Kauli 8 ambazo mwanamke akizitoa jihadhari sana

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,093
Reaction score
34,909
81a8b1883d75ed42727c13b638ff25b6944a90889d7ccfe59762998c592bdfbcef5bf694437eab3b3fc1734368739bf2354f8df42f9c504769a2ae90d2c20c6e95e578bca21ed4250cb14c944fa37e7aac10cc35ac20472
​

1. Mwanamke anaposema, 'sasa hivi' au 'dakika moja tu,' maana yake ni kwamba, ni nusu saa ijayo. kwa mwanamke sasa hivi ya kujiandaa ina maana sasa hivi ya muda mrefu mara sita zaidi kuliko ule anaoutaja. kama akisema , 'nusu saa tu, naja,' unapaswa kwenda kufanya shughuli nyingine kwanza, kwa sababu huenda ukiamua kuamini kwamba ni nusu saa kweli, utasimama au kukaa mahali kumsubiri hadi miguu iingie tumboni au makalio yaote ganzi.
​
2. Mwanamke anaposema, 'utajua mwenyewe,' ana maana kwamba amekasirishwa na kukatishwa tamaa na tabia yako na sasa hajali tena. maana yake ni kwamba kwa upande wake haoni sababu ya kujiumiza bure na huenda atachukua uamuzi ambao nawe pia hautaufurahia. Je, anaweza kuanza kutoka nje baada ya hapo? inawezekana ingawa siyo lazima.​

3. Mwanamke anapopumua kwa nguvu, yaani kushusha pumzi kwa kishindo, hiyo pia ni kauli kwa upande wake. kama anashusha pumzi kwa nguvu wakati mkijadili au kuongea jambo, ni taarifa kwamba amekudharau. yaani amekuona mjinga nambari moja. ni kauli kwamba, haoni sababu ya kuendelea kuwepo hapo kubishana nawe, kwani huna jambo la maana unalomweleza.

4. Mwanamke anaposhusha pumzi polepole, ina maana kwamba, amekubaliana na wewe. Sasa hapo usifanye kosa kwani, ukibadilika kidogo au kuleta mambo mengine kinyume na na hayo yaliyomridhisha, ndipo hapo atashusha pumzi kwa nguvu , yaani kuanza kukuona huna maana kwa wakati huo. Kumbuka kwamba, mwanamke akishusha pumzi kwa nguvu kwa maana ya kukuona huna lolote, hukuona hivyo kwa wakati ule tu au kwa hilo jambo linalohusika tu, siyo kwamba, hukuona hivyo siku au muda wote. vivyo hivyo kwenye kushusha pumzi pole pole, hukuona 'babu kubwa' kuhusiana na na jambo mnalojadili kwa wakati huo tu.

5. Mwanamke anapotumia neno, 'sawasawa,' kwa kawaida kama kuna jambo umemfanyia, ina maana kwamba, 'ninachukua muda kutafakari, halafu utaona nitakachokulipa baadaye.' Kauli hii siyo nzuri na mara nyingi ni ya hatari. Wanaume ambao wamewahi kulipiziwa visasi kwa njia mbaya na ya hatari na wapenzi wao wamekiri kuambiwa,'sawasawa,' au 'sawa bwana,' kabla ya visasi hivyo.

6. Mwanamke anapotamka neno, 'we endelea tu,' anakuwa na maana ya kwamba, siku si nyingi zijazo, atafanya jambo ambalo hutalifurahia, kama hutaacha kufanya kitu au jambo lenye kumuudhi. hiyo ni kauli ya kukutahadharisha kwamba, usije ukashangaa pale ambapo utaona amefanya kitendo cha hatari dhidi yako kutokana na tabia yako au matendo yako mabaya dhidi yake.

7. Kuna wakati mwanamke anaweza kusema, 'sawa bwana fanya,' kama kuna jambo ambalo hamjafikia muafaka au amebaini umekuwa ukifanya jambo fulani baya au lenye kumkera. Hapa hana maana kwamba, amekuruhusu kwa moyo mmoja, hapana. Hapa anataka ubaini kwamba, hajakubaliana nawe, anakupa muda wa kujaribu kutafakari tena.

8. Je kama mmeshindana katika jambo au umemkera katika jambo au mambo fulani, kutokana na tabia au mwenendo fulani, halafu akakumabia, 'asante sana,' itakuwa na maana gani? Hii ina maana umemkera kupita kiasi na bado wala hajajua akufanye nini. Hii ni toafauti na 'asante' ya kawaida. Mwanamke anapoongeza neno 'sana,'ujue umemkera hasa, kuliko unavyoweza kufikiri. Halafu kama baada ya kusema, 'asante sana,' anashusha pumzi kwa nguvu, ujue hali ni mbaya zaidi, bora unyamaze kwanza, hata radhi usiombe kwa muda huo, subiri apoe kwanza​
 
Sina uhakika kama wote Humaanisha hivi yalivyotafsiriwa haya maneni,
MziziMkavu, Tuletee na maneno ya wanaume basi
 
Last edited by a moderator:
Izo hisia ni kwa wote mkuu fanya utafiti na wanaume wapo hivyo.
Kwa kuongeza tu hizo kauli hazitoki kwa kila mwanamke ama kwa kila mwanaumume ila ni kwa wale ambao wana true loce with high committement taking his/her love a meaning person and the only person to trust and share things
 
