RAGNAR LOTH
JF-Expert Member
- Oct 11, 2016
- 698
- 1,589
Katika makeither ushuani na mie
SureKumbe mimi ninawaza tofauti kabisa
-Usikombe mboga - namna ya kumfunza na kumkuza mtoto kuwa mstaarabu na kula kwa staha. Asiwe mlafi.
-Usivae nguo za kanisani - Kumuandaa mtoto /kijana kuwa na chaguzi. Kuelewa ni nyakati gani afanye kipi, avae nini na heshima ya kila sehemu. Akiachwa bila kujitambua yeye, mahali na uhusika hata ukubwani ataenda na sare za kazi (bar, kuchezea mpira, kuogelea nk) na sare za kazi.
-Chukua nyama-ni funzo la adabu na utii. Mtoto ajifunze kula kwa staha na kwa utulivu. Asikimbilie kipande kidogo cha nyama ambacho kinamuhangaisha muda mrefu badala ya kupata mlo mkuu (wali, ugali, ndizi nk) ili kujenga siha. Na hata hivyo familia nyingi za Kiafrika tunaishi kijumuia. Hivyo basi mzazi anapomwambia mtoto chukua nyama ni kwa mapenzi mema tu. Haiwezekani mtoto anaanza kula tu, nyama mkononi anahangaika nayo. Anafunzwa uvumilivu. Zile nyama zipo tu na atapata fungu lake.
Kumbuka :Mimi mzazi, nawalea watoto nilionao kwa misingi ya maadili na haki.