Kauli dhidi ya Malawi: JWTZ wamshushua Lowassa!

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,649
Nikiwa naelekea ofisini asubuhi hii Radio Clouds wakiwa wanapitia habari za kwenye magazeti ya leo wamesoma gazeti moja likisema JWTZ limemkanya Edward Lowassa kwa kauli yake aliyotoa hivi karibuni kwamba amethibitishiwa kwamba Jeshi letu liko imara na Tayari kwa vita.

JWTZ wanadai kauli ya namna hiyo ilipaswa kutolewa na Amiri Jeshi Mkuu peke yake.

SOMO LA LEO
1. Lowassa bado anamahaba na Urais,
2. Jeshi linatumika kumpunguza speed ya uroho wake wa madaraka
3. Kikwete ni dhaifu kweli kwa kushindwa kuzuia watu kuingilia madaraka yake
4. Jeshi letu linaendeshwa kiprofessional
5. Jeshi letu linaelewa madhara ya vita, na lisingependelea kulazimishwa kuingia vitani bila sababu za msingi kama kwenye ka issue ka ziwa nyasa.
6. Intelligencia za Jeshi letu hazijaona likelyhood ya vita dhidi ya Malawi so far. NO POINT FOR WAR.
7. Ujumbe huu uwafikia SITTA NA MEMBE AS WELL.
8. Ni fundisho kwa wanasiasa wote wa CCM wanaoropoka bila kufikiria na kuthibitisha uwezo mdogo sana wa uongozi, na kwamba wananchi tuendelee kusimamia imani yetu kwamba CHAMA hiki hakifai, sababu baada ya kutusukumiza kwenye umasikini wa kututosha sasa ni wazi wako tayari kumwaga na damu zetu.

Asante JWTZ kwa kuweka mambo sawa.
 
Nahisi kama hapa Lowassa kapigwa ngumi ya mbavu, haamki tena huyu fisadi.
 
No comment, despite several attempts of re-reading your contents. I understand your intents tho.
 
sioni ttz kwa mh Lowasa kutoa remark hiyo kwani hata sisi raia wa kawaida tulifurahi kuona jinsi JWTZ walivyoreact na kuonyesha ukomavu na utayari wao kikazi, Mh ametoa tamko hilo kwa mapenzi yake na TZ na hiyo unavyofikiria ww ndivyo hivyo hivyo na itatimia
 
Hivi hamjui Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Tanzania ni nani?

Hakuna Mwanajeshi wa chini yake anaeweza kuliongelea taifa kisiasa bila amri na au idhini yake.
 
Hivi hamjui Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Tanzania ni nani?

Hakuna Mwanajeshi wa chini yake anaeweza kuliongelea taifa kisiasa bila amri na au idhini yake.

Okay. So you mean kwamba Jakaya kaliinstruct Jeshi lim-burst lowasa? kama ni kweli safi sana na ninawithdrawal kauli yangu ya udhaifu, lakini kwanini asifanye hivyo mwenyewe? ataendelea kujificha nyuma ya wasaidizi wake mpaka lini?
 
Ambaye ana authority ipi over JWTZ?
kusema jeshi lipo fit kwa kupigana, wanakanusha nini kwani hawako fit? JK anawaza safari, bora EL amedhubutu hata kuwatishia no matter tuna nguvu ana la!

Amiri Jeshi mkuu hatakiwi kusema tupo tayari ni kusema vijana kazi ianze!
 
... "Jeshi letu linaendeshwa kiprofessional". Hii ni kweli, isipokuwa wakati wa uchaguzi mkuu!
 
Lowasa alisema kama mwenyekiti wa kamati ya bunge ya ulinzi na usalama
KATIBA ya JMT haimtambui mtu huyu. Niliyasema haya kwenye ile thread ya Mwanakijiji aliokuwa akidadisi uwezo na utayari wetu kwa vita. Lowasa ameishi serikalini kwa muda mrefu. Alipaswa kulifahamu hili. Sio kukurupuka kutamka yale maneno eti kwa kuwa mahasimu wake akina Membe na Sitta wametangulia kuyasema!
 
Back
Top Bottom