Katuni: Bunge letu na dhihaka toka Kenya

Katuni: Bunge letu na dhihaka toka Kenya

Hawajakosea sema wamesahau kuweka sehemu wanadooo! maana wakiwa dodoma machango wote wanahamia huko!
 
we acha uongo utukufu na matusi wapi na wapi au unadhani wote hamnazo
 
attachment.php
Shame Kiti cha Spika... Watanzania wote tunabeba aibu hii kwa wapumbavu wachache kama akina Ndugai et al...Bila ya kuweka mambo ya vyama mbele...Wabunge wa CCM wanaongoza kwa Ulevi, Kulala, Umalaya, Kupitisha sheria zenye kuitafuna nchi... Wabunge wa CCM wanaongoza kwa kushabikia mambo ya kijinga Bungeni badala ya kuiadabisha Serikali... I think Wakenya wako sahihi sana kwa hili...
 
wadau heb angalia jinsi wakenya wanavyodhihaki bunge letu tukufu,
View attachment 92823
Samahani mkuu. Kwa kuweka kumbukumbu, Mchora katuni hii (GADO) ni MTANZANIA.
Miaka michache nyuma alichora katuni yenye taswira ya waandishi wa habari watz wakila miguuni mwa wanasiasa. Waandishi walimwandama kwa makala kwenye magazeti. Lakini ni kweli kuwa wanahabari wetu wamewekwa mifukoni na matajiri na wanasiasa
 
attachment.php


i have liked this..is this GADO?

tasfiri yake ni kuwa limekuwa genge ambalo kila mtu ana interest yake...

aliyekaa chini na sigara namfananisha na kibajaji... yaani teja wa upande ule..

waziri akliyepanik na kumropokea mwenzie aliyekaa kiti ya nyuma
anawakilisha mtazamo wa serekali ya ccm kwa wabunge wao wanaoihoji.............

kulala lala kwenye upande huo wa watawala kuna ishara ya u laize affair wa wabunge na serekali ya ccm....lugha ishara kuwa hoja zinapita na wao kuziunga mkono bila kupembua madhara yao kwao na kwa waliowatuma....

mkojo wa serukamba kwa kiti cha spika ni ujumbe kuwa tusi lile limedharaulisha kiti cha spika ambaye hata habari hana.........

kati kati kuna kijiwe (kaka na dada) kinachoonyesha kuwa kuna watu wako pale hawajui ni kitu gani kimewaingiza mjengoni kwao ni kula bata kwa kwenda mbele....

makatibu wa bunge..wao ni watumishi tu hawajalala..kwa mbaali mmoja anajribu kupunguza spidi ya upande wa pili

MASHATI YA KIJANI niishara ya chama kinachohisi kina kopiraiti ya kutawala.....kilichoshindwa kutafautisha utawala na uongozi

UPANDE wa pili - KWA WAPINZANI

kuna mikono miwili...mmoja unanyoosha kidole .... yaani unalaumu

KUNA MKONO mwingine.... unakaataa na kusema hapana......

kwa ujumla hii ndio hali halisi ya bunge letu..hongera mchoraji.....

Analysis nzuri. Umesahau moja kuwa hawa jamaa wametupa makabrasha yao chini hakuna mwenye muda wa kuyasoma.
 
Bunge gani unaliita tukufu, hili la mama Makinda? Mkiambiwa ukweli mnasema mnadharauliwa. Bunge gani hili, upuuzi mtupu!
A man boasts his P... though small. Tuwe wazalendo tusikubali kutukanwa na media nje halafu tukashahabikia. Ninaomba wataalamu wa sheria washauri chakufanya.
 
attachment.php

Mwangalie Serukamba hiyo ndiyo maana na neno lake Bungeni

Hii funga kazi. Huyu bwana Mdogo (sijui Gado huyu)hana Mchezo! Kuna mzee kavaa nguo ya maua maua anammezea mate mama mmoja anayepata hapo ka mvinyo; sijui ni nani huyu. Madame Speaker anauchapa mchana kweupe! Mkuu Serukamba yeye katoa mkuki anajisaidia Bungeni na nguo za ndani zimeanikwa bungeni halafu wenyewe wakiinuka wanasema BUNGE LAKO TUKUFU. Kwa hii ya katuni sioni utukufu hapa.

Ile Kamati ya Bunge ya Haki na Mamlaka ya Bunge ambayo iliwahi kuwahoji akina mama Terry imeenda wapi? Ingemuita Gado na kumhoji!!
 
A man boasts his P... though small. Tuwe wazalendo tusikubali kutukanwa na media nje halafu tukashahabikia. Ninaomba wataalamu wa sheria washauri chakufanya.
Siendi kwa emotions mkuu, siwezi kusifia upup.u eti kwa vile ni "changu". Kuna nini katika hili bunge zaidi ya mipasho ya kijiweni? Tunaambiwa bunge ni kwa ajili ya kuisimamia serikali. Angalia hivi sasa kama kweli wanaisimamia serikali zaidi ya kuitetea. Eti niwe mzalendo, uzalendo au uzandiki? Natumia kichwa kutunza ubongo na akili wala situmii kichwa kubeba masikio na kufuga nywele mkuu!!!!
 
Naona wasira amedondoka chini kama chungwa na kuanza kuuchapa usingizi huku lukuvi akinywa kikombe cha babu kwa mbwembwe
 
Ndiooooooooooooooooooooooooooooooooooooo!!!!! Naunga mkono hii katuni Asilimia 100 kwa 100!
 
Hivi waheshimiwa wetu wa mjengoni wanapoona kitu kama hiki wanajisikiaje? Au wao wanapotezea tu? Kwa kweli inatia aibu sana kwa mambo ambayo wamekuwa wanayafanya pale mjengoni na hawana budi kubadilika.
 
Back
Top Bottom