Katibu wa Itikadi CCM, Shaka kwa Wasira: Nitaendelea kujifunza ili niwe bora zaidi

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
439
742
LUMUMBA DAR ES SAALAM

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndg Shaka Hamdu Shaka leo 25 Mei 2021 ametembelewa na kufanya mazungumzo na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM ya Taifa Ndg Steven Masato Wasira katika ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es salaam.

"Umefanya kazi nzuri sana ukiwa Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar na baadae Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa. Ulichapakazi ya kijasiri, ukijibu mapigo ya upinzani kwa wakati na kwa nguvu ya hoja. Umekuwa ukipangua hoja kwa mirejesho ya kisiasa, kihistoria aidha ya TANU au ya ASP endelea hatuna hofu nawe kwenye nafasi hii" Mzee Masato Wasira (MNEC)

" Siku zote wanasiasa mahiri na mashuhuri sana duniani wamejifunza, kuelekezwa, kuandaliwa, kukoselewa na kushauriwa lakini hatimaye hufahamu na kuwa mweledi hasa ukikubali kujifunza toka kwa wanasiasa waliokutangulia kwani hata walimu nao wana wakufunzi wao, kwa uwezo MwenyeziMungu sitawangusha" Shaka Hamdu Shaka. Katibu NEC Itikadi na Uenezi

#ChamaImara #KaziIendelee
#KaziImepataMfanyakazi

IMG_20210525_172807_164.jpg
IMG-20210525-WA0070.jpg
 
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa - Itikadi na Uenezi Ndg. Shaka Hamdu Shaka leo 25 Mei 2021 ametembelewa na kufanya mazungumzo na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM ya Taifa Ndg. Steven Masato Wasira katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar Es Salaam.

Katika mazungumzo yao Ndg. Wasira ameeleza na kumumwagia sifa lukuki Ndg. Shaka kwa kazi alizozifanya vyema katika kipindi cha nyuma na kueleza wazi kuwa hawana hofu naye katika nafasi anayoitumikia kwa sasa.

Ndg. Wasira amesema, "Umefanya kazi nzuri sana ukiwa Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar na baadae Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Taifa. Ulichapakazi ya kijasiri, ukijibu mapigo ya upinzani kwa wakati na kwa nguvu ya hoja. Umekuwa ukipangua hoja kwa mirejesho ya kisiasa, kihistoria aidha ya TANU au ya ASP endelea hatuna hofu nawe kwenye nafasi hii."

Ndg. Shaka ameahidi kuwa hatawaangusha na ataendelea kujifunza mambo mbalimbali.
Ndg. Shaka amesema "Siku zote wanasiasa mahiri na mashuhuri sana duniani wamejifunza, kuelekezwa, kuandaliwa, kukoselewa na kushauriwa lakini hatimaye hufahamu na kuwa mweledi hasa ukikubali kujifunza toka kwa wanasiasa waliokutangulia kwani hata walimu nao wana wakufunzi wao, kwa uwezo MwenyeziMungu sitawaangusha."

Kazi Inaendelea, Tufanye kazi kwa maendeleo yetu binafsi na taifa.

IMG-20210525-WA0167.jpg
 
Wewe Hujui kuwa Wassira ni Team Msoga wa kutupwa? Kumnasibisha na JPM ni kuonesha kiwango kikubwa cha ujinga wako.
Hizo timu za ndani kwa ndani ni zenu. Mkiparurana ni wenyewe wandugu. Tusiyotaka hata kuisikia ni timu Mwendazake wa kutesa na kuua watz wenzake.
 
Naona mzee anajaribu kutengeneza njia ya 2025.

Make mkakati wake sasa anamwandaa mwanae kuja kugombea jimbo la BUNDA MJINI 2025.

Juzi kati ametoka kupambana kwenye uchaguzi wa mwenyekiti wa CCM wilaya ya BUNDA amefanya figisu yeye na Charles KAJEGE wakampitisha SOSPETER MASAMBU GOMBOROJO kuwa mwenyekiti CCM wilaya ya BUNDA kwenye uchaguzi Mdogo.

Naona mzee anapambana mapema kutafuta huruma ya chama kwa mwanae.
 
Huyu ni kati ya watu ambao zilikuwa haziiviani na mwendazake. Waanaanza kujitokeza mmoja mmoja kama panya wanavyofanya baada ya paka kuondoka.
Hawa ndio aliowasema kuwa wanawashwa washwa! Kuna siku alikataliwa kuingia
Ikulu kwenye mkutano wa NEC kwani JIWE alikua Na taarifa zake kuwa Kikwete alikuwa anamtumia kuleta hoja za Membe kikaoni ili kumtetea!!
Wasira awamu zote bado yupo!!!
 
Naona mzee anajaribu kutengeneza njia ya 2025.
Make mkakati wake sasa anamwandaa mwanae kuja kugombea jimbo la BUNDA MJINI 2025.
Juzi kati ametoka kupambana kwenye uchaguzi wa mwenyekiti wa CCM wilaya ya BUNDA amefanya figisu yeye na Charles KAJEGE wakampitisha SOSPETER MASAMBU GOMBOROJO kuwa mwenyekiti CCM wilaya ya BUNDA kwenye uchaguzi Mdogo.

Naona mzee anapambana mapema kutafuta huruma ya chama kwa mwanae.
Duuuuuuuuh
 
Tunakuomba tu mzee wasira usipandikize siasa ngumu za mwenyekiti aliyepita. Watanzania tumechoka masiasa ya namna hiyo.
Unafiki huo;
Umechoka na nani wewe?, In five years tu, how about 60yrs past?
 
CCM itadumu sana na wale wazungu waliomwambia JK kwanini ni chama kinachodumu wakati vingine vimeshakufa, watakufa wakikiacha kipo hai.

Ni chama chenye uwezo mkubwa wa kurithisha vipaji (succession plan). Mwaka 1973 wakati Wassira akiapishwa na RIP Nyerere na kuingia serikali, sidhani kama Shaka alikuwa ameshazaliwa. Leo hii wamekaa pamoja wakiongelea siasa, uzoefu wa mkongwe mmoja unahamia kwa kijana mmoja.
 
Ukiachana na Siasa Wasira hakuna kingine anakijua...Wasira ni siasa siasa ni Wasira.!
 
eti CCM is going back to the root...yetu macho!!
Huyu mzee naye ana jipya lipi kwa mfano !!
 
CCM itadumu sana na wale wazungu waliomwambia JK kwanini ni chama kinachodumu wakati vingine vimeshakufa, watakufa wakikiacha kipo hai.

Ni chama chenye uwezo mkubwa wa kurithisha vipaji (succession plan). Mwaka 1973 wakati Wassira akiapishwa na RIP Nyerere na kuingia serikali, sidhani kama Shaka alikuwa ameshazaliwa. Leo hii wamekaa pamoja wakiongelea siasa, uzoefu wa mkongwe mmoja unahamia kwa kijana mmoja.
Hakika tunaiishi ahadi ya kuwa binadamu wote ni sawa. Chama Imara, vyama vingine vinatakiwa kujifunza.
 
Back
Top Bottom