Katika hili, namwamini Shetani


Aliwapa adhabu ya kifo baada ya kuona wangekula tunda la uzima wakaishi milele . Mwanzo 3:20

Ile ilikua tu mikwara , wote tumeona tunda alikuwadhuru bali liliwapa ufahamu kama shetani alivyosema Ila Mungu kwa kuogopa binadamu watamzidi maarifa au kufanana nae akaamua kutupa kikomo cha kuishi , soma kitabu cha mwanzo


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ajuza hakuna uzushi kwenye Biblia mtume mwenyewe ameikubali alafu wewe uliyeletewa dini na ngalawa unaita Biblia fake news alafu who is pope? Ni mtu kama wewe hebu heshimu Vitabu vya wenzio na ukiendelea nakulipua
Sent using Jamii Forums mobile app
 
 
Huwezi ogopa kitu ulicho kifanya wewe yani Mungu amwogope mwanadamu?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Biblia Ina jichanganya
 
Aliwatoa bustanini kijana soma uelewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu hakuongopa kusuhu kufa, kabla ya adam kula mti wa kati Mungu aliwaambia hawatakufa wataishi milele hii ina maana kama adam angemtii Mungu basi mpaka saivi tungekuwa nae.
kwaiyo Mungu hakuongea uongo aliwaambia mkila mtakufa na kweli adamu alikufa na eva nae alikufa na wewe mkuu utakufa.
mkuu mtoa mada uelewa wako hapo kwenye kufa ulidhani yani pale adam kaling'ata tu tunda basi palepale alitakiwa kufa, Mungu hakumaanisha hivo mkuu
 
Katika hilo bandiko umeona wapi nimeAndika hayo uyasemayo? Weka nukuu... Ukishindwa basi elewa kuwa una "hallucinations" na hiyo ni dalili kuwa u "schizophrenic".

Wewe usitake kujifanya mjanja Mimi Nina akili Mara kumi yako.Sio mpaka useme "haya papa huyo kasema hayo Na huyo ndo kila kitu kwenu " for us to understand what you are actually trying to say.Kuna "inferred meaning ".Jinsi ulivyoileta comment yako umesema eti hata papa mwenywe amethibitisha kuwa bible Ina fake news.Hapo moja kwa moja mtu mweny akili Timamu anaelewa unachojaribu ku derive hapo I.e papa ndo Ana say kweny mambo ya kikristo so Kama alisema maneno yake yana nguvu.Yes exaaaactly that's what you said indirectly tatizo unakurupuka afu unakuja kujikana mwenywe ukiona unashindwa.uwe unatuliza akili kwanza Na ufanye research yako kwanza kabla ya kutuletea hao representatives wako wa Dini Yetu unaowahisi wewe Ni representatives


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nakushauri uwe makini watu wengi si wasomaji wa biblia sasa utakuwa na cha kujibu kama wakipotea kwa sababu ya ulichoandika.Nitakujibu kwa kadili nitakavyopata muda lakini kwanza nataka wewe na wengine mjue kwamba Shetani ni baba wa uongo,lakini haimanishi shetani husema uongo muda wote.Shetani kuna muda husema ukweli kwa sababu angekuwa anasema uongo muda wote asingepata watu wa kumwamini.
Hapo nilipo highlight red acha kupotosha Mungu alitoa adhabu ya kifo kabla hata hawajala hilo tunda(Mwanzo 2:16-17),
"16Mwenyezi-Mungu alimwamuru huyo mwanamume, “Waweza kula matunda ya mti wowote katika bustani; 17lakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya, usile, maana siku utakapokula matunda ya mti huo, hakika utakufa.”

nitakuwa nakujibu kidogo kidogo kwa hiyo unatakiwa utubu umedanganya kwenye maelezo yako hapo juu.Lakini ppia nataka kujua je wewe ni msomaji wa Biblia?Kama ni msomaji kuna mambo unatakiwa uyajue,mara nyingi Mungu humpa mwanadamu kuchangua ingawa humshauri achague nini ili awe salama.Kama ambavyo wengine wamechangia Adam na Hawa walikufa,ingawa kwa mwanzoni unaweza ona Mungu alidannganya na ndivyo shetani alivyowaambia kwamba hamtakufa,kama wachangiaji wengine walivyosema hakuwaaambia watakufa muda huo huo.Lakini unatakiwa kujua kwamba Mungu huutangaza mwisho kuanzia mwanzo,aliona mbeleni watakufa ila shetani a liongelea immediately hapo ndiyo tofauti na wewe umemwamini.Hapo hakuna kipya,ule mti jina jingine ni mti wa ujuzi wa mema na mabaya ambapo baada ya wao kula tunda kweli walikuwa na ujuzi wa mema na mabaya.Kwa hiyo shetani hakuna jipya alilowaeleza isipokuwa aliwadanganya hawatakufa akimanisha immediately baada ya kula tunda,lakini baadaye walikufa.
Biblia siyo kitabu cha hadithi za kutungwa kama vitabu vingine tunaposema mtu unahitaji Roho mtakatifu akusaidie kuelewa huwa hamtueleimi,hicho kitabu si kama vy kidunia "if you can read it you can understand" siyo applicable kwenye bible.
Na hapo wale ndugu hutumia kupotosha watu,na wanaopotoshwa ni wale wakristo wenye majina ya kikristo ila hawaishi the christian life.
by the way nataka kujua wewe ni devoted christian au husoma Biblia mguu mmoja ndani mwingine nje?
 
Kupata ufahamu wa kujua mema na mabaya hiyo haiwezi kufanya uwe sawa na Mungu hapo inadhibitisha hata shetani mwenyewe alikua mwongo kwa kuwaambia wakila wangekua sawa na Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…