Kauli ya Ex wangu ilibadili maisha yangu

Kauli ya Ex wangu ilibadili maisha yangu

Miaka tano hivi imepita baada ya Ex wangu kuniambiea ‘’nisiwe nang'ang'ania vitu vyenye thamani ya gari wakati hata spea ya piki piki sina”.

Mwana JF kauli hii aliniambia Ex wangu baada ya kuniona mimi sina kipato cha kukizi mahitaji yake na aliniomba tuachane maana tunapotezea muda tu.

Nilikuwa namng'ang'ania asiwe mtu wa maamuzi ya haraka lakini alikataa na alipoona namsumbua sana ilibidi anipe dose yangu kuwa “nisiwe nang'ang'ania vitu vyenye thamani ya gari huku sina hata spea ya piki piki, alienda mbali akisema tafuta kwanza pesa ukiwa na pesa utaepukana sana na usumbufu wa wadada,utaepuka kuongea sana au kumbembeleza sana mwanamke unaemuhitaji.

Akazidi kusema wanawake wanatabia moja ukitaka apatikane kirahisi wewe fanya kumshawishi kimatendo na sio maneno.

Mwambie niko malaika beach au tukutane rock beach,atakupa jibu la ndio hata kama ujaeleza shida yako na sio zile promise za tukutane chini ya mti, jua utadhaulika kabla ya...na ukitaka kuamini we tafuta pesa.

Halafu huoni kwanza pesa zitakupa kajeuri fulani hivi kwa mwanamke tofauti kabisa ikiwa huna kitu na ni wanawake wachache sana ambao wanaweza kukuvumilia akiona maybe siku moja utatoboa na mambo yatakuwa sana”

Kauli hii nilihisi kuwa amenidharau mpaka mwisho niliona isiwe case nikaachana nae.

Kauli yake kimaneno nilipinga ila kimoyo moyo nikaikubali na ndio siku nilianza kutafata pesa na kutunza pesa kwa makini tofauti na zamani nilikuwa natafuta pesa ya kodi na soda basi na sikuwa na ndoto yakumilki nyumba gari au vitu fulani hivi vya kunipa mafanikio.

MREJESHO: Baada ya kuanza kutekeleza kauli ya Ex wangu nilianza kuwa na ndoto ya kufika mbali sana kimaisha na kila nilipokuwa nakumbuka kauli hii ndipo nilikuwa nafanya juhudi za kufanikisha shughuli zangu ili mambo yakae sawa.

Saivi mambo swari yamenyooka na nimeachana na zile ahadi za tukutane chini ya mti, na kweli nimeamini asilimia kubwa ya wanawake wanapenda kushawishiwa sana na vitu vidogo vidogo na ukiwa na pesa hawana lolongo.

EX wangu huwa namtafuta nimpe hongera lakini kwa bahati mbaya sijawahi kukutana nae na namba zake nilifuta baada ya kunipa DOSE.

Kijana mwenzangu tafuta pesa.



Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe ni dhaifu na mkaidi. Wazazi wako unawatunza vyema!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kitu tunakosea sana.
Tunajaribu kuwachagulia watu aina ya maisha tuyapendayo sisi au wafuate malengo yetu.

Kila mtu ana malengo flani maishani, na anapofikia malengo yake yeye huyaita mafanikio.

Mfano;
Mimi ninapenda sana kununua ardhi na kuhenga, tamaa yangu nijenge nyumba nyingi niwezavyo na kila mkoa palipo na uhitaji wa nyumba za kisasa za kupangisha.
Nyumba za kawaida na hata za juu/ghorofa.
Sababu kuu ya kupenda biashara hii zinapanda thamani kila siku

Pili nina penda magari mazuri ya kutembelea na ya biashara.
Ninapoweza kumudu haya kwangu ni MAFANIKIO

LAKINI
Kuna watu wanapenda wawe na mapesa mengi kusudi wang'oe mademu wakali, siwezi kuwalamu sababu hayo ndiyo malengo yao na kwao ni MAFANIKIO


Your ex, she was very smart. She told you the plain truth. Find purpose and meaning of life beyond women.

"Saivi mambo swari yamenyooka na nimeachana na zile ahadi za tukutane chini ya mti, na kweli nimeamini asilimia kubwa ya wanawake wanapenda kushawishiwa sana na vitu vidogo vidogo na ukiwa na pesa hawana lolongo" …from this statement, it is clear that you learned nothing from that encounter. Your head is still wrapped around "
Mwambie niko malaika beach au tukutane rock beach" instead of bettering yourself.

You are still glued at impressing women instead of bettering yourself.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mapenzi ni multidimensional sana, kuna baadhi ya wanawake hata ukiwa na hela yako hataki umuendeshe eti kisa tu una hela. Big no na nafikiri wanawake wa hivyo ni wasiojitambua pia same to men eti hela yako iwe kigezo cha mahusiano bora. Nina mwanamke wangu haniulizi kuhusu hela wala nini na hataki ujinga ujinga eti nimtreat vyovyote tofauti na uhuru wake kisa pesa. She need transparent, understanding and respect to each other. Na kiukweli huyu mwanadada kanifundisha mengi
 
Hiii nitrue nakumbuka 2015 nikiwa chuo flan nilikua kilanaemtongoza ananpiga chni nilipoanza mbishe zakuuza mazagazaga nikajulikana kiladem alikua anajisogeza alafu nagingatuu ilaela hapatiii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Change transparent to transparency
Mapenzi ni multidimensional sana, kuna baadhi ya wanawake hata ukiwa na hela yako hataki umuendeshe eti kisa tu una hela. Big no na nafikiri wanawake wa hivyo ni wasiojitambua pia same to men eti hela yako iwe kigezo cha mahusiano bora. Nina mwanamke wangu haniulizi kuhusu hela wala nini na hataki ujinga ujinga eti nimtreat vyovyote tofauti na uhuru wake kisa pesa. She need transparent, understanding and respect to each other. Na kiukweli huyu mwanadada kanifundisha mengi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom