Katu usimkekete binti yako...

Kama.huu utamaduni was ukeketaji...uanafaida kwa Jamii Husika...wafanye TU...SASA SISI TUTAWAZUIA NINI Kama wao wanaona Ni Heshima na ni hadhi kwa mwanamke..

Zabron Hamis Msiache kukeketa hao watu wenu... IWE YA KIZAMANI AU.YA KISASA.
 
Ukeketaji
 

MNHHHH sio lazima kutembelea huko,hakuna lililojificha kuhusu FGM,kiasi kwamba mtu afunge safari ya kwenda for fact finding mission, wastage of time. HAKUNA jipya atalokutana nalo huko ambalo halijaongelewa BADO...infections,psychological trauma,kutoka damu nyingi,nk ni vitu vinajirudia consistently ndani na across FGM studies, ukivi ignore is up to you..

Nimeshangaa kitu madhara ya kisaikolojia eti hayaonekani siku hio hio,mnhhhhhhhh hivi unajua kisaikolojia damage ni kubwa inayoweza kulast life time?, nilichokuelewa unachukulia ukeketaji ni social function,watu wana enjoy kupata wakati wa kusocialize na kuja pamoja,hufikirii yule msichana mmoja ambae maisha yake yameharibiwa siku hio ili watu wanywe wafurahi..mkuu ombea binti yako apate mtu anayetoka kabila lako au mwanaume 'understanding' ...otherwise,una compromize furaha ya maisha ya ndoa ya binti yako UNECCESSARILY......tuambiane tuu....
 
Aisee!! Nimesarenda. Nimejaribu kuzungumza uhalisia matokeo yake nimeishia kupondwa kana kwamba kuna mahali nafaidika na huo ukeketaji. Kila mtu abaki na imani yake. Wewe amini kwamba mimi nashabikia ukeketaji, na mimi niendelee kuamini ninachokiona kwenye jamii, full stop.
 

Wewe kushabikia ama kutoshabikia ukeketaji haiongezi au kupunguza au lolote uko free kuongea lolote, hatuangalii wangapi wanashabikia ukeketaji,tupo hapa kudiscuss harmful effects of FGM,
 
Ni ukweli ndivyo wanavyofanya. Kila mtu na vifaa vyake. Wakimaliza wanaviacha hapo kwako wanahamia kwa mwingine. Wanatumia vifaa vyake mpaka zoezi linamalizika. Na wanachoma sindano za kuzuia damu kuvuja sana na kuwahi kukausha kidonda.
 
Hyo clitoris wanayotoa ndio huongeza Raha ya tendo kuliko chomeka chomoa, pia kiukweli huko chini kukikatwa hamu ya tendo na kuathirika kisaikolojia kuko nje nje, ndio nasema Bora wa huko kijijini wanaolewa na watu wa humo, humo wakija mjini ni kupata fedheha, nimeshuhudia mabinti wadogo wa kimasai wakimwagika damu nyingi Hadi kuongezewa damu baada ya hilo kovu kuchanika. In short inasikitisha
 
Ndugu hao wanawake wasiolalamika wamedaganyika na hawana elimu ya kutosha kuhusu hyo kitu. Wanawake kutokulalamika haimaanishi hilo jambo ni sahihi. Halafu na wewe kutumia JF bado hujaelimika una support huo ujinga utakuwa unatokea Mara huko hata watu wakiwa ma prof huwa hawaelimiki ujinga uko pale pale.
Eti tohara ya Sasa hivi ni nzuri kuliko zamani na wanawake hawalalamiki, very shame
 
All in all hiyo mila haikufi leo wala kesho. Maana watoto wenyewe wanapenda, wazazi wengi bado wanapenda, wale wazee wa kimila ndio huwaambii kitu (labda wazee wa kimila wote wafe) kwasababu kwanza watu wanawaogopa, halafu hawa viongozi nao ndio huwa wanakaa na kupiga nao story kupanga mikakati. Kipindi cha kampeni wazee wa kimila wanahusika sana sana kuliko unavyodhani. Sasa wazee wa kimila washakusaidia kushinda uchaguzi utaenda kuwakataza kuhusu FGM yani haiwezekani.
 
Nikukumbushe tu. Katika kila kauli usiyoipenda jaribu kuchunguza angalau zuri ndani yake. Mnanilisha sana maneno ndugu zanguni. Kwanza tangu mwanzo wa mjadala hakuna sehemu nimesema tohara kwa watoto wa kike ni nzuri, hakuna niliposema nasapoti mila hii.

