Kwa maelezo yako..Japo SI dhahiri inaoneka unaona ni kitu Cha kawaida kupunguza maumbile ya kike.
Kwangu ni kitu cha kawaida kwakuwa nimekulia mazingira inakofanyika lakini hakuna sehemu niliyosema naunga mkono. Hii ni mila ya baadhi ya makabila hapa nchini hivyo kwabaadhi ya mabinti hufikia hatua ya kutoroka na kwenda kufanyiwa au wengine huomba wenyewe wafanyiwe.
Tofauti ya zamani na sasa ni kwamba zamani binti alikatwa na sehemu ya kisimi kuondolewa, lakini siku hizi ni kuchanjwa tu hii huitwa kiccm (enzi za mzee wa msoga na ufisadi iliomekana jambo lolote la maana linaweza kufanywa kizembe na kusiwe na shida).
Ilikuwa nadra sana baada ya binti kukeketwa umkute anacheza ngoma ya asili (litungu) tena mchana wa jua kali kwani damu huvuja sana lakini kwasasa wanaume ndio hufanyiwa tohara asubuhi na mapema ili kabla ya jua kuwa kali wawe kivulini (nyumbani) ilhali kwa mabinti hufanyiwa kuanzia saa nne hadi mchana kulingana na idadi na eneo tukio linapofanyika.
Naomba nihitimishe kwakusema kuwa kwasasa madhara ya ukeketaji katika uhalisia wake ni madogo sana kuliko inavyoelezwa kwa vyombo vya habari. Kama nasema uongo nawaruhusu watafiti waingie kazini. Mchukue mwanamke aliyefanyiwa ukrketaji kuanzia 2000 kurudi nyumba na aliyefanyiwa kuanzia 2002 kuendelea kisha linganisha maumbile yao kwa kuzingatia mikato ya kisimi. Utagundua kabisa sikuhizi ni kama mabinti huenda eneo la tukio kutimiza mila na desturi na sio kukatwa sehemu zao. Zamani mwanamke anakaa ndani hata miezi miwili akiuguza kidonda wakati kwasasa baada ya wiki moja tu mabinti huanza kubananishwa uchochoroni au magetoni kwa wanaume.
Nimeandika matusi wanajf mnisamehe, kuna maneno ambayo nimelazimika kuyatumia ili nieleweke. Sio kwamba nafurahia lakini huo ndio uhalisia hasa kwa mila za kwetu wakurya (hasa wanyamongo) ila kwa koo zingine sina uelewa nako kwakuwa koo ya wanyamongo na watimbalu (wakira kwa mbali) huwa na tamaduni zinazoingiliana na hata maeneo yao yameendelea kidogo hii huwafanya kutotumia nguvu sana kwenye tohara.
Kwakuchomekea tu. Zamani kijana ili aonekane jasiri na ametimiza mila ilikuwa lazima atahiriwe kimila, wale waliotahitiwa hospitali ilifika mahali wakawa wanatengwa ama kutukanwa na wenzao wa rika sawa (saiga) na ilip3leka baadhi kurudiwa upya kutahiriwa na wazee. lakini siku hizi ni ngumu kukuta haya yakifanyika isipokuwa kwa kutaniana tu na ukimtukana mwenzako kwakuwa tu alitahiriwa hospitali utajuta.