Katika hili, Dr. Slaa anastahili sifa!

Katika hili, Dr. Slaa anastahili sifa!

Hussein J Mahenga

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2012
Posts
751
Reaction score
656
Leo nimevuta fikra sana na hatima yake nimeona Slaa anastahili sifa na ikiwezekana anafaa kuwa rais wa nchi yetu.

Kikubwa zaidi kilichonifanya niseme hivi ni baada ya kukumbuka majirani zetu Kenya mwaka 2008 nikiwa kidato cha kwanza.Katika uchaguzi uliofanyika mwaka huo, Kibaki Mwai ndo alitangazwa mshindi dhidi ya Odinga Raila. Kutokana na madai ya kuwa Mwai hakushinda kwa uhalali, Odinga aliwaambia wafuasi wake kuwa yeye ndiye alikuwa mshindi na badala yake wananchi walimwaga damu.

Pia kumbukumbu yangu ikanijia kufikiri tukio jingine hapa kwetu Z'bar. Sharif Hamad alidai kuwa ktk uchaguzi uliofanyika mwaka 2000, yeye ndo alikuwa mshindi na hatimaye wazanzibar walimwaga damu isivyo kifani.

Ninachotaka kukizungumzia hapa ni kwamba,kiongozi anaweza akawa msomi,mwenye lundo la shahada na hata masters lakini bila kuwa na hekima na busara,huyo mtu hafai.Kiongozi anayekuwa hana huruma na roho za binadamu ama analazimisha siasa hadi kwenye uhai,huyo hafai.

Kwanini nimesema Dr Slaa anafaa kusifiwa?

Katika uchaguzi huu uliofanyika mwaka 2010 nikiwa kidato cha tatu umenifanya nimpende Slaa na kummwagia sifa kemkem japo bado nipo mwanafunzi na sijaijua vizuri siasa lakini kwa hili imenibidi leo nivunje ukimya. Tuhuma nyingi zilionekana kuwa Slaa alikuwa na kura nyingi katika majimbo mengi na hivyo angeamua kuwaambia mashabiki wake kuwa yeye ndo alistahili ushindi, sidhani kama vita vingekosekana kama kenya na Z'bar.

Mwenyezi Mungu amjalie 2015 aweze kuichukua nchi maana hata mimi nitakuwa ndiyo kwanza nimemaliza kidato cha sita hivyo nitakuwa na muda kumpigia debe. Dr Slaa ana uamuzi mzur wenye hekima na busara.Nampenda sana Slaa.
 
Ni kweli sifa mojawapo ya kiongozi bora ni kuwa na busara hata hivyo hakuna busara inayoruhusu kukubali kuporwa haki.
 
Safi sana dogo, hakikisha unakuwa sehemu ya kudai daftari la wapiga kura liboreshwe ili nawe uwe mpiga kura halali 2015.welcome to Tanzania
 
Afadhali umeuanza mwaka huu kwa kuionesha hisia zako.Lakini,Dr.Slaa ni jembe kweli ingawa ni kwasababu tofauti na zako.Yeye ni kiongozi mvumilivu na mnyenyekevu.Ni Mwalimu na mtu makini
 
Pens down, collect the papers.....
Then marking pannel inafanyakazi yake
Paper resurt
1. Mwigulu Nchemba ~ 09%
2. J. Mtatilo ~ 52%
3. Dr Lwaitama ~ 100%
4. Nape ~ 0.0006%
5. Mbowe ~ 100%
6. Sir H ~ 100%
 
Mimi nadhani utoto wako na kutofuatilia mambo kweli utakuwa umechangia kufikiri kama unavyofikiri. Kwani kenya ODINGA alipata kura ngapi na KIbaki alipata ngapi? Ni upi ulikuwa msimamo wa tume ya uchaguzi ya kenya kuhusu matokeo? Ni upi ulikuwa msimamo wa waangalizi wa kumataifa kuhusu matokeo yale?

