Katika Sikukuu hii ya Watakatifu Wote tuwaombe Julius Nyerere, Benjamin Mkapa na John Magufuli waliombee taifa la Tanzania


Hatujui wako upande gani kule walipo! Wengine kwa waliyoyafanya wanaweza kuwa upande wa motto. Hivyo tueaombee kwanza waondoke huo upande
 
Jiwe Yuko Motoni huko ,Labda awaombee Kwa Shetani Muende Motoni
 
dini ya kwanza? dini haimfikishi mbinguni mtu wewe, hata sisi tulikuwa wakatoliki kama wewe hadi tulipofunguka macho.
 

Ajali! Imani gongana hapo. Taabu hayupo aliyekwisha kwenda na kuleta mrejesho.
 
Hakuna wa kumuombea hapo kwa sababu maisha yao ya mauti walisha jiandalia wenyewe wakiwa wazima wa afya
 
Hajawa mwenyeheri.

 
Mtu akishakufa hesabu yake nayo huishia hapo anachosubiria ni hesabu ya yale aliyoyatenda, ni wajibu wako uliye hai kujiombea maana umepewa hiyo neema ya UHAI si kwa upendeleo bali kwa kusudio maalum la Mungu.
 
Huelewi mambo

Ukimuomba Babu yako unaweza ukawa tajiri sana, Humuabudu bali unamuomba akusaidie

Tofautisha kuomba na kuabudu

Hapa anaongelea wasaidie kuombea sio wao kuwaabudu

Vitu viwili tofauti

Baada ya Samweli kufa na Sauli kuachwa na Mungu sababu ya kukosa utii, Sauli alienda kumwomba marehemu Samweli aongee na Mungu amuombee msamaha.

Soma Sauli alichojibiwa na marehemu Samweli

1Samweli 28: 15-18
Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Mbona umenitaabisha mimi, hata kunipandisha juu? Sauli akajibu, Mimi nimetaabika sana; kwa kuwa hao Wafilisti wananifanyia vita, naye Mungu ameniacha; hanijibu tena, wala kwa manabii, wala kwa ndoto; kwa hiyo nimekuita wewe, ili wewe unijulishe nifanyeje.

Samweli akasema, Kwa nini kuniuliza mimi, akiwa Bwana amekuacha, naye amekuwa adui yako?

Yeye Bwana amekutendea kama alivyosema kwa kinywa changu; Bwana amekurarulia ufalme mkononi mwako, na kumpa jirani yako, yaani, Daudi.

Kwa sababu wewe hukuitii sauti ya Bwana, wala hukumtimilizia hasira yake kali juu ya Amaleki; kwa sababu hii Bwana amekutendea hili leo.
 
Kwanza,hakuna yeyote Mbinguni na Ardhini mwenye sifa ya utakatifu isipokua Mwenyezi Mungu.Anayejiita mtakatifu anajidanganya na kudanganya wenziwe pia.
Pili,wote ambao ni marehemu hawana uwezo wala fursa ya kutuombea tulio hai bali sisi ndio tunaopaswa kuwaombea.Ndugu zangu tujitahidi kusoma kujua imani zetu.Imani lazima ikubaliane na akili.Kubeba imani tu bila kuishughulisha akili ni kupotea kubaya mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…