitoa juzi usiku, Obama alisema katika operesheni iliyofanywa na Marekani wamemuua kiongozi huyo wa al-Qeda nchini Pakistan na kuuweka mwili wake chini ya ulinzi.

  Mapema Jumapili Marekani ilizindua operesheni yake dhidi katika eneo la Abbottabad nje ya mji mkuu wa Pakistan, Islamabad na baadaye kuthibitisha kuwa Osama ni mmoja kati ya magaidi waliokufa katika mapigano hayo, alisema Obama.

  Vyanzo vya habari vya Pakistan vimethibitisha kutokea kwa kifo hicho cha Osama, hali ambayo Obama ameiita ni moja kati ya mafanikio makubwa ya Marekani na kwamba muda mfupi baada ya kuwa Rais mwaka 2009, alimtaka Mkurugenzi wa Shirika la Upelelezi nchini humo kuweka suala la kukamatwa ama kuuawa kwa Osama kipaumbele.

  Alisema Marekani ilipata taarifa za kumfuatilia Osama tangu Agosti mwaka jana na kufanya tathmini ambapo walibaini kuwa alikuwa amejificha ndani ya Pakistan na kwamba kwa kushirikiana na Pakistan wamemuua kiongozi huyo pamoja na mtoto wake wa kiume, mwanamke mmoja na wafuasi wake watatu.

  Aidha, katika operesheni hiyo iliyohusisha helikopta nne na kuchukua takribani saa mbili, watu 12 wakiwemo watoto sita, wanawake wake wa Osama wawili na marafiki zake wanne wa karibu wamekamatwa.

  Osama ambaye alizaliwa nchini Saudi Arabia mwaka 1957, amekuwa akifahamika kama kiongozi wa kundi la ugaidi duniani kote na kuhusishwa na matukio mbalimbali ya mashambulizi nchini Marekani likiwamo la Septemba 11, 2001.

  Kwa mujibu wa Ofisa Mwandamizi wa Marekani mwili wa Osama umezikwa baharini kwa kufuata sheria na taratibu zote za Kiislamu.

  "Hili ni jambo tunalolipa kipaumbele na ndio maana tumefuata taratibu zote," alisema.

  Muda mfupi baada ya kutangazwa kifo cha Osama, Msemaji wa kundi la Taliban nchini Pakistan lilikanusha taarifa hizo na kudai kuwa bado Osama yuko hai.
   
 7. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,056
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  [​IMG] kikwete.jpg
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  May 3, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Chamoto sijaona akiatoa pongezi kwa Wamarekani kwa kufanya kazi ambayo sisi hatukuwa na uwezo wa kuifanya.
   
 9. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,056
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Nimekuelewa! Ni kwamba hakutoa shukrani, sivyo?
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  May 3, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  hakutoa pongezi na kuwatia shime watu wetu wenyewe. Labda hilo swali hapo juu niliandike kwa lugha gani sijui...
   
 11. The Stig

  The Stig JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 880
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80
  MMKJJ, tuko kwenye frequency moja.

  Tanzania ilipaswa kuwa mstari wa mbele kumsaka osama na pale alipouwawa, ingepaswa kuwa nchi ya kwanza kabisa kushangilia. Watu wengi hawaelewi, lakini Tanzania ilionja adha ya osama hata kabla ya marekani.
   
 12. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #12
  May 3, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Kikwete hawezi kupeleka salamu zozote za pongezi kwa Obama au serikali ya Marekani kwa vile bado ana donge kuwa walimchunia uchaguzi wake wa chakachua
   
 13. Chamoto

  Chamoto JF-Expert Member

  #13
  May 3, 2011
  Joined: Dec 7, 2007
  Messages: 2,056
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Nimekupata mkuu.
   
 14. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #14
  May 3, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Nadhani swala la "uislamu" pia linachangia Kikwete kukaa kimya - Sehemu kubwa ya waislam (fundametalist) hawajapendezwa na hiki kitendo - and I think Kikwete would not want kuona maandamano ya Sheikh Ponda(s) pale Magomeni
   
 15. W

  WildCard JF-Expert Member

  #15
  May 3, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Ninachojiuliza siku zote ni kwamba maamuzi ya George Bush na mshirika wake Tony Blair kuivamia Iraq na hatimaye watu wengi kufa na wanaendelea kufa yana tofauti gani na maamuzi ya Osama juu ya Wamarekani na washirika wao wa Magharibi?
   
