Dkt. Chaula ahimiza uwajibikaji wa pamoja Shirika la Posta

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
879
956
DKT CHAULA AZUNGUMZIA UWAJIBIKAJI WA PAMOJA POSTA

Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Zainab Chaula ameitaka Menejimenti ya Shirika la Posta Tanzania kufanya kazi kwa tija, