Kauli Ya Ehud Barak Si Tu Ya Kupuuzwa, Bali..... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli Ya Ehud Barak Si Tu Ya Kupuuzwa, Bali.....

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by maggid, Dec 31, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Dec 31, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Nimefuatilia michango ya waliotangulia. Nami mtazamo wangu ni huu; Kauli ya Ehud Barak si tu ya kupuuzwa. Bali, Tanzania , kama taifa, iliweke wazi hilila upuuzi wa Barak kwa Serikali ya Israel na kwa njia za Kidiplomasia ili Israel kama nchi ielewe upuuzi uliotamkwa na Waziri wake.  Ni kauli ya dharau kubwa kutoka kwa waziri wa taifa ambalo lingeweza kuwa jirani zetu kama League of Nations ingeendelea na hoja ya kuwatafutia Waisrael waliokuwa wakitangatanga duniani ardhi ya kujishikiza baada ya Vita Kuu ya Dunia. Uganda ilikuwa tayari kutoa sehemu ya ardhi ya nchi yake kuwasitiri Wayahudi.

  Kwa kutambua ukweli huu wa kihistoria na kauli hiyo ya Barak. Hivyo basi,Tanzania iitake Israel ituombe radhi. Kinyume cha hapo, Tanzania ina uwezo wa kupambana na kushinda kwenye vita vya Kidiplomasia dhidi ya Israel. Na nia na sababu za kufanya hivyo tutakuwa tunazo. Ndipo hapo ndipo Israel itatambua kuwa Tanzania is relevant.

  Nawasilisha.

  Maggid Mjengwa,
  Bagamoyo.

  Desemba 31, 2011
  Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
   
 2. m

  matunge JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 60
  Anayeibariki Israel naye atabarikiwa na ailaaniye naye atalaaniwa!
   
 3. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2011
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwani walisemaje,mkuu? Sijaipata hiyo kauli tafadhali
   
 4. b

  busar JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2011
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Kwani mtu akikuambia "we mpumbavu" ilhali we unajua c mpumbavu, then ukamtaka akuombe samahani akakataa, unafanyaje? C kweli we mpumbavu? Unaonaje!
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Dec 31, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Jiulize enzi za Nyerere angethubutu kusema hayo uyo Ehud Barak?
  Current regime is not serious in everything!
   
 6. S

  Sheba JF-Expert Member

  #6
  Dec 31, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 210
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimependa mtazamo huu. Umejaa busara na hekima. Hauna pupa ba umeonyesha ukomavu.
   
 7. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #7
  Dec 31, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,986
  Likes Received: 3,735
  Trophy Points: 280
  we need some consistency here. unless of course the above "outburst" has been triggered by some "israel factor".

  why am i saying this?

  yupi utakayehitaji akuombe radhi zaidi na ukamkalia kooni hadi afanye hivyo kati ya hawa..... anayekwambia "you are irrelevant" (Israel) au yule anayekwambia "shika ukuta" (britain)?

  zaidi ya kuipinga kauli tu na kulalamikalalamika dhidi ya britain, sijamsikia mtu yeyote aliyewataka watutake radhi (sisi tukiwa ni beneficiaries wakubwa tu wa grants/loans kutoka britain, this barb was aimed rightly at us amongst many like us!).

  so why pick on israel now before settling the britain score first?
   
 8. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #8
  Dec 31, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Na Habari hii sio ya kupuuzwa

  Canada has always spat on the face of Tanzanians!” read a line on a mail from one of my friends after I circulated the article which publicised the deportation of Canadian diplomat who spat at the police personnel in Tanzania. But spitting on one’s face does not equal the untold story of the 13 year old girl who was forced to have sexual intercourse with a dog in the hands of Barrick Gold Corporation in Sengerema District – Tanzania.
   
 9. d

  dotto JF-Expert Member

  #9
  Dec 31, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Heshima ya nchi hujengwa kwa mifano hai ya watu wake. Nchi hii yote ni ya wageni wachumaji. Wakati inauzwa mbona hukusema. Kama imeuzwa umaana wake uko wapi? Bora Ehud kuliko mawazo yako. Nchi hii hata chaguzi zake ni uji-nga mtupu. Yaliyojiri igunga ni ushetani mtupu. Hatuna heshima kama Taifa. Mfano: change ya Rada ni uji-nga tu!
   
 10. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #10
  Dec 31, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  ehud barak amejibu mapigo,chokochoko zilianzishwa na sisi.mara leo watu wameandamana kuwasupport wapalestina,mara kesho watanzania wanafuturu kwenye ubalozi wa palestina.membe kwa mara kadhaa ametoa kauli dhidi ya israel,kwa vyovyote vile israel hawakufurahishwa na kauli au vitendo vyetu na hivyo wanajibu mapigo.sioni haja ya kulalamika kama vipi tuendeleze vita ya kidiplomasia.
  hapa tunapata funzo kuwa kiherehere hakitakiwi bado tuna mambo mengi ya kuyaongelea na sio mashariki ya kati,libya,zimbabwe n.k
  tufunge midomo na tuongee kwa maslahi ya tanzania tu.
   
Loading...