81a8b1883d75ed42727c13b638ff25b6944a90889d7ccfe59762998c592bdfbcef5bf694437eab3b3fc1734368739bf2354f8df42f9c504769a2ae90d2c20c6e95e578bca21ed4250cb14c944fa37e7aac10cc35ac20472
​

1. Mwanamke anaposema, 'sasa hivi' au 'dakika moja tu,' maana yake ni kwamba, ni nusu saa ijayo. kwa mwanamke sasa hivi ya kujiandaa ina maana sasa hivi ya muda mrefu mara sita zaidi kuliko ule anaoutaja. kama akisema , 'nusu saa tu, naja,' unapaswa kwenda kufanya shughuli nyingine kwanza, kwa sababu huenda ukiamua kuamini kwamba ni nusu saa kweli, utasimama au kukaa mahali kumsubiri hadi miguu iingie tumboni au makalio yaote ganzi.
​
2. Mwanamke anaposema, 'utajua mwenyewe,' ana maana kwamba amekasirishwa na kukatishwa tamaa na tabia yako na sasa hajali tena. maana yake ni kwamba kwa upande wake haoni sababu ya kujiumiza bure na huenda atachukua uamuzi ambao nawe pia hautaufurahia. Je, anaweza kuanza kutoka nje baada ya hapo? inawezekana ingawa siyo lazima.​

3. Mwanamke anapopumua kwa nguvu, yaani kushusha pumzi kwa kishindo, hiyo pia ni kauli kwa upande wake. kama anashusha pumzi kwa nguvu wakati mkijadili au kuongea jambo, ni taarifa kwamba amekudharau. yaani amekuona mjinga nambari moja. ni kauli kwamba, haoni sababu ya kuendelea kuwepo hapo kubishana nawe, kwani huna jambo la maana unalomweleza.

4. Mwanamke anaposhusha pumzi polepole, ina maana kwamba, amekubaliana na wewe. Sasa hapo usifanye kosa kwani, ukibadilika kidogo au kuleta mambo mengine kinyume na na hayo yaliyomridhisha, ndipo hapo atashusha pumzi kwa nguvu , yaani kuanza kukuona huna maana kwa wakati huo. Kumbuka kwamba, mwanamke akishusha pumzi kwa nguvu kwa maana ya kukuona huna lolote, hukuona hivyo kwa wakati ule tu au kwa hilo jambo linalohusika tu, siyo kwamba, hukuona hivyo siku au muda wote. vivyo hivyo kwenye kushusha pumzi pole pole, hukuona 'babu kubwa' kuhusiana na na jambo mnalojadili kwa wakati huo tu.

5. Mwanamke anapotumia neno, 'sawasawa,' kwa kawaida kama kuna jambo umemfanyia, ina maana kwamba, 'ninachukua muda kutafakari, halafu utaona nitakachokulipa baadaye.' Kauli hii siyo nzuri na mara nyingi ni ya hatari. Wanaume ambao wamewahi kulipiziwa visasi kwa njia mbaya na ya hatari na wapenzi wao wamekiri kuambiwa,'sawasawa,' au 'sawa bwana,' kabla ya visasi hivyo.

6. Mwanamke anapotamka neno, 'we endelea tu,' anakuwa na maana ya kwamba, siku si nyingi zijazo, atafanya jambo ambalo hutalifurahia, kama hutaacha kufanya kitu au jambo lenye kumuudhi. hiyo ni kauli ya kukutahadharisha kwamba, usije ukashangaa pale ambapo utaona amefanya kitendo cha hatari dhidi yako kutokana na tabia yako au matendo yako mabaya dhidi yake.

7. Kuna wakati mwanamke anaweza kusema, 'sawa bwana fanya,' kama kuna jambo ambalo hamjafikia muafaka au amebaini umekuwa ukifanya jambo fulani baya au lenye kumkera. Hapa hana maana kwamba, amekuruhusu kwa moyo mmoja, hapana. Hapa anataka ubaini kwamba, hajakubaliana nawe, anakupa muda wa kujaribu kutafakari tena.

8. Je kama mmeshindana katika jambo au umemkera katika jambo au mambo fulani, kutokana na tabia au mwenendo fulani, halafu akakumabia, 'asante sana,' itakuwa na maana gani? Hii ina maana umemkera kupita kiasi na bado wala hajajua akufanye nini. Hii ni toafauti na 'asante' ya kawaida. Mwanamke anapoongeza neno 'sana,'ujue umemkera hasa, kuliko unavyoweza kufikiri. Halafu kama baada ya kusema, 'asante sana,' anashusha pumzi kwa nguvu, ujue hali ni mbaya zaidi, bora unyamaze kwanza, hata radhi usiombe kwa muda huo, subiri apoe kwanza​

Mi naona wanawake kama wangebadilisha hii hali na kuyaongea yanayowasibu ili kupata suluhisho mahusiano yangedumu! Siyo kila mwanaume atajua majibu yao mbadala na sidhani kama kila jambo lingepingwa hata baada ya mazungumzo.
 
Madame B hii inaashiria nyie ni wa muhimu sana kwetu, hivyo hatuna budi kuwafahamu kwa mapana, marefu na utuo ili kuwakwaza iwe aghalabu. Hili nalo ni baya?

Ahsante sana kwa compliment hii kwa niaba ya wanawake wote!!! Napenda kusikia wanaume wakitutambua sisi ni wa MUHIMU sana katika maisha yao kama ambavyo na ninyi(WANAUME) mlivyo wa MUHIMU kwetu! Kaka una malezi na hata aliye nawe amepata mwenza!
 
Back
Top Bottom