Kauli dhidi ya Malawi: JWTZ wamshushua Lowassa!

sioni ttz kwa mh Lowasa kutoa remark hiyo kwani hata sisi raia wa kawaida tulifurahi kuona jinsi JWTZ walivyoreact na kuonyesha ukomavu na utayari wao kikazi, Mh ametoa tamko hilo kwa mapenzi yake na TZ na hiyo unavyofikiria ww ndivyo hivyo hivyo na itatimia

Hata haueleweki weye!
 
Dira ya mtanzania ni gazeti Lenye Mahaba na sitta na membe hivyo limetumika kumshambulia lowassa tu Adui Yao, Mimi nawajua makamanda wakubwa wote aw jeshi wanampenda lowassa
 
Kubali au kataa. Lowasa ndiyo Raisi wa Tz kwa sasa. Ndiyo maana alitoa kauli ya kuwatisha wa Malawi. Jk kawekwa kama sura tu ya kiti cha uraisi, hawa Jk na El hawakukutana street, wanamakubaliano yao ambayo wengine hatuyajui. Kama huamini jiulize, jeuri, ujasiri na nguvu ya El inatoka wapi kama yeye si raisi aliye nyuma ya pazia? Bomu hili litaripuka kabla ya uchaguzi 2015. Hapo ndipo wa Tz wengi tutaujua ukweli kati ya El na Jk.

Nonsense!
 
Huyo amiri jeshi mkuu wenu alikua Ghana wala hana time na migogoro ya nchi yetu. Hapo ndio mjiulize lowasa angekua rais angeshaongea Rais wetu kimya hata hajasema kitu wakati yule wa malawi tayari kashazungumza ... Sometimes u wonder ka hii nchi ina kiongozi

Wewe hujaongea, mbona wengi tu wanaongea, lkini wako kama wewe, mwenzangu na mie, nani atakusikia?

Kwi kwi kwi teh teh teh!

Kikwete wacha kutolea tamko, kisha kutana na Rais wa Malawi na wakaliongea hilo. Huyo ndio Kikwete, wewe msikie tu. Kwa kazi zake yule humuwezi wala hakuna wa kabla yake aliyemfikia hata robo. Jamaa hakisii yule.
 
Na kwa cheo alichonacho he is obliged to know the withstand of the TPDF over any threat facing the country

Soma na uelewe alichosema Lowasa. Kauli yake ilipaswa au inaweza kutolewa na Wazri wa Ulinzi au Rais tu labda Waziri Mkuu.
Nafasi ya Lowasa kama M/kiti wa Kamati ni ipi katika jambo la Mpaka na vita?
Pia Membe hakupaswa kutoa kauli île kwani kwa nafasi yake kama Waziri wa Mambo ya nje ni Mwanadiplomasia hivyo ilikuwa busara yake kuona mazungumzo kwanza yanafanyika na vitisho kutolewa na "mwingine".
 
Okay. So you mean kwamba Jakaya kaliinstruct Jeshi lim-burst lowasa? kama ni kweli safi sana na ninawithdrawal kauli yangu ya udhaifu, lakini kwanini asifanye hivyo mwenyewe? ataendelea kujificha nyuma ya wasaidizi wake mpaka lini?

Kwani walikutana barabarani wale? hujui maana ya good cop, bad cop? Kama huijui, isome.
 
... "Jeshi letu linaendeshwa kiprofessional". Hii ni kweli, isipokuwa wakati wa uchaguzi mkuu!

Kulikuwa na outlier moja ambayo ilikuwa inawaza kulinda ufisadi wake. Bado ninaamini kabisa kuwa Jeshi la Tanzania lina watu makini sana zaidi ya Shimbo, kwani ukiisha liendesha jeshi kisiasa maanaake unaitakia nchi civil war kwani jeshini wapo wanaoamini itikadi tofauti. Na hili CCM wanatakiwa walijue na walitambue kuwa wawatumie vimemo kina Mwema et al. kusumbua upinzani, lakini JWTZ waliache wasilicontaminent na siasa.

Kauli ya Lowassa ni kauli mbaya sana kuwahi kutolewa na mwanasiasa asiyekuwa amiri jeshi mkuu. Kauli kama ya Lowassa ni ya kuididimiza nchi, utafukuza uwekezaji, utafanya investors kufikiria upya kwenye miradi walioiamulia ndani ya Tanzania. Inaongeza wasiwasi miongoni mwa wananchi. Ni nani asiyekumbuka hali ya uchumi ilivyokuwa baada ya vita ya Uganda 1978?, kwa waliokuwepo wanakumbuka watu walikula unga yanga na kuvaa magunia.

Kauli ya kupinga vita ilitakiwa kutolewa na JK mwenyewe si kuwaachia JWTZ, JK anatakiwa kuwa kiongozi sasa, asimame mbele aseme kuwa hana nia ya kuingia vitani, LEADING FROM BEHIND strategy needs to stop.
 