 16. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #16
  May 3, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Sijajua nasumbuliwa na nini moyoni mwangu lakini nafsi yangu inanilazimisha kutopendezwa na mauaji ya OSAMA, na hata Sadam alipokuwa hanged ilinihuzunisha pia. I feel like Dunia inakosa kitu fulani.
   
 17. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  kweli. Dunia inakosa kitu kiitwacho uadilifu. Osama,sadam na wenzie walikosa uadilifu ndo maana hata hawa marekan,pakistan na wenzao wamekosa uadilifu na kuamua kumtoa roho mwenzao osama. Hamna anayependa kuua mwenzie lakini alivofanya osama anastahili kuwajibishwa kwa kufuata vitabu vitakatifu anavyoviamini! Kila afanyaye maovu atalipwa. Hongera Marekani kwa kupunguza ugaidi ktk dunia ya leo! Osama must not be killed but must have died,and must die. Burian Osama!
   
 18. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #18
  May 3, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,736
  Likes Received: 1,447
  Trophy Points: 280
  My Take:
  Sijui kama tumechelewa au bado tunafikiria tutoe kauli ya namna gani. Kwa ufupi ingetakiwa tuwe miongoni mwa watu wa kwanza kutoa pongezi kwani mhusika wa uhalifu ulioua Watanzania 11 hatimaye hayupo tena baada ya kukutwa na kile ambacho kwa miaka mingi alikuwa akiwalazimisha kwa kutumia mafundisho na sera zake kiwakute wengine.

  Ni matumaini yangu Rais atatoa kauli yeye mwenyewe kuelezea furaha ya Watanzania kuwa mhalifu nambari duniani amekutwa na haki. Haitaji kusema mengi au kuyapamba sana bali machache yenye kuonesha kuwa tunajalii kilichotokea.[/QUOTE]


  Heshima kwako MM,

  Hapo ndipo mara nyingi unafikia kujiuliza kama Tz kweli ni nchi yenye maono ya mbele, au kama ina viongozi wenye uwezo, au hata kuwa na ethos za uongozi. Kimataifa huwa (naendelea kuchunguza) haina rafiki ukiondoa China, Russia na India. Hata hapo EA marafiki zake ni wachache sana. Naifananisha na Pakistan na Saudia zilivyo kwa America, ila kwa Tz ni umaskini wao tu ndio unawafanya wailaghai America kwa kujipendekeza.

  Na pia ni vizuri wakibaki kimya maana naelewa vizuri. Wakiongea wataharibu.
   
 19. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #19
  May 3, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  HTML:
  
  
  Inawezekana kweli alistahili kuuwawa, lakini pia ulimwengu ulikuwa na haki ya kusikia kile ambacho Osama alikuwa anakipigania, Osama alikuwa anastahili kupelekwa kwenye mahakama huru za kimataifa kama ICC ili haki itendeke. kuuwa ni kuuwa na ni dhambi kubwa, naungana na wewe kwamba wote wamekosa uadilifu, lakini nani atawashtaki kina Obama na washirika wake kwa kufanya hii dhambi ya mauwaji? Au ni kwa sababu wao ni wakubwa kwa hiyo wamefanya haki kuuwa? Unyonge na umaskini wetu ndiyo unatufanya tupongeze mauwaji ya Osama. (Siungi mkono ugaidi lakini pia siungi mkono hatua ya marekani kuua ili hali walikuwa na uwezo wa kumkamata akiwa hai)
   
 20. Mshindo

  Mshindo JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2011
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 479
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwenye red hapo weeeeee!!! Unadhani ni rahisi sana eeh? Huwezi kuwa serious ukam-under estimate mtu kama yule. Wamemtafuta kwa karibu miaka ishirini huyu. Sidhani hata kama angekua radhi wamguse akiwa hai. Infact inawezekana alijimalizia kabla hawajamkamata.
  Kivita,priority inakua ni kumkamata akiwa hai,lakini kama mtu ni armed na ni hatari, order level inaongezeka na kuwa shoot-on-site. Osama ni casualty of war kwahiyo huwezi kuishitaki mahakamani marekani kwa kosa la kuua, unless useme haikua halali hata kumtafuta. Kwa niaba ya.....ninatoa pongezi za dhati kwa amiri mkuu,vikosi vya marekani na washirika zake kwa kufanikiwa kumuua kiongozi huyu wa ugaidi duniani.
   
Loading...