Katikati ya dagaa wazuri na dagaa wabovu sokoni

Katikati ya dagaa wazuri na dagaa wabovu sokoni

Barnabas Mashamba

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2020
Posts
1,112
Reaction score
3,020
Nikiwa natembea sokoni (maeneo mengine huitwa gulioni au mnadani), katikati ya soko kulikuwa na kinjia (vile vinatengenezeka kwa watu kupita eneo hilo mara kwa mara).

Kinjia hicho kilikuwa kinatenganisha sehemu mbili za soko. Upande mmoja kulikuwa na biashara zikiendelea. Waliokuwa wanauza bidhaa karibu na kinjia hicho walikuwa ni wafanyabiashira wa dagaa wale wa ziwani (hasa ziwa Victoria). Dagaa hao walikuwa ni wazuri sana machoni mwa mtazamaji, unaweza hata kuwatafuna kabla ya kupikwa.

Upande wa pili wa kinjia, lilionekana dampo, lakini si la kuchimbwa bali dampo linalotokea kwa mrundikano wa takataka. Asilimia kubwa ya takataka ilikuwa ni dagaa waliooza. Yaani, dagaa waliokaa muda mrefu pasipo kununuliwa, walioza na hatimaye kutupwa katika dampo hilo.

Ajabu lakini kweli

Rundo la dagaa wazuri lilikuwa na ukubwa sawa na rundo la dagaa walioharibika.

Aaaarrrrrgggggg!!!!!!!
 
Back
Top Bottom