Katika suala zima la ndoa, dini ya Kiislamu ipo vizuri

Hata mm kuliko nioe kanisani bora niende bomani yan
Ndoa zote zinaidhinishwa na Serikali.
Maana yake anayefungisha ndoa ni Serikali.
Ndio maana ukitaka kuvunja ndoa ni lazima uende katika vyombo vya serikali kama Mahakama.

Na Serikali ikijiridhisha kuwa ndoa flani ilifungwa kwa kukiuka kanuni za ndoa, inaivunja hiyo ndoa bila kujali ilifungwa Kanisani au Hekaluni.

Huko Kanisani na Misikitini viongozi wake wanaiwakilisha tu kazi ya serikali.

Hata kiongozi wa Mila anaruhusiwa kwenda Serikarini na kuchukua vyeti vya ndoa na kuwafungisha watu wake, ili mradi tu aaminike na jamii yake na Serikali.

Kuhusu kuoa wake wengi au mmoja
hii inategemea na uwezo wa Mwanaume.

Taraka haipaswi kutolewa kwa urahisi kwakuwa Wanaume wasio na busara wanatumia fimbo ya Taraka kuwaumiza wanawake.

Wengi wetu uwezo wetu ni wakuoa mke mmoja tu.
Kama ilivyoandikwa kwenye Biblia Takatifu.
 
Hakuna ndoa inayoitwa "ndoa uji" kwenye Uislamu.Hizo ni dhana potovu.Uislamu umeweka wazi sheria za ndoa na miiko yake.Huo unaousema ni uzushi tu usiokuwepo kwenye taratibu za kisheria.
Watu watajaribu kuhalalisha uzinzi wao kwa kuutolea majina tofauti tofauti.
sijaandika ndoa uji dada/kaka soma tena
 
Sema unachotaka kusema itakuwa hujui usemalo.
Sipendi nikukere, ila kiufupi tu ni kwamba sipendi kuona mwanamke ananyanyaswa, kudharauliwa, kudhalilishwa, wala kuonekana kwamba yeye si wa maana na kutumiwa kama chombo cha starehe kwa kurundikwa ndani na mwanamme ikali hana uwezo wa kuwahudumia.
 
Hakuna ndoa inayoitwa "ndoa uji" kwenye Uislamu.Hizo ni dhana potovu.Uislamu umeweka wazi sheria za ndoa na miiko yake.Huo unaousema ni uzushi tu usiokuwepo kwenye taratibu za kisheria.
Watu watajaribu kuhalalisha uzinzi wao kwa kuutolea majina tofauti tofauti.
Wallah mie sijawahi kuona
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Nawasalimu kwa jina la jamuhuri

Binafsi nimekuwa mfuatiliaji mkubwa sana hasa wa maswala haya yahusuyo ndoa lakini kwa upande wangu nimeona ndoa kwa mujibu wa dini ya kiislamu wapo vizuri sana hasa katika swala zima la:-

1)Ndoa kwa ujumla
2)Talaka

NDOA KWA UJUMLA
-Hapa napenda kuzungumzia swala zima la kuoa mke zaidi ya mmoja ama kwa hakika hii kitu ni nzuri sana.

Maana licha ya kwamba tamaa ipo kwa mtu mwenyewe lakini pia kuoa mke zaidi ya mmoja inasaidia kupunguza swala zima la michepuko.

Pia ukipata wake wazuri kwa kushirikiana nao kwa pamoja unaweza kufika mbali hasa katika swala zima la maendeleo

Lakini changamoto kubwa iliyopo hapa pindi mume anapofariki watoto kuanza kugombania mali hivyo naamini nyie ni mashuhuda kwa baadhi ya familia.

TALAKA
Sasa hapa kwenye talaka ndio wamepatia kabisa yani haiwezekani mke wangu nimfumanie ugoni halafu niambiwe kitatutenganisha kifo huo ni uongo.

Haiwezekani mke awe na tabia zisizofaa ikiwemo kudharau ndugu zangu halafu niendelee kumkumbatia kisa kifo ndio kitatutenganisha.

Kama mke kakosea umemuadhibu mara mbili ya tatu bado anafanya kosa lile lile talaka ndio halali yake.

Hii sheria ya kwamba kifo kitutenganishe imewaponza watu wengi sana hadi kupelekea wengine kuona ndoa zao ni chungu na kukimbilia kutafuta tulizo nje kisiri (mchepuko) maana wanaona maovu ya wenza wao lakini wanashindwa kuwapa talaka kwa kisingizio cha hadi kifo kitutenganishe.

Kama wewe si muislamu basi funga ndoa hata ya kiserikali lakini uweke kipengele cha kuongeza mke mwingine hapo hatokuwa na jeuri ya kuringa maana kwenye ndoa ya kiserikali hata talaka zipo.

Kwa kumalizia kwenye swala la kuoa mke zaidi ya mmoja waislamu mmeupiga mwingi sana

Kumbuka kuoa sio lazima pia ndoa ndoano

Naomba kuwasilisha
Naunga mkono hoja 100% upo sahihi mkuu...
Hakuna kufa na kuzikana hapa
 
Unaonaje? Na wanawake wangeruhusiwa kuolewa na wanaume wanne kama ilivyo kwa wanaume kuoa wanne naona hapa kama imeegemea upande mmoja mkuu.. maana kwa maisha ya sasa wanawake wana uwezo wa kufanya kazi na kupata pesa pia na wana uwezo wa kumudu wanaume wengi pia.. unalionaje? Hili mkuu na kama haiwezekani kwanini?
 
...haiwezekani mke wangu nimfumanie ugoni halafu niambiwe kitatutenganisha kifo huo ni uongo.
Huwezi kuacha kwa sababu ndogo ndogo kama dharau, ugomvi, nk..
Ila kwa habari ya uzinifu (pekee), kuachana kunaruhusiwa:

Mathayo 5:32
Lakini mimi nawaambieni, anayempa mkewe talaka, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, anamfanya azini; na mwanamume akimwoa mwanamke aliyepewa talaka, anazini.

Mathayo 19:9
..Basi nawaambieni, yeyote atakayemwacha mke wake isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, akaoa mke mwingine, anazini.”

Maana ya hiyo mistari ni kuwa kama mke akithibitika kuwa mzinzi, kumuacha ni ruksa
 
Back
Top Bottom