kiagata
JF-Expert Member
- Jan 12, 2012
- 206
- 79
katika uzinduzi wa kampeni ya ubunge kwenye jimbo la arumeru mashariki mgombea wa chadema alitoa kauli moja nzinto, aliongea mambo mengi ya msingi alakini funika ni lile la kuhusu wazazi kuchangishwa hela ya madawati kila watoto wanapofaulu kujiunga kwenye shule za sekondari, mzazi mwanae hawezi pokelewa mpaka aje na dawati au atoe hela yenye thamani ya hiyo dawati.
Swali gumu sana kulijibu na rahisi sana kulijibu. Kwa mtazamo wangu labda uwe na roho ngumu kuliko ya paka ndipo utakapo chukua uamuzi wakuipigia kura sisiemu. Hivi hata wewe mzazi umeshawahi kujiuliza swali kama hilo nahatakama ulijiuliza dhahiri hukua na wakukusaidia zaidi ya kulala mika na kuacha mambo yaende.
Toka lini mwanao karudi na dawati aliloenda nalo siku yakwanza shule?inamaana lilichakaa au ilikua vipi mbona hakurudi nalo? Huu wizi na unyanyasaji tuupige vita kwa kuchagua chadema daima tofauti na hilo tutabaki kuumizwa mpaka siku tunaenda kaburini. Tuache ushabiki katika mambo ya msingi kama haya.
katika suala la dawati hapa walimu wanajisahau sana,nadhani hawajui kama tunajua.mimi mwanangu kamaliza shule f iv nilipeleka dawati,sasa amemaliza lakini hawakumpa dawati alilopeleka akiwa f i. Moja kwa moja dawati lile lile kauziwa mwanafunzi/mzazi mwingi kwa bei ya juu zaidi tofauti na nilivyonunua mimi.sasa jiulize hivi dawati lililo nunuliwa na kukaliwa bei inatakiwa ipande au ishuke?.
Watanzania tunaibiwa.hawa hawanatofauti na majambazi ila hawa hawatumii silaha. Ila mwizi ni mwizi tu.