Katibu wa tlp songea mjini naye atimkia chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Katibu wa tlp songea mjini naye atimkia chadema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Stephano Mango, Apr 23, 2012.

 1. S

  Stephano Mango Verified User

  #1
  Apr 23, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Na Stephano Mango, Songea
  KATIBU wa Chama Cha Tanzania Labour party (TLP) jimbo la Songea mkoani Ruvuma Joseph Mkondora (72) ametangaza kujivua uwanachama wa chama hicho ambacho amedai kuwa kimepoteza mwelekeo na badala yake ameamua kujiunga na Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) ambacho ndio chama pekee cha upinzani kinacho onyesha kwa dhati dira ya maendeleo kwa watanzania .
  Akizungumza na waaandishi wa habari jana kwenye hoteli ya Majimaji mjini Songea Mkondora alisema kuwa kwa kauli yake yeye mwenyewe ameamua kujivua uwanachama wa chama hicho na kujiunga na CHADEMA kwa sababu mwenyekiti wa TLP Taifa Agustino Liyatonga Mrema tangu achaguliwe kuwa Mbuge wa jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro ameshindwa kabisa kuangalia hali halisi ya TLP inavyoendelea kudorola kwenye jimbo la Songea mjini na badala yake anaonekana kuwa ni wakala wa chama cha CCM.
  Mkondora ameeleza zaidi kuwa chama cha TLP katika Jimbo la Songea mjini mpaka sasa siku hadi siku kinaendelea kupoteza mwelekeo kwani hali ya kisiasa sio nzuri kabisa licha ya kuwa taarifa ya hali hiyo alicha ipeleka makao makuu ya chama cha TLP lakini mpaka sasa hakuna majibu ya aina yeyote yaliyoletwa.
  Alisema kuwa amekuwa akifanya mawasiliano ya mara kwa mara na TLP makao makuu kuelezea hali halisi ya mwenendo mzima wa chama lakini jambo la kushangaza uongozi wa chama hicho umekaa kimya kabisa
  “Ndugu zangu waandishi hali ya TLP jimbo la Songea mjini iko taabani kisiasa kwani hapo awali ilikuwa na wanachama zaidi ya elfu saba lakini hivi sasa chama hicho kimebakiwa na wanachama kumi na moja tu ndio maana kwa ukimya wa uongozi wa TLP makao makuu chini ya Mwenyekiti wa chama hicho Agustino Mrema unahofiwa kuwa umekuwa ni mawakala wa CCM ambao umekuwa ukitengeneza mazingira ya wanachama wake kujiondoa” alisema Mkondora
  Alifafanua zaidi kuwa kwa muda mrefu amekitumika chama hicho akiwa kiongozi kwa nafasi hiyo lakini tangu mwenyekiti wa TLP Taifa Mrema alipochaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Vunjo ameonekana kuwa hakijali kabisa chama chake na badala yake anaonekana kuwa ni mpiga debe wa CCM kwenye jimbo hilo.
  Mkondora amesema kuwa kutokana na hali hiyo iliyopo ndani ya TLP ameamua kwa dhati kukiama chama cha TLP na kujiunga na Chadema ambako amepokelewa kwa baraka zote na sasa hivi anatarajia kukabidhi mali za chama cha TLP ambazo alikuwa anazitunza ambapo alizitaja kuwa ni Kadi za chama hicho, Majarada ya ofisi , Vitabu mbalimbali vikiwemo vitabu vya katiba ya TLP, ikiwepo samani za ofisi pamoja na bendera moja ya TLP kwa mwenyekiti wa jimbo la Songea mjini Daudi Mpangala ambaye naye anasita kukabidhiwa mali hizo.
  Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama hicho jimbo la Songea mjini Daudi Mpangala alipoulizwa na www.stephanomango.blogspot.com kuhusiana na kujivua uwanachama Katibu wake Mkondora alisema kuwa ni vigumu yeye kuzungumzia kwa wazi kiasi hicho lakini anatarajia kuitisha kamati yake ya utendaji ili kupata ufafanuzi wakujivua uwanachama kiongozi huyo.
  Hata hivyo Katibu wa chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) jimbo la Songea mjini Masumbuko Paul Masumbuko alithibitisha kumpokea Joseph Mkondora ambaye alikuwa ni mmojawapo kati ya wanachama wapya 52 wakiwemo mabalozi toka CCM ambao waliojiunga na chama hicho wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa kujaza nafasi ya udiwani kata ya Lizaboni ambayo iliachwa wazi na Ali Manya aliyefariki dunia miezi sita iliyopita ambapo katika uchaguzi huo mgombea udiwani kupitia chadema Alanusa Mlongo aliibuka kuwa mshindi kwa kumwaga mgombea wa udiwani kupitia CCM George Odo Mbunda.
  Mwisho.
   
 2. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #2
  Apr 23, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  Chadema oye
   
 3. STK ONE

  STK ONE JF-Expert Member

  #3
  Apr 23, 2012
  Joined: Dec 31, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Let them come....all of them...they should come...
   
 4. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #4
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  If they all join CHADEMA then there would be no need of multi-partism

  Karibu Nyumbani kamanda
   
 5. D

  DOMA JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 946
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Karibu sana
   
 6. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #6
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Aiseeeeee sasa CCM wanafanyaje Mungu wangu? Mafilili yuko wapi sijui
   
 7. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Kokoro la CDM ni kiboko, linabeba kila kitu humo njiani. Nilidhani ni CCM pekee kumbe linawakumba hadi wana TLP, sasa naanza kuogopa wavuvi haramu wa makokoro kule ziwani...
   
 8. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Miaka 72!!!!!???? umri umekwenda hatujui kama akili inakuwa timamu kwa binadamu wote at this age.
   
 9. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Mbona mshauri wenu mkuu ni Kingunge? Unajua umri wake? Mzee kuliko reli ya kati!
   
 10. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  ​Babu yako ana miaka mingapi? Je hana akili timamu?
   
 11. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #11
  Apr 23, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,394
  Trophy Points: 280
  chadema inapokea kada zote za watu,ila vijana ndio wanakua ktk day to day jobs!wazee baraza la ushauri
   
 12. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #12
  Apr 23, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,908
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  Malecela ana umri gani?Pius Msekwa ana umri gani?wana akili timamu? Nipo pamoja na Masumbuko na hivi karibuni tunaenda Mletele kwenye uchaguzi wa diwani.Tutachukua tena.Mikakati yetu kapuni lakini tutawaliza tena.
   
 13. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #13
  Apr 23, 2012
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Safi chadema songea andaeni vijana na hao wazee wanaweza kutumika kama washauri.
   
Loading...