ustadhijuma
JF-Expert Member
- Jul 20, 2015
- 3,133
- 2,117
Askofu Josephat Gwajima ameendelea kudhihirisha chuki zake dhidi ya Uislamu, msimamo aliokuwa nao tangu enzi za Rais Jakaya Mrisho Kikwete na ambao sasa ameuhamishia kwa Rais Samia Suluhu Hassan.
Si mara moja wala mara mbili ambapo Gwajima ametumia majukwaa ya dini na siasa kutoa kauli zenye ubaguzi wa kidini.
Katika moja ya video zake enzi ya utawala wa Kikwete, Gwajima aliwahi kusema hadharani: “Uongozi wa Kikwete ndiyo ulikuwa wa mwisho kufuga majini Ikulu.”
Kupitia kauli hiyo, alijaribu kupandikiza fikra potofu kuwa Rais Kikwete, kwa kuwa Muislamu, alikuwa mshirikina na mfuga majini.
Si hilo tu, aliwahi pia kusema kuwa “dini ya Kiislamu ni dini ya uchawi na majini.” Kauli ya uchochezi inayolenga kuchafua taswira ya dini hiyo.
Gwajima pia aliwahi kutamka kuwa ana ndoto ya “kugeuza misikiti yote kuwa shule za Sunday Schools” akisisitiza kuwa hatafariki kabla ya kutimiza ndoto hiyo.