Kauli ya Godfrey Mgimwa kwa wana KALENGA

hata mimi nimemsikia akiyasema hayo, busara ya kawaida tu wamuulize kwa mshahara wake mzuri na maisha yake mazuri huko ulaya, nini amewahi kufanya kwa wana-kalenga?
Hapo kwenye BLUE hilo ni swali zuri sana kama lingeulizwa lakini kwa jinsi ilivyo hakuna sehemu ambayo hawa jamaa wanaruhusu maswali na nafikiri wanajua wazi kama wakiruhusu issue ya maswali Mgimwa hawezi kujibu na isitoshe shujaa atakayejitokeza kuuliza swali lolote gumu inawezekana kabisa ndio ukawa mwisho wake kwani kinara wa Ugaidi ndani ya siasa za Tanzania ndie anayeendesha kampeni kwa upande wa CCM.
 
Wakati huohuo Mh. Chris Lukos amegoma kuacha kubeba box kule ULAYA. Kwlei wana Iringa ni Ulaya Ulaya tu.
Pia Chriss Lukos anaogopa kuja Tena Tanzania na hususani kwao Iringa kwa kuwa amekula fedha za lambilambi za Marehemu mwangosi.
 
Hata lisu naye alishasemaga alikuwa Ulaya na alikuwa analipwa Mshahara mzuri ulaya, Kwa Mgimwa leo imekuwa ni ajabu? Acheni kudanganya wananchi , watu wanataka maendeleo waacheni waamue wenyewe.
 
siasa mchezo mchafu sana. eti ameacha maisha mazuri ulaya. pumbaaaaaaaaf, hiyo nayo ni point?
unaweza kukuta alikuwa bank teller tu halafu anawadanganya watu hapa.
 
Umbea huu tafuteni hoja za maana za kushindana na mgimwa japo naamini hamtaweza kabisa dogo yuko vizuri sana.
Mtu ameishi muda mwingi ULAYA, umeyajua saa ngapi matatizo ya wanaKalenga?
Wanaweza wakamchagua halafu muda mwingi wa ubunge wako akawa anaenda kukaa ULAYA, si amezoea ULAYA?
 
Nawashauri wana Kalenga mumchague Grace Tendega mwana Mama mahiri atawasaidieni sana. msijali Chama huyo Mama ni maakini sana. Achaneni na Jamaa, nimeishi ulaya, Nimefanya kazi kwenye moja ya Benki kubwa duniani, nimeacha mshahara mkubwa huko Ulaya. Haya ni matusi kabisa. Chagueni mwenzenu mliyekuwa mnaishi naye MAMA GRACE TENDEGA.
 
Hata lisu naye alishasemaga alikuwa Ulaya na alikuwa analipwa Mshahara mzuri ulaya, Kwa Mgimwa leo imekuwa ni ajabu? Acheni kudanganya wananchi , watu wanataka maendeleo waacheni waamue wenyewe.

huyu Mgimwa Ulaya hakuwa na kazi, alikuwa cheki bob tu mtaani. myoyo wa baba
 
Back
Top Bottom