Ni kweli natokea mkoa tajwa hapo juu lakini tusilazimishane kukubaliana kila kitu. Jaribu kukosoa bila matusi kwani hata kama mtu amekosea ukishatumia lugha/tendo baya unakuwa umekosea pia. Kutumia jf sio kipimo cha kuelimika, tukumbuke tu kwamba siku hizi wimbi la wanafb kuvamia jf ni kubwa. Goodmorning.
 
Kisimi ndio kila kitu na ndio maana wanakitoa hicho,
Au hujui sababu zipi zinawafanya wawakekete hao watoto?
 
Faida ya kukeketwa ni nn? Na nani anapata hiyo faida, tuanzie hapo.
Hakuna faida yeyote ya maana....na wanaofanya huo mchezo hawataki kusema ukweli....kimsingi utamaduni huu unatokana na wivu tu wa wanaume wenzetu....utamaduni huu ni uliasisiwa na baadhi ya Wazee wetu kipindi cha nyuma... lengo ni kudhibiti hisia za mapenzi za mwanamke....ili asitoke nje ya ndoa...hasa mumewe anapokuwa hayupo karibu....labda kaenda kwenye Vita ...au utafutaji wa maisha wa kawaida....kama inavyojulikana kisimi ndio sehemu yenye hisia kali za mapenzi kwa mwanamke....takribani Neva za hisia 8000... Ni nyingi sana hizi....mara mbili ya tulizonazo wababa....ndio maana wababu wakaona wazipunguze kwa kukeketa...ili wa kina mama wawe na utulivu....kwa Mimi hasara ni nyingi kuliko faida.
 

Mosi kabisa, "sanitized FGM" au "Clinical FGM" ipo sana. Hata Kenya kuna daktari anayepromote hilo. Haimaanishi kuwa kukeketa mtoto wa kike ni sawa. Sasa hivi makabila mengine yamehamia kukeketa watoto chini ya mwaka ila waume zao na jamii zisijue! Huo ni unyama wa hali ya juu!

Pili, madhara niliyoyaongelea yapo na nimeshakutana na kina mama na mabinti wakanielezea. Nimeshazungumza na wanandoa wanaopata shida kwa sababu ya hili. Kuna wakina mama nimeongea nao wakanieleza jinsi waume zao walikuwa wanawapiga kisa hawafurahii tendo la ndoa kwa hiyo mwanaume anajihisi siyo rijali anamalizia hasira kwa mkewe. Wengine wameachika kwa sababu hiyo.

Halafu, kuna aina nne au zaidi za ukeketaji na zote zinamadhara kwa upana wake kutokana na aina aliyofanyiwa. Hata kama kuna wanaopona na kuendelea na maisha yao, pia kuna wanaoumizwa. Ni kitendo kisicho na tija yoyote, why the risk? Kama ni mila nyingine za kumuandaa binti kimakuzi, au kumfundisha mila na taratibu za jamii yake, kwanini zisifanyike bila kumuumiza? Mila gani zinazohitaji damu ya mtu na ulemavu wa kudumu?!

Na sasa hivi kuna baadhi ya waganga wanaoshirikiana na mangariba kununua sehemu zilizokatwa kwaajili ya ushirikina.

Halafu licha ya kufanyia utafiti hili eneo kwa zaidi ya miaka miwili, nimetoka kwenye jamii inayokeketa ila nashukuru familia yangu imekataa kujihusisha na huu unyama.
 

Wewe ni 100% psychopath!
 
Ni kweli hii mila haifi leo wala kesho. Ila nitatofautiana na wewe kwenye kuipenda.
Hakuna kitu muhimu kwa asilimia kubwa ya binadamu kama kuwa sehemu ya jamii. Jamii hukupa ulinzi, upendo, support ya maisha, nk. Kutengwa na jamii yako ni kitu kinachoumiza sana. Hii ni nature ya wanyama walio wengi, ikiwamo binadamu. Sasa imagine, ukienda kinyume na jamii yako ukatengwa hadi na familia yako. Unafanyiwa kila aina ya masahibu ilimradi kukufedhehesha na kukuonyesha hauna thamani yoyote. Halafu ukute hauna kwingine kwa kukukimbilia, utaishia kukubali tu ili usitengwe na jamii. Saikolojia na sosholojia ya hili swala ni pana sana.

Hilo la siasa nina kubaliana na wewe asilimia mia moja. Ndio maana nilipomsikia Mwita Waitara anasupport ukeketaji kwenye hadhara nikajua tu anatafuta kura.

Kazi ipo kubwa sana. Labda jitihada zikiendelezwa, vizazi vitano mbele vitakuwa na ahueni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…