Nyankurungu2020
JF-Expert Member
- Oct 2, 2020
- 4,086
- 6,568
Hivi mbona ni aibu kubwa sana kwa taifa kubwa lenye rasimali nyingi na utajili wa maliasili kama Tanzania kufikiria juu ya kukamua tozo toka kwa wananchi wanyonge badala ya kufikiria kutumia rasimali kama madini, uvuvi na kilimo kupata mapatoa ya kuendesha nchi.
Hayati Mwalimu na hayati Julius Magufuli walikuwa makini juu ya hili na hawakupenda kuona raia wa chini na wanyonge wakisumbuliwa kwa sababu taifa lao lina rasilimali za kutosha kujiendesha.
Ni kweli wakati wa hayati Mwalimu wananchi walikuwa wachache. Lakini alimudu kusomesha wananchi bure na matibabu bure hakukuwa na wawekezaji wakubwa wa uchimbaji madini hapa nchini. Leo hii kila kona madini yanachimbwa na raia wanapigwa tozo za kila namna.
Leo hii kuna vyanzo kibao vya mapato vya taifa letu lakini raia wanyonge ndio wananyanyaswa kwa tozo za kila namna .
Akumbumbwe hayati JK Nyerere na hayati JPM