Kuna ubaya kumwambia ex girlfriend wangu kwamba asinitafute maisha yake yote yaliyobaki?

Mbishi 4 real

JF-Expert Member
Jan 16, 2014
616
548
Kuna ex girlfriend wangu mmoja kwasasa tupo mikoa tofauti ingawa hakuna umbali sana katika ya mkoa aliopo yeye na mimi.

Simuhitaji tena na ndio maana hata naweza nikakaa hata miezi mitatu au sita bila kumtafuta na namba zake za simu nilishafutaga na kichwani pia hazipo mana sina kawaida ya kukalili namba za mpenzi wangu ninaekua nae kwenye mahusiano.

Tatizo huyu binti ndie huwa ananitafuta mimi hata tukikaa miezi mitatu au sita lazima atanitafuta wakati mimi sina time nae tena.

Juzi alinitafuta na kunisalimia na nikamjibu fresh tu ila nikaona nimuweke wazi kwa kumuambia kwamba asinitafute katika kipindi chote cha maisha yake yaliyobaki mana ni kama atakua anajipotezea tu muda wake wakati mimi sina interest nae tena.

Nimemwambia hivyo just for good ili aweze ku focus zaidi kwenye maisha yake.

Je kwa kufanya hivyo nitakua nimekosea kumchana ukweli ili asipoteze muda wake au nitakua nimeupiga mwingi?
 
Kitendo cha wewe kupokea simu Inamaana kwamba wewe unampenda...

Ungekuwa humpendi usingepokea...
Huwa ananitext tu na huwaga nazijibu text zake kwa ufupi sana, ni busara tu huwa naonyesha lakini sio kama namuhitaji tena ukizingatia tayari nina mtu mwingine, ili asiniharibie ndio maana nimeona nimkataze mazima yeye kunitafuta.
 
Hahahahah wewe kama unaijua namba yake ipige tofali tu ili asikupate kabisa. Ila pia kama kuachana kwenu hakukuwa kwa ubaya sioni sababu ya kumpiga life ban hata ya kukutafuta. Haya maisha tunayoishi penda sana kujenga ujamaa kuliko uadui hasa kwa nchi zetu hizi za ulimwengu wa 3 wa dunia.

Ipo siku usioijua huyo demu anaweza kukufaa kwa namna moja ama nyengine. Mimi kuna watu nimeachana nao ila naweza kuwapigia any time na tukaongea freshi sababu tuliachana katika ukomavu tu sio kwa sababu za kishenzi. Ila kama mliachana kwa bifu basi haina budi kuendelea mlipoishia.
 
Back
Top Bottom