Uchambuzi: Ziara ya Makamu Rais wa Marekani, Kamala Harris ina faida gani kwa Tanzania?

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
09c8f913-22ac-457c-adb1-04b5d8d49a4e.jpg
Tanzania ina ugeni wa Makamu Rais wa Marekani, Kamala Harris ambaye amefika akiwa katika ziara yake ya Nchi kadhaa Barani Afrika, ambapo pia ratiba yake ni kupita yatika mataifa ya Ghana na Zambia.

Kitendo cha kioongozi huyo ambaye taifa lake lina nguvu kubwa Duniani kuichagua Tanzania kuwa moja kati ya mataifa ambayo anayatembelea kimepokelewa katika mitazamo tofauti.

Wapo ambao wanaitazama kama ni ziara chanya katika pande zote mbili na wapo ambao wanaona inaweza kuwa na faida kubwa kwa upande mmoja.

Nimefanikiwa kuzungumza na wachamuzi kadhaa na kuichambua ziara hiyo au ujio huo wa Kamala katika ardhi ya Tanzania na hoja ambazo wanafafanua ni:

Mpango.jpg
Ugeni huo una maana gani kisiasa kwa pande zote mbili? Una maana yoyote kiuchumi kwa Tanzania?

Ikumbukwe pia hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Anthony Blinken na mke wa Rais Joe Biden pia walitembelea Afrika, je, ziara zao nazo zilikuwa ni sehemu ya mkakati wa Marekani?

Na je, ziara hizo zina uhusiano wowote wa kupunguza nguvu ya China na Urusi katika masuala ya Kidiplomasia kwa Nchi za Afrika?

MAJID MJENGWA:
Marekani kuichagua Tanzania kuwa mmoja ya Nchi ambazo Kamala anatembela ni kutokana na kuona umuhimu wa juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan anazofanya kuweza kujenga ushawishi nje ya mipaka.

Mara nyingi inapotokea ziara kama hizo uamuzi wa kuchagua Nchi husika ya kwenda kuitembelea huwa inategemea na uhusiano uliopo kwa wakati husika.

Ziara ya Kamala ina faida kiuchumi na Kidiplomasia kwa pande zote, huu ni wakati ambapo Dunia imekumbwa na vuguvugu la vita ya Urusi na Ukraine, pia kuna China na Urusi nao wamekuwa na mikakati ya kuifikia Afrika kwa ukaribu.

Kutokana na mazingira hayo ya kimataifa ndio maana Marekani nayo imeanza kuona kuna umuhimu wa kuja Afrika ili kuendelea kujipambanua.

Kwa kawaida inapotokea Rais au Makamu wa Rais wa Marekani amefanya ziara nje ya Taifa lao, Dunia huwa inaiangazia Nchi husika na hata Wamarekani wenyewe wanaanza kuifuatilia nchi ambayo kiongozi wao ameelekea.

Naweza kusema kuwa hapo ndipo tunapoona umuhimu wa kitu kama Royal Tour ambayo ilifanywa na Rais Samia na kuzinduliwa Marekani.

Marekani ni taifa kubwa kiuchuni na wanaopenda kusafiri, hivyo kiuchumi ziara hiyo ya Kamale pia inaweza kuongeza watalii, upande mwingine ni kuwa hata wawekezaji nao wanaweza kusogea na kutaka kujua fursa zilizopo hapa Nchini.

Tanzania tunatakiwa kutumia nafasi hii kama fursa kubwa kwa ajili ya kuongeza kitu kwenye uchumi wetu.

Lakini katika jicho lingine ziara hiyo inaweka ushawishi wa kufanya kazi na Wamarekani kwa kuwa China ni moja ya Taifa ambalo limetengeneza ngome ya kujitanua kiuchumi katika Nchi za Afrika.

LUQMAN MALOTO:
Nchi ilikuwa inapitia kipindi kigumu wakati wa utawala uliopita ndio maana hakukuwa na kiongozi mkubwa kutoka Marekani ambaye alikuja Nchini.

Kama unakumbuka mazingira yalivyokuwa ilifika hatua hadi aliyekuwa DR wa Dar es Salaam akawekewa pingamizi la kuingia Marekani na Wamarekani wenyewe.
00cddb30-389a-4fd7-bef5-8213ae662e8e.jpg

Rais Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo Rasmi na mgeni wake Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Ujuo wa Makamu wa Rais Kamala ni kama tabasamu kati ya Marekani na Tanzania.

Rais Samia ameifungua nchi na ameondoa migogoro, pia ni sehemu ya matunda ya kongamano la Desemba 2022 lililofanyika Washington DC ambapo Marekani iliahidi kuisapoti Afrika na kusisitiza kuhusu kusapoti viongozi Wanawake, hivyo kinachofanyika ni sehemu ya kutimiza kile walichokiahidi.

Makamu wa Rais Kamala ni Mwanamke wa kwanza kuwa katika nafasi za juu za uongozi Nchini Marekani kama ilivyo kwa Rais Samia Nchini Tanzania, hivyo hii ni historian inayowekwa katika kutekeleza kilichoahidiwa na Taifa hilo kubwa kiuchumi.

Pia Wamarekani wapo katika mchakato wa kupunguza ushawishi wa China katika Bara la Afrika na kutaka kushinda kuwa na nguvu ya ushawishi.

Nasema hivyo kwa kuwa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na mataifa mengi yanayokimbilia China kufanyabiashara na kuwekeza kwenye mambo mbalimbali, ongezeko la mpishano wa wafanyabiashara China na Afrika limekuwa likitishia kupunguza nguvu ya Marekani kama ‘Super Power’.

Kama hali itaendelea kuwa hivyo, Marekani imeona inaelekea kupoteza utawala wake wa kuwa Taifa lenye nguvu.

Pamoja na yote yanayoendelea katika ngazi ya kimataifa, sisi Tanzania hatuwezi kuegemea upande wowote,Mwalimu Julius Nyerere alitujengea mazingira mazuri ya kutofungamana na upande wowote, hivyo hata ujio wa Kamara sidhani kama unaweza kuwa chachu ya kugemea upande mmoja.

Msimamo wa kutoegemea upande mmoja umekuwepo kwa muda mrefu, tunaweza kushirikiana na Marekani lakini hiyo haitabadilisha ukweli kuwa mataifa yote ni rafiki kwetu na sidhani kama ziara ya Kamala inaweza badilisha hilo.

Kingine ni kuwa wakati wa utawala wa Donald Trump, Marekani iliisahau Afrika, ndio maana kumekuwa na ziara za viongozi wa juu wa Marekani hivi karibuni.

Siyo tu hao waliokuja bado naamini kuna uwezekano hata Rais Joe Biden mwenyewe kuja Afrika mwaka huu.
 
Back
Top Bottom