KATIBA ya JMT haimtambui mtu huyu. Niliyasema haya kwenye ile thread ya Mwanakijiji aliokuwa akidadisi uwezo na utayari wetu kwa vita. Lowasa ameishi serikalini kwa muda mrefu. Alipaswa kulifahamu hili. Sio kukurupuka kutamka yale maneno eti kwa kuwa mahasimu wake akina Membe na Sitta wametangulia kuyasema!
Hali hii ni inaendelea kuonyesha udhaifu wa JK. Ni kweli yawezekana kauli ya EL ilitolewa na mtu asiyestahili, lakini ilitolewa muda muafaka. Ni wazi kuwa imesaidia sana kuleta joto kali Malawi na kuwafanya warudi nyuma!
Hata vyomba vya habari vya Malawi na wananchi wake walipaniki na kufikia kuwaita Watanzania wapenda vita!
Maswali ya kujiuliza, aliyetakiwa kutoa kauli hiyo katika muda muafaka alikuwa wapi? Je, alitoa kauli yoyote?
Kwa nini hakutoa wakati ilikuwa ni muhimu sana kipindi kile? Napata tabu kuelewa kama ipo siku ataelewa kuwa uongozi ni pamoja na kuchukua hatua sahihi katika muda muafaka.
Vyombo vya habari, mna rekodi kubwa ya matukio mbalimbali ambayo Mkulu alilala tu, hatoi kauli mpaka mambo yameharibika. Mfano, Wabunge kujiongezea posho kinyemela! Alikaa kimya mpaka hali ilipokuwa mbaya , akawaruka. Huu si uongozi. Wananchi wanapaswa kukumbushwa matukio haya.Baba hutoka chumbani watoto wanapogombana sebuleni!
El, pamoja na ufisadi umejitahidi kwa hili.
JWTZ, kauli imetulia. Tumewaelewa, ni lugha ya kitu uzima, ya kusema aliyetakiwa kutoa kauli alikuwa kimya as if hajui kinachoendelea!Itamuuma sana hii kulika EL.