Katika watu ambao niliamini wakiondoka CHADEMA na yenyewe itasambaratika ni Dr. Slaa

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,227
16,178
Niliwahi kuhisi slaa anaweza kuisambaratisha chadema kutokana na kuhisi ni mmoja ya watu wenye heshima sana ndani ya chadema lakini nilichokishuhudia juzi niliamini kabisa anaiua kabisa chadema.

Lakini baada ya saa kadhaa toka amalize kuzungumza nilitegemea kila mtu atamuunga mkono lakini mpaka sasa naona maajabu heshima ya slaa imeshuka kama theluji na hatimae anaelekea kudharaulika kabisa niliwahi kuambiwa na MTU chadema sio ya mbowe wala slaa nikambishia lakini sasa naelekea kumwamini

Sijawahi kuamini kama watu wanaweza kumpuuza kirahisi hivyo Dr slaa ama kwa hakika ccm tujiandae kuondoka madarakani kama wanachi wakiamua kumpa kura lowasa nasema tena siamini kama slaa amepuuzwa kwa kasi kiasi hicho ccm ya bibi yangu babu yangu ama kweli inaelekea kupotea tuwe wapole tu/ haya ndio mawazo ya wana ccm kwa sasa na nimeitoa kwa mmoja wao
 
Slaa kaondoka na watu wengi ambao ndio mtaji wenu kwenye kura. Subiri matokeo baada ya uchaguzi ndipo utakapojua impact ya kuondoka kwake

Hizo sasa ndoto, mara Chadema haina watu wengi mara Slaa kaondoka na watu wengi. Tushike lipi! Kaondoka na.watu wengi kwenda wapi?? Hao vijana mliowakodisha. Haya tumewaumbua sasa
 
ki ukweli sisiemu inachukiwa ile mbaya. Na Ukitaka uonekane wa maana sifia Ukawa, nenda kariakoo.:A S shade: na pondea CCM. Vijana wa Dotcom wanaikubali UKAWA ile mbaya. watu washachoka na ccm. watu kweli wanahitaji mabadiliko. :bange:. Pia ccm haina guts ya kumkosoa EL kwa lolote, labda iwatumie viongozi na wanachama wa Ukawa ili kummaliza EL.
 
tehetehetehe ,.... mliandaa maandamano mwisho wa siku ikawa aibu tupu ... endeleeni kununua Tshirt za CHADEMA ...
Slaa kaondoka na watu wengi ambao ndio mtaji wenu kwenye kura. Subiri matokeo baada ya uchaguzi ndipo utakapojua impact ya kuondoka kwake
 
Wala hajaharibu. Wafuasi wa Dr. Ni wakimya hawana muda wa kupunguza stress kupitia mtandao. Namba mtaisoma jogoo wa kwanza.
 
Badala ya CHADEMA kutikisika CCM ndo imezidi kutikisika zaidi kwa kuumbuliwa live mbinu zao zote za kupanga maandamano na kuambulia kichapo.. Mwisho wa ubaya wa CCM ni AIBU!!
 
Slaa kaondoka na watu wengi ambao ndio mtaji wenu kwenye kura. Subiri matokeo baada ya uchaguzi ndipo utakapojua impact ya kuondoka kwake
Ni aibu kujiita mwana ccm kwa sasa.Majuzi Mbinga mida ya asubuhi kuna mzee alivaa shati la ccm alizomewa mpaka akaokolewa
 
Slaa kaondoka na watu wengi ambao ndio mtaji wenu kwenye kura. Subiri matokeo baada ya uchaguzi ndipo utakapojua impact ya kuondoka kwake

Sasa hivi unasubiri matokeo ya kura tena,sio Ukawa/Chadema kusambaratika kama ulivyojitapa hapo mwanzoni kuwa mwanzoni wa Sept kutatokea mtikisiko Ukawa?
 
Slaa kaondoka na watu wengi ambao ndio mtaji wenu kwenye kura. Subiri matokeo baada ya uchaguzi ndipo utakapojua impact ya kuondoka kwake
wangapi mkuu? au wale walivalishwa tshirt ofisini kwenu wakaambiwa waandamane bila kujua? huyo mliyekuwa mnadhani ni risasi yenu ya mwisho ni mweupe kama karatasi iliyotoka kiwandani
 
Back
Top Bottom