Kauli nzito aliyoitoa Joshua Nassari yawagusa wazazi walala hoi wa tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli nzito aliyoitoa Joshua Nassari yawagusa wazazi walala hoi wa tanzania

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by massai, Mar 10, 2012.

 1. m

  massai JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Katika uzinduzi wa kampeni ya ubunge kwenye jimbo la arumeru mashariki mgombea wa chadema alitoa kauli moja nzinto, aliongea mambo mengi ya msingi alakini funika ni lile la kuhusu wazazi kuchangishwa hela ya madawati kila watoto wanapofaulu kujiunga kwenye shule za sekondari, mzazi mwanae hawezi pokelewa mpaka aje na dawati au atoe hela yenye thamani ya hiyo dawati.

  Swali gumu sana kulijibu na rahisi sana kulijibu. Kwa mtazamo wangu labda uwe na roho ngumu kuliko ya paka ndipo utakapo chukua uamuzi wakuipigia kura sisiemu. Hivi hata wewe mzazi umeshawahi kujiuliza swali kama hilo nahatakama ulijiuliza dhahiri hukua na wakukusaidia zaidi ya kulala mika na kuacha mambo yaende.

  Toka lini mwanao karudi na dawati aliloenda nalo siku yakwanza shule?inamaana lilichakaa au ilikua vipi mbona hakurudi nalo? Huu wizi na unyanyasaji tuupige vita kwa kuchagua chadema daima tofauti na hilo tutabaki kuumizwa mpaka siku tunaenda kaburini. Tuache ushabiki katika mambo ya msingi kama haya.
   
 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Mar 10, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,114
  Trophy Points: 280
  ..kwanza hotuba ya mwenyekiti ilikuwa ndefu kuliko ya mgombea ubunge Joshua Nassari.

  ..pili mgombea alipoteza muda kwa kuzungumzia mambo ya kuoa na kuanza kutoa mifano ya wabunge wa chadema ambao hawajaoa au kuolewa.

  ..tatu, Joshua Nassari akamtambulisha mama yake huku akimsahau baba yake.

  ..baada ya hapo akaanza kutoa orodha ya malalamiko na kero bila kueleza yeye ana program gani ya kutatua malalamiko na kero alizoorodhesha.

  ..I want CDM to win in this contest, but I was not inspired by Nassari's performance today.

  NB:

  ..suala la elimu kwa kweli linanigusa sana.

  ..naamini wananchi wanapaswa kuchangia kwa ajili ya elimu, iwe ktk manunuzi ya vitabu, madawati, kuwamotisha waalimu kufundisha muda wa ziada,etc etc.
   
 3. D

  Dopas JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2012
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Atakuwa alipaniki tu, muhimu ni nia yake njema ya kuwahudumia kiaminifu wana Arumeru. Hotuba nzuri tu bila utendaji si chochote... wala haitawasaidia watz. Tumwombee tu afya njema na safari njema anayoanza leo.
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mkuu vitu alivyoongea Nassari ni kwamba ndio silaha wanazotumia CCM. Kwa mfano wanaambia watu wasimchague huyo Nassari kwa sababu ni mdogo sana hata kuoa hajaoa!

  Kuhusu Baba yake mbona Nassari alimtambulisha?
   
 5. T

  Topical JF-Expert Member

  #5
  Mar 10, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hivi mnafikiri chadema wako serious..

  Wajinga ndio waliwao..
   
 6. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #6
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Siasa tu.
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  Mar 10, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,805
  Likes Received: 5,114
  Trophy Points: 280
  FJM,

  ..hakumtambulisha baba yake kwa uzito uleule aliompa mama yake.

  ..mimi nadhani tatizo lilitokana na mgombea kupewa muda mchache kuongea.

  ..pia tatizo lingine inawezekana Nassari hakuandika hotuba yake na kuifanyia mazoezi kabla ya mkutano wa kampeni.

  ..binafsi naomba tu ajipange vizuri zaidi ili awe more articulate ktk hoja zake.

  ..CDM imeshindwa ktk chaguzi mbili zilizopita, they have to win this one.
   
 8. LOWE89

  LOWE89 Senior Member

  #8
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Nakaribia kutowaelewa nini hakikueleweka. Leo ilikuwa uzinduzi mwenyekiti alikuwa anatoa mstakabali mzima wa uchaguzi na umuhimu wake kitaifa, nataraji Joshua atapata nafasi zaidi kwenye mikutano ya kampeni.
   
 9. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #9
  Mar 10, 2012
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,277
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280


  Nassari atazunguka na ataongea meeeengi tu, leo ilikuwa ufunguzi ndio maana Mwenyekiti kaongea mengi, baada ya hapo Nassari atazungumza mengi tu katika kampeni zake za kila kata
   
 10. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #10
  Mar 10, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  mdogo wangu your mentally unfit.
   
 11. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #11
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  miaka 27 tu, lakini Dogo kaongea nondo za nguvu yaani hata yule Wassira wa Magamba hajawahi tema cheche kama zile...
   
 12. T

  Topical JF-Expert Member

  #12
  Mar 10, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Why? can you prove?

  Chadema hawako serious baba..unawajua yale makanisa ya manabii yanayoibuka kama uyoga..kitabia wanafanana na cdm

  Nilichoka na hotuba ya mwenyekiti (sijui lini amekuwa mlokole)...80% anazungumzia mungu wake wtf..

  Nikwambia mdogo arudi haraka nyumbani maan umekuwa mkutano wa dini na si wa siasa..
   
 13. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #13
  Mar 10, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Hivi kila dawati moja anakalia mwanafunzi mmoja?
   
 14. AcinonyxJubatus

  AcinonyxJubatus Senior Member

  #14
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Acha fitina zako. Watu tulikuwepo na aliwatambulisha wote baba yake na mama yake.
   
 15. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #15
  Mar 10, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  bado uja'prove kwamba your mentally fit, dogo acha kukurupuka.
   
 16. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #16
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,689
  Likes Received: 656
  Trophy Points: 280
  Kuhusu michango ya madawati, hilo ni suala la Local government.
  Je, composition ya local government Meru ikoje?
  Na kuna diwani yeyote kutoka CDM aliyewahi kupinga hilo?
  If not, yeye aliwahi kumshauri diwani yeyote wa CDM apinge suala la madawati?
   
 17. K

  Keil JF-Expert Member

  #17
  Mar 10, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hilo ndio lilikuwa tatizo kubwa zaidi, kwamba alipewa muda kidogo sana na ukishapewa muda kidogo unakuwa unaongea kwa kukimbia na hata kama umeandika speech sina hakika kama unaweza kukumbuka kusoma au kufuata hoja ambazo umeandaa kuzigusia.

  Halafu pia wakati mwingine siasa za Bongo ni ngumu sana, CCM huwa hawa ainishi kero za wananchi na namna ya kuzishughulikia, na matokeo yake huwa wanakimbilia kwenye hoja za ajabu ajabu ambazo hazina mashiko. Kwa kuwa wapiga kura wengi wana matatizo ya uelewa na ufahamu, huwa ni wepesi sana wa kuingizwa mkenge kwa hoja za ajabu ajabu.

  Angalia jinsi kete ya udini ilivyotumika Igunga na walipoona inakosa mashiko, dakika za mwisho kabisa wakaenda na hoja kwamba CHADEMA inawadharau vijana wa Igunga na ndio maana CHADEMA walipeleka vijana wa kusimamia kura kutoka nje ya Igunga.

  Sasa hapo Arumeru tayari walishaanza na kampeni ya kwamba Lema amewatukana wazee "washili" na kwamba wamemtaka asikanyage pindi kampeni zikianza. Mgombea anaweka pingamizi kwa kigezo kwamba Nasari ni mdogo, hapo lazima uweke alama kubwa ya kuuliza. Baadaye utaambiwa huyu hana mke as if kuoa ni kigezo cha kuwa Mbunge.

  Siasa za Bongo kwa kiasi kikubwa sana zinatawaliwa na siasa za maji taka za CCM na mara nyingi zimekuwa zikiwaingiza wapinzani mkengeni bila kujua.

  Wakati mwingine huwa ninachanganyikiwa na kujiuliza, hivi wapiga kura huwa wanapiga kura kwa kufuata mkumbo au kwa kufuata/kuangalia namna ambavyo mgombea anaainisha kero za eneo husika, vipaumbele vyake na namna atakavyoshughulikia hizo kero.
   
 18. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #18
  Mar 10, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  JokaKuu,
  Mkuu mbona unayumba? Post yako ya kwanza umeandika Nasari hakumtambulisha baba yake. Post ya pili umegeuka na kusema alimtambulisha lakini hakumpa uzito kama alivyofanya kwa mama yake.

  Sasa mkuu hapa unajaribu kutaka kutufikishia ujumbe gani? I mean hoja yako ni ipi katika hilo.
   
 19. PISTO LERO

  PISTO LERO JF-Expert Member

  #19
  Mar 10, 2012
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 2,821
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135

  mambo ya makanisa yametoka wapi sasa.jaribu kuficha upumbavu wako itakusaidia sana.kama huwezi ni bora ukawa msomaji tu,
  ama kweli tunasafari ndefu ya kuwakomboa baada ya chama chenu kufa.
   
 20. Manjagata

  Manjagata JF-Expert Member

  #20
  Mar 10, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 4,217
  Likes Received: 1,750
  Trophy Points: 280
  Hii kitu ndo nini jamani? "Your mentally unfit" na "Your mentally fit" au macho yangu?
   
Loading...