Kauli 8 ambazo mwanamke akizitoa jihadhari sana

Kauli 8 ambazo mwanamke akizitoa jihadhari sana

Dah umenigusa hapo namba 8,jana nimekasirishwa ile mbaya,nlikua cjui namfanyaje da boy,nkaishia kumwambia asante sana umenitreat so nicely,dah i don't what to think more about what happened yesterday,but i was real boring day!
 
81a8b1883d75ed42727c13b638ff25b6944a90889d7ccfe59762998c592bdfbcef5bf694437eab3b3fc1734368739bf2354f8df42f9c504769a2ae90d2c20c6e95e578bca21ed4250cb14c944fa37e7aac10cc35ac20472
​

1. Mwanamke anaposema, 'sasa hivi' au 'dakika moja tu,' maana yake ni kwamba, ni nusu saa ijayo. kwa mwanamke sasa hivi ya kujiandaa ina maana sasa hivi ya muda mrefu mara sita zaidi kuliko ule anaoutaja. kama akisema , 'nusu saa tu, naja,' unapaswa kwenda kufanya shughuli nyingine kwanza, kwa sababu huenda ukiamua kuamini kwamba ni nusu saa kweli, utasimama au kukaa mahali kumsubiri hadi miguu iingie tumboni au makalio yaote ganzi.
​
2. Mwanamke anaposema, 'utajua mwenyewe,' ana maana kwamba amekasirishwa na kukatishwa tamaa na tabia yako na sasa hajali tena. maana yake ni kwamba kwa upande wake haoni sababu ya kujiumiza bure na huenda atachukua uamuzi ambao nawe pia hautaufurahia. Je, anaweza kuanza kutoka nje baada ya hapo? inawezekana ingawa siyo lazima.​




3. Mwanamke anapopumua kwa nguvu, yaani kushusha pumzi kwa kishindo, hiyo pia ni kauli kwa upande wake. kama anashusha pumzi kwa nguvu wakati mkijadili au kuongea jambo, ni taarifa kwamba amekudharau. yaani amekuona mjinga nambari moja. ni kauli kwamba, haoni sababu ya kuendelea kuwepo hapo kubishana nawe, kwani huna jambo la maana unalomweleza.


4. Mwanamke anaposhusha pumzi polepole, ina maana kwamba, amekubaliana na wewe. Sasa hapo usifanye kosa kwani, ukibadilika kidogo au kuleta mambo mengine kinyume na na hayo yaliyomridhisha, ndipo hapo atashusha pumzi kwa nguvu , yaani kuanza kukuona huna maana kwa wakati huo. Kumbuka kwamba, mwanamke akishusha pumzi kwa nguvu kwa maana ya kukuona huna lolote, hukuona hivyo kwa wakati ule tu au kwa hilo jambo linalohusika tu, siyo kwamba, hukuona hivyo siku au muda wote. vivyo hivyo kwenye kushusha pumzi pole pole, hukuona 'babu kubwa' kuhusiana na na jambo mnalojadili kwa wakati huo tu.


5. Mwanamke anapotumia neno, 'sawasawa,' kwa kawaida kama kuna jambo umemfanyia, ina maana kwamba, 'ninachukua muda kutafakari, halafu utaona nitakachokulipa baadaye.' Kauli hii siyo nzuri na mara nyingi ni ya hatari. Wanaume ambao wamewahi kulipiziwa visasi kwa njia mbaya na ya hatari na wapenzi wao wamekiri kuambiwa,'sawasawa,' au 'sawa bwana,' kabla ya visasi hivyo.


6. Mwanamke anapotamka neno, 'we endelea tu,' anakuwa na maana ya kwamba, siku si nyingi zijazo, atafanya jambo ambalo hutalifurahia, kama hutaacha kufanya kitu au jambo lenye kumuudhi. hiyo ni kauli ya kukutahadharisha kwamba, usije ukashangaa pale ambapo utaona amefanya kitendo cha hatari dhidi yako kutokana na tabia yako au matendo yako mabaya dhidi yake.


7. Kuna wakati mwanamke anaweza kusema, 'sawa bwana fanya,' kama kuna jambo ambalo hamjafikia muafaka au amebaini umekuwa ukifanya jambo fulani baya au lenye kumkera. Hapa hana maana kwamba, amekuruhusu kwa moyo mmoja, hapana. Hapa anataka ubaini kwamba, hajakubaliana nawe, anakupa muda wa kujaribu kutafakari tena.


8. Je kama mmeshindana katika jambo au umemkera katika jambo au mambo fulani, kutokana na tabia au mwenendo fulani, halafu akakumabia, 'asante sana,' itakuwa na maana gani? Hii ina maana umemkera kupita kiasi na bado wala hajajua akufanye nini. Hii ni toafauti na 'asante' ya kawaida. Mwanamke anapoongeza neno 'sana,'ujue umemkera hasa, kuliko unavyoweza kufikiri. Halafu kama baada ya kusema, 'asante sana,' anashusha pumzi kwa nguvu, ujue hali ni mbaya zaidi, bora unyamaze kwanza, hata radhi usiombe kwa muda huo, subiri apoe kwanza​

mkuu ukitandikwa sonyo je!?
 
Ukisikia mwanamke anakwambia nikwambie kitu....kifuatacho mzinga.

hahaha! Hiyo mara nyingi inatokea kwenye calls au sms!

ni vipi ukiwa nae faragha unaongea nae issue sensitive yeye anakuwa busy tu kukuna kuna kichwa na kurekebisha nywele zake ina ashiria nin?
 
Siku moja, nilipatwa kuambiwa "Asante sana" nikajibu "Asante ya kushukuru" kilichojiri hasikuambie mtu, lilitimka vumbi, mpaka magari yakapitiliza vituo.
 
Ukiona weekend upo nyumban na mwenza wako anakujua mtu wa totozi.. na msg like Leo hautoki?,Nyumban upo had saa ngap,Usitoke pumzika tu nyumban..Hapo kaa ukijua anataka kukupiga suprise aje kimya kimya.Chakufanya kaa mbal na watoto na pamba hata picha zake kama unazo.,akija akakuta hivyo basi tena ushammaliza

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Sina uhakika kama wote Humaanisha hivi yalivyotafsiriwa haya maneni,
MziziMkavu, Tuletee na maneno ya wanaume basi

Wanaume hawanaga kasumba ya kuongea sana. Mwanamke ana udhaifu wake na kuongea kwao ni kama kuexpress their emotions. Men never use words to express emotions the way women do. A stressed woman will always do something to show her stresses but a stressed man will be as quiet as possible. Know the difference. In case you want to know more about this nitafute. Tehe tehe tehe tehe tehe
 
huyu wangu ana mtindo wa hiyo namba tatu,nakushukuru kwa kunifumbua macho sasa hivi akifanya hivyo tu namkata makofi.
Nalog off
 
huyu wangu ana mtindo wa hiyo namba tatu,nakushukuru kwa kunifumbua macho sasa hivi akifanya hivyo tu namkata makofi.
Nalog off
Usimpige Mwanamke mwanamke huwa hapigwi hata kidogo unamwambia tu atakusikiliza . Mwanamke ni kama uwa na ni pambo la mwanamme kwanini umpige kipenzi chako? Mkuu TUKUTUKU acha tabia mbovu ya kupiga wanawake.
 
Last edited by a moderator:
Hiyo no 6 nimemwambia leo kinachofuata shahidi yake atakua shetani.
 
Back
Top Bottom