Kauli ya Ex wangu ilibadili maisha yangu

Bullshit

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
1,300
1,495
Miaka tano hivi imepita baada ya Ex wangu kuniambiea ‘’nisiwe nang'ang'ania vitu vyenye thamani ya gari wakati hata spea ya piki piki sina”.

Mwana JF kauli hii aliniambia Ex wangu baada ya kuniona mimi sina kipato cha kukizi mahitaji yake na aliniomba tuachane maana tunapotezea muda tu.

Nilikuwa namng'ang'ania asiwe mtu wa maamuzi ya haraka lakini alikataa na alipoona namsumbua sana ilibidi anipe dose yangu kuwa “nisiwe nang'ang'ania vitu vyenye thamani ya gari huku sina hata spea ya piki piki, alienda mbali akisema tafuta kwanza pesa ukiwa na pesa utaepukana sana na usumbufu wa wadada,utaepuka kuongea sana au kumbembeleza sana mwanamke unaemuhitaji.

Akazidi kusema wanawake wanatabia moja ukitaka apatikane kirahisi wewe fanya kumshawishi kimatendo na sio maneno.

Mwambie niko malaika beach au tukutane rock beach,atakupa jibu la ndio hata kama ujaeleza shida yako na sio zile promise za tukutane chini ya mti, jua utadhaulika kabla ya...na ukitaka kuamini we tafuta pesa.

Halafu huoni kwanza pesa zitakupa kajeuri fulani hivi kwa mwanamke tofauti kabisa ikiwa huna kitu na ni wanawake wachache sana ambao wanaweza kukuvumilia akiona maybe siku moja utatoboa na mambo yatakuwa sana”

Kauli hii nilihisi kuwa amenidharau mpaka mwisho niliona isiwe case nikaachana nae.

Kauli yake kimaneno nilipinga ila kimoyo moyo nikaikubali na ndio siku nilianza kutafata pesa na kutunza pesa kwa makini tofauti na zamani nilikuwa natafuta pesa ya kodi na soda basi na sikuwa na ndoto yakumilki nyumba gari au vitu fulani hivi vya kunipa mafanikio.

MREJESHO: Baada ya kuanza kutekeleza kauli ya Ex wangu nilianza kuwa na ndoto ya kufika mbali sana kimaisha na kila nilipokuwa nakumbuka kauli hii ndipo nilikuwa nafanya juhudi za kufanikisha shughuli zangu ili mambo yakae sawa.

Saivi mambo swari yamenyooka na nimeachana na zile ahadi za tukutane chini ya mti, na kweli nimeamini asilimia kubwa ya wanawake wanapenda kushawishiwa sana na vitu vidogo vidogo na ukiwa na pesa hawana lolongo.

EX wangu huwa namtafuta nimpe hongera lakini kwa bahati mbaya sijawahi kukutana nae na namba zake nilifuta baada ya kunipa DOSE.

Kijana mwenzangu tafuta pesa.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Angalia zisiishe ukakutana na X ukiwa huna kitu ukaanza maneno mengi kama unajua nilitusua ila sasa sikukutana na wewe, yaani kama tungekutana miezi sita iliyopita bla bla bla.. Nakwambia hivi maana inaonekana unazitafuta kumprove x wako wrong, pia ombea asiwe amepanda viwango na si yule uliyemwacha
 
Wewe ni kama kenge,husikii mpaka masikio yatoe damu. Huoni umuhimu wa kutafuta pesa mpaka uambiwe na mtoto wa kike,ndio maana amekukimbia. Angekuona una juhudi angevumilia kidogo ajue labda zitakuja.
 
Angalia zisiishe ukakutana na X ukiwa huna kitu ukaanza maneno mengi kama unajua nilitusua ila sasa sikukutana na wewe, yaani kama tungekutana miezi sita iliyopita bla bla bla.. Nakwambia hivi maana inaonekana unazitafuta kumprove x wako wrong, pia ombea asiwe amepanda viwango na si yule uliyemwacha

No sina mashindano naye mkuu ila tu alinipa motisha


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom