Kauli tata Mei Mosi 2019

Kauli tata Mei Mosi 2019

Trust me Pakawa... We are done...
Kuongoza taifa lililofanya makosa ya kuwa na majaribio ya uongozi wa nchi inahitaji karama, ujasiri, ushupavu, huruma hata ukatili ikibidi..awamu zilizopita ama kwa kujua au kutokujua ziliwafanya watanzania kuwa watu wa aina hii; wabinafsi, wapenda starehe, wavivu, wanafiki, wanapenda short cut, wanapenda vitu rahisi, hawataki kufikiri, WALALAMISHI, wasiopenda kujitoa(kusacrifice) kwa ajili ya manufaa siku za usoni, hawana uvumilivu..nk na hapa nina maana ya kuanzia awamu ya pili yaani uongozi baada ya Mwl. kuongoza watu wa aina hii ukitaka ufanikiwe ajenda ya maendeleo, na hasa ukiangalia kwa upeo wa mbali kdg ni vyema kutosikiliza lawama na kilio fake..Mtumishi wa Mungu Musa kama tunavyosoma kutoka maandiko matakatifu, alishindwa kuiona nchi ya ahadi kutokana na makwazo yaliyosababishwa na lawama nyingi na kukosa shukurani kwa anaowaongoza, akateleza akamkosea Mungu pakubwa! Ni jambo la msingi sana kumuombea Mh. Rais kwa kuwa anaongoza taifa lililoharibiwa kwa kiwango kikubwa ndani ya mioyo, akili na matarajio yao, hata kama kwa nje wanaonekana watu wenye ustawi na kusifia awamu zilizopita lakini uharibifu uliotokea kwa mtu wa ndani (kila binadamu ana mtu wa nje na wa ndani, mtu wa ndani ndiye anaelekeza mtu wa nje)kwa kila mmoja wa watanzania ni mkubwa sana!! wengi hawana maarifa haya ni ubishi tu unaoongozwa na uchoyo, tamaa na ubinafsi..wanaofahamu habari hii hawachoki kumuombea Rais kwa sababu ni wajibu ili taifa liendelee kuwepo na kustawi kama aliyeliumba anavyotaka. Kutopandisha mishahara hadharani hata kama ni kwa miaka yote kumi atakayokaa madarakani hakufanyi maisha yetu kukosa thamani na matumaini, wapo wengi na mifano ipo mingi mahali tofauti tofauti waliopitia hali za kutisha, magonjwa, vita, mauaji ya kimbari, maafa ya asili nk kwenye maisha yao kama nchi..lakin leo wanafaidi mema ya nchi zao! mambo ya mishahara ni madogo sana kwa kutimiza lengo la kuumbwa kwako!
 
Sawa, lakini ajira za walimu ni za lazima kuliko hata za askari. Utabana matumizi ili uzalshe raia punguani, halafu hayo maendeleo yaendelezwa na nani. Kutoongeza mshahara si issue lakini shule ina walimu watatu wewe bize unanunua ndege. Punguani kama mapunguani wengine.
 
Basi kama wewe ulimwelewa kuwa alimaanisha hivyo, basi mimi nashauri apandishe mwaka 2025, mwishoni mwa kipindi chake cha pili, au wewe unasemaje?
Hata asipopandisha sawa tu. Tumeshajua kwamba anatuona sisi wote mabwege tu na hatuwezi kufanya lolote. Ila ipo siku. Hata Iddi Amini alijua atadumu muda wote lakini sasa imebaki Historia.
 
Sawa, lakini ajira za walimu ni za lazima kuliko hata za askari. Utabana matumizi ili uzalshe raia punguani, halafu hayo maendeleo yaendelezwa na nani. Kutoongeza mshahara si issue lakini shule ina walimu watatu wewe bize unanunua ndege. Punguani kama mapunguani wengine.
Waambie ndugu yangu. Watu hawajui. Taifa linajengwa na watu na siyo vitu. Duniani kote mataifa yaliyoendelea yalijikita kwenye maendeleo ya watu na siyo maendelea ya vitu. Yaani wewe ndani ya nyumba yako hupeleki watoto shule, huwanunulii chakula wala mavazi ila umekazana kununua magari, kujenga majumba, n.k. Huo ni ujinga uliopindukia. Serikali ya watu, inawekwa na watu, kwa ajili ya watu. Wenzetu wamebadilisha uhalisia sasa serikali ya vitu, inaangalia vitu, kwa ajili ya vitu. Bure kabisa. Ni heri usomeshe watoto, uwalishe vizuri, wavae vizuri, ukiwa kwenye nyumba ya kupanga.
 
Hivi may mosi ni kwa ajili ya nini ?
Mimi nilifikiri ni kwa ajili ya kuwapa faraja wafanyakazi kwa kuongeza mishahara, ajira,kupandisha madaraja, n.k lakini katika awamu ya tano naona watu wanasherekea sikuku may mosi kama vile wapo msibani badala tuone ni kama wapo harusini
 
Ni kama birthday kwa mtoto
 
Hata asipopandisha sawa tu. Tumeshajua kwamba anatuona sisi wote mabwege tu na hatuwezi kufanya lolote. Ila ipo siku. Hata Iddi Amini alijua atadumu muda wote lakini sasa imebaki Historia.
Watu tunatofautiana sana
 
Jiwe kanitoa kwenye mood kabisa.Acha niongeze juhudi katika shughuli zingine tu
 
Sawa, lakini ajira za walimu ni za lazima kuliko hata za askari. Utabana matumizi ili uzalshe raia punguani, halafu hayo maendeleo yaendelezwa na nani. Kutoongeza mshahara si issue lakini shule ina walimu watatu wewe bize unanunua ndege. Punguani kama mapunguani wengine.
Wafanyakazi wote wa serikali kwa nafasi zao ni wa lazima..hata wanaofanya usafi maofisin ni wa lazima! uchumi haujengwi na mtazamo wa kuona walimu ni muhimu zaidi ya muuguzi..wote ni muhimu!! nchi ina mahitaji yake na unapoamua kujenga nchi kupitia viwanda au madini au utalii kuna mahitaji yake pia, watanzania wanaoishi maeneo yaliyo na vivutio vya utalii wanajikimu kupitia ujio wa watalii, serikali inapata kodi kupitia watalii na hivyo kumudu kulipa watumishi wake wakiwemo walimu! unaongeza kuajiri walimu pesa za mishahara zitaongezekaje kama huongezi watalii pia??ndio maana ndege ni muhimu sababu ni nyenzo kuongeza namba ya watalii ili kuajiri walimu, wauguzi, wafanya usafi ofisini nk na kuweza kuwalipa stahiki zao.
 
Mkuu kaeleweka vZur Sana!mpaka atakapokuwa anakarbia kutoka madarakan,ko ni mwaka 2024!

sijui kajuaje kuwa uchaguz ujao atashinda!!siasa za bongo bwana!!!!
Kisha kamilisha teuzi za Wakurugenzi wa Wilaya .....!!
 
Waambie ndugu yangu. Watu hawajui. Taifa linajengwa na watu na siyo vitu. Duniani kote mataifa yaliyoendelea yalijikita kwenye maendeleo ya watu na siyo maendelea ya vitu. Yaani wewe ndani ya nyumba yako hupeleki watoto shule, huwanunulii chakula wala mavazi ila umekazana kununua magari, kujenga majumba, n.k. Huo ni ujinga uliopindukia. Serikali ya watu, inawekwa na watu, kwa ajili ya watu. Wenzetu wamebadilisha uhalisia sasa serikali ya vitu, inaangalia vitu, kwa ajili ya vitu. Bure kabisa. Ni heri usomeshe watoto, uwalishe vizuri, wavae vizuri, ukiwa kwenye nyumba ya kupanga.
..hicho chakula, mavazi unachodai huwanunulii vinakuja umelala usingizi??kama ni mkulima lazima ununue jembe, mbolea, mbegu hata muda wako nk ili hatimaye upate kipato cha kununulia watoto chakula, mavazi na waende shule, jembe, mbegu, mbolea haviji kama zawadi..lazima ununue! huo ndio msingi wa kuendelea, tusidanganyane hapa..kununua ndege, kujenga SGR, Kujenga mitambo ya umeme ni sawa na mkulima kununua vitendea kazi ili amudu kuhudumia familia yake!! labda kama ni mabishano tu na chuki zinazotokana na sababu zingine hatutaki kufahamu na kukiri ukweli ulivyo.
 
Nchi ngumu sana hii
Falsafa ya Mwl. watanzania kufuta ujinga anapohitimu darasa la saba kama akili ni ngumu basi kidato cha nne awe amefuta ujinga kichwani nadhani ilikoma miaka kadhaa nyuma, sasa hivi hata muhitimu wa ngazi ya chuo kikuu bado hajafuta ujinga, hili ni moja ya matatizo yaliyopo sasa kwa nchi hii. Kiwango cha ujinga ni kikubwa sana..watu wanaelimika vertically, horizontally ni ZERO!
 
Wafanyakazi wote wa serikali kwa nafasi zao ni wa lazima..hata wanaofanya usafi maofisin ni wa lazima! uchumi haujengwi na mtazamo wa kuona walimu ni muhimu zaidi ya muuguzi..wote ni muhimu!! nchi ina mahitaji yake na unapoamua kujenga nchi kupitia viwanda au madini au utalii kuna mahitaji yake pia, watanzania wanaoishi maeneo yaliyo na vivutio vya utalii wanajikimu kupitia ujio wa watalii, serikali inapata kodi kupitia watalii na hivyo kumudu kulipa watumishi wake wakiwemo walimu! unaongeza kuajiri walimu pesa za mishahara zitaongezekaje kama huongezi watalii pia??ndio maana ndege ni muhimu sababu ni nyenzo kuongeza namba ya watalii ili kuajiri walimu, wauguzi, wafanya usafi ofisini nk na kuweza kuwalipa stahiki zao.
Hao wote hawawezi kuwepo na kuzalisha bila elimu. Simaanishi wasiajiriwa la hasha. Lakini tatizo la walimu nchini ni kubwa kuliko tunavyoliona na kwa bahati mbaya athari zake huonekana baada ya kitambo sana. Kuna shule zina walimu wawili, watatu au wanne tu toka awali hadi la saba na hali inakuwa hivyo kwa zaidi ya miaka saba. Ina maana watoto hao wanapohitimu wanakuwa hawajfikia kiwangu cha elimu stahiki yaani la saba, ingawa wako shuleni kwa miaka saba. Wanapokwenda sekondari kupitia mitihani magumashi hawawezi kuhimili elimu ya sekondari kwa kuwa msingi wao ni mbovu. Wakifika kidato cha nne ndo darasa zima dv3 wawili na dv4 10 the rest ni zero. Nini kitatokea hapa kama si kuiua jamii hii? Utapata hao marubani, waongoza watalii, manesi watatoka wap?
Jambo baya zaidi ni kuwa watoto wao wanasoma nje na kutuacha sisi maskini katika shule zisizo na walimu.
 
..hicho chakula, mavazi unachodai huwanunulii vinakuja umelala usingizi??kama ni mkulima lazima ununue jembe, mbolea, mbegu hata muda wako nk ili hatimaye upate kipato cha kununulia watoto chakula, mavazi na waende shule, jembe, mbegu, mbolea haviji kama zawadi..lazima ununue! huo ndio msingi wa kuendelea, tusidanganyane hapa..kununua ndege, kujenga SGR, Kujenga mitambo ya umeme ni sawa na mkulima kununua vitendea kazi ili amudu kuhudumia familia yake!! labda kama ni mabishano tu na chuki zinazotokana na sababu zingine hatutaki kufahamu na kukiri ukweli ulivyo.
Wewe ndio umesema nini hapa sasa. Kwenye nadharia za uongozi duniani kuna viongozi wa makundi makuu mawili. La kwanza ni wale ambao mkazo wao mkubwa na kipaumbele ni maendeleo ya vitu kwanza. Kundi la pili ni la viongozi ambao wao kipaumbele na mkazo mkubwa ni maendeleo na ustawi wa watu kwanza. Kwa hiyo sisi tumepata kiongozi wa kundi la kwanza. Ndio basi tena tutafanya nini. Tulikosea 25/10/2015, tuangalie tulipojikwaa na siyo tulipoangukia
 
Back
Top Bottom