Wewe hujaongea, mbona wengi tu wanaongea, lkini wako kama wewe, mwenzangu na mie, nani atakusikia?

Kwi kwi kwi teh teh teh!

Kikwete wacha kutolea tamko, kisha kutana na Rais wa Malawi na wakaliongea hilo. Huyo ndio Kikwete, wewe msikie tu. Kwa kazi zake yule humuwezi wala hakuna wa kabla yake aliyemfikia hata robo. Jamaa hakisii yule.

Mahaba hayo.
 
Soma na uelewe alichosema Lowasa. Kauli yake ilipaswa au inaweza kutolewa na Wazri wa Ulinzi au Rais tu labda Waziri Mkuu.
Nafasi ya Lowasa kama M/kiti wa Kamati ni ipi katika jambo la Mpaka na vita?
Pia Membe hakupaswa kutoa kauli île kwani kwa nafasi yake kama Waziri wa Mambo ya nje ni Mwanadiplomasia hivyo ilikuwa busara yake kuona mazungumzo kwanza yanafanyika na vitisho kutolewa na "mwingine".

Nimekupata but nilipoegemea mimi sio kauli yake bali mamlaka ya uwenyekiti alionao juu ya kamati nyeti kama hiyo ndani ya bunge anapaswa kujua yanayoendelea juu ya hii dispute. Kuhusu kauli aliyoitoa, ni utashi wake mwenyewe uliomtuma na hapo sipo nilipoegemea. Nadhani nimeeleweka.
 
Sasa hapo Lowasa ana kosa gani wakati utayari wao wenye JWTZ Waliuonesha hadharani wakati wa sherehe za miaka 50 ya uhuru.

uwezo gani walionesha kipindi cha sherehe ya miaka 50..?! ule wa kupasia matofali kwa vichwa ..?
 
Dira ya mtanzania ni gazeti Lenye Mahaba na sitta na membe hivyo limetumika kumshambulia lowassa tu Adui Yao, Mimi nawajua makamanda wakubwa wote aw jeshi wanampenda lowassa
Nikweli gazeti la DIRA lina mahaba na Sitta na Membe mahaba si kitu lkn wazidisha nyeupe wanatuaminisha ni nyeusi! kwa gazeti hilo Lowasa hamna alichofanya,hafadhali hata gazeti la cdm tanzania daima mahaba wanapunguza kidoga,sasahili la TSJ to much,musiwasingizie JWTZ wapo pamoja na mwenyekiti wa bunge.
 
Nilihoji siku moja hapa JF, kwamba Lowasa ni nani mpaka atoe kauli kuwa Jeshi letu lipo tayari kwa vita?
 
Nilihoji siku moja hapa JF, kwamba Lowasa ni nani mpaka atoe kauli kuwa Jeshi letu lipo tayari kwa vita?
Jeshi lolote duniani kama ni la Nchi lipo tayari kwa vita,kujua hili halihitaji kufika darasa la saba,ila kuanzisha vita ni kazi ya amirijeshi mkuu,yeye ni boss wa maswala ya ulinzi na usalama bumgeni.
 
Nikiwa naelekea ofisini asubuhi hii Radio Clouds wakiwa wanapitia habari za kwenye magazeti ya leo wamesoma gazeti moja likisema JWTZ limemkanya Edward Lowassa kwa kauli yake aliyotoa hivi karibuni kwamba amethibitishiwa kwamba Jeshi letu liko imara na Tayari kwa vita.

JWTZ wanadai kauli ya namna hiyo ilipaswa kutolewa na Amiri Jeshi Mkuu peke yake.

SOMO LA LEO
1. Lowassa bado anamahaba na Urais,
2. Jeshi linatumika kumpunguza speed ya uroho wake wa madaraka
3. Kikwete ni dhaifu kweli kwa kushindwa kuzuia watu kuingilia madaraka yake
4. Jeshi letu linaendeshwa kiprofessional
5. Jeshi letu linaelewa madhara ya vita, na lisingependelea kulazimishwa kuingia vitani bila sababu za msingi kama kwenye ka issue ka ziwa nyasa.
6. Intelligencia za Jeshi letu hazijaona likelyhood ya vita dhidi ya Malawi so far. NO POINT FOR WAR.
7. Ujumbe huu uwafikia SITTA NA MEMBE AS WELL.
8. Ni fundisho kwa wanasiasa wote wa CCM wanaoropoka bila kufikiria na kuthibitisha uwezo mdogo sana wa uongozi, na kwamba wananchi tuendelee kusimamia imani yetu kwamba CHAMA hiki hakifai, sababu baada ya kutusukumiza kwenye umasikini wa kututosha sasa ni wazi wako tayari kumwaga na damu zetu.

Asante JWTZ kwa kuweka mambo sawa.

Chad ema Kama ilivyo unapomaliza sala unasema Amina wao Amina Yao Ni CCM. Wataeleza Jambo wakifika mwisho wansema CCM.
 
Back
Top Bottom