Ni upi ulikuwa msimamo wa mashirika ya kimataifa na mataifa mbalimbali juu ya uchaguzi ule?je?unafahamu slaa alipata kura asilimia ngapi dhidi ya rais kipenzi cha watu Ndug.JAKAYA KIKWETE? JE?unafahamu nini ulikuwa msimamo wa tume ya uchaguzi tanzania na waangalizi mbalimbali wa uchaguzi?

Je? Unadhani Slaa alikuwa na haki ya kukataa matokeo;au kufanya hivyo ingekuwa ni kosa kisheria na madhara yote ambayo yangejitokeza ingekuwa ni matokeo ya kosa hilo? Kama kufanya hivyo ingekuwa ni kosa;vipi umpongeze mtu kwa kutofanya kitu ambacho hata hivyo hakutakiwa akifanye?
 
Kama kweli wewe ni mwanafunzi wa kidato chatatu bila kujali undani wa mada yako mi nakupongeza kwa kupanga angalau maelezo mazuri safi sana kijana utakuwa mfano mzuri wa eilimu yetu
 
Alikuwa hana sababu ya msingi ya kuwaambia watanzania kuwa ndiye mshindi wakati ukweli anaujua na alikuwa anaendekeza hasira za kabila lake.

Idadi ya Wabunge wa CHADEMA ndo kipimo tosha hata kwa mtoto mdogo kama wewe kuwa kura alizopata Dr. Slaa ndiyo ilikuwa stahiki yake na si vinginevyo. Hakuna mwananchi ambaye angemwaga damu wakati wengi wanajua walimpigia JK.
 
Kama kweli wewe ni mwanafunzi wa kidato chatatu bila kujali undani wa mada yako mi nakupongeza kwa kupanga angalau maelezo mazuri safi sana kijana utakuwa mfano mzuri wa eilimu yetu

Labda nami niungane na wewe kuwa amepanga vizuri maneno yake. Lakini uhalali wa alichokiandika hakipo. Huwezi kulinganisha siasa za Kenya, nchi yenye ukabila mkubwa afrika mashariki na siasa za Tanzania. Kenya wanapigia kura kabila na sio kiongozi. Zanzibar hawakumwaga damu kwa sababu eti Seif alitangaza kuwa yeye ni mshindi, bali uhasama ulioyokuwepo tangu awali baina ya CCM na CUF.
 
Ulivyopangilia hoja umethibitisha kwamba wewe si wa sekondari za kata a.k.a saint kayumba. Kama nimekosea dogo H ataniambia. Ki ukweli dakt Slaa sio tu anastahili sifa bali Anastahili heshima.Dakt ni msumari wa moto kwenye masaburi ya magamba
 
Leo nimevuta fikra sana na hatima yake nimeona Slaa anastahili sifa na ikiwezekana anafaa kuwa rais wa nchi yetu.Kikubwa zaidi kilichonifanya niseme hivi ni baada ya kukumbuka majirani zetu Kenya mwaka 2008 nikiwa kidato cha kwanza.
kama ulienda sawasawa hujarudia-rudia madarasa kama mimi basi utakuwa na miaka 18, kwa umri wako na njisi ulivyoelezea basi nakupa tano.

Tunahitaji vijana 10,000 tu kila mkoa wenye umri na mtazamo kama wa kwako, hakikisheni mnajiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura muda ukifika 2015 basi chagueni Rais atakayewakomboa, atakayewatunzia raslimali zenu, atakayerudhisha moyo wa uzalendo, atakayehakikisha kilichopo kinagawiwa sawa kwa wote -- kumbukeni nyie ndiyo wenye nchi hawa wazee baada ya miaka 20 wengi watakuwa wameitwa mbele ya haki kujibu yote waliyoyafanya duniani.

Pia kumbuka wenzako wenye umri wako wanasoma shule za kata ambazo hazina walimu, maabara kwa wanafunzi wa sayansi, hakuna mabweni hata kwa watoto wa kike wa umri wako ambao wengi wao wamepanga uraiani, hakuna maktaba nk -- hii ndiyo sera ya elimu ya CCM, ukiwauliza wanasema ni bora kuwa na hizi shule as a start rather than nothing!!
 
Kama kweli wewe ni mwanafunzi wa kidato chatatu bila kujali undani wa mada yako mi nakupongeza kwa kupanga angalau maelezo mazuri safi sana kijana utakuwa mfano mzuri wa eilimu yetu
anamzidi ujajanja ile chemba ya singinda yenye ushaidi wa cdm wakipanga njama za mauaji
 
Mi naamini Sir H katoa mada yake kwa ufasaha na weredi mkuu. ni veme ww ndo utoe takwimu unazozifahamu kuliko kufanya uchaguzi kama hesabu za "direct proportion-eti kama Wabunge wa Chadema ni wachache hivo hata Rais hawezi kuwa Chadema" unataka kuwaaminisha wana JF kuwa Rais wako alipata kura nyingi kuwapita wapinzani wake katika kila jimbo ambalo mbunge wa Magamba alishinda? Acha umagamba CCM mnalazimisha kuongoza ndo maana mko radhi kutoa vitisho kwa wananchi ili muendelee kubaki madarakani. CCM imeshakuwa chama cha kurubuni wanawake kwa kuwapa chumvi na kanga ILA MWISHO WENU UMEWADIA!
mimi nadhani utoto wako na kutofuatilia mambo kweli utakuwa umechangia kufikiri kama unavyofikiri.kwani kenya ODINGA alipata kura ngapi na KIbaki alipata ngapi?ni upi ulikuwa msimamo wa tume ya uchaguzi ya kenya kuhusu matokeo?ni upi ulikuwa msimamo wa waangalizi wa kumataifa kuhusu matokeo yale?ni upi ulikuwa msimamo wa mashirika ya kimataifa na mataifa mbalimbali juu ya uchaguzi ule?je?unafahamu slaa alipata kura asilimia ngapi dhidi ya rais kipenzi cha watu Ndug.JAKAYA KIKWETE? JE?unafahamu nini ulikuwa msimamo wa tume ya uchaguzi tanzania na waangalizi mbalimbali wa uchaguzi?je?unadhani slaa alikuwa na haki ya kukataa matokeo;au kufanya hivyo ingekuwa ni kosa kisheria na madhara yote ambayo yangejitokeza ingekuwa ni matokeo ya kosa hilo?kama kufanya hivyo ingekuwa ni kosa;vipi umpongeze mtu kwa kutofanya kitu ambacho hata hivyo hakutakiwa akifanye?
 
Mi naamini Sir H katoa mada yake kwa ufasaha na weredi mkuu. ni veme ww ndo utoe takwimu unazozifahamu kuliko kufanya uchaguzi kama hesabu za "direct proportion-eti kama Wabunge wa Chadema ni wachache hivo hata Rais hawezi kuwa Chadema" unataka kuwaaminisha wana JF kuwa Rais wako alipata kura nyingi kuwapita wapinzani wake katika kila jimbo ambalo mbunge wa Magamba alishinda? Acha umagamba CCM mnalazimisha kuongoza ndo maana mko radhi kutoa vitisho kwa wananchi ili muendelee kubaki madarakani. CCM imeshakuwa chama cha kurubuni wanawake kwa kuwapa chumvi na kanga ILA MWISHO WENU UMEWADIA!
hiyo hoja ya wabunge umeleta wewe.mimi sijazungumzia wabunge hapa.
 
uchambuzi mzuri dogo, upo kidato cha 5 au 6 bilashaka ila uchambuzi wako umeenda shule hasa, umewazidi hata le mutuz aliyekaa ulaya miaka 30 na madigrii yake hahahahahahaha
 
Back
Top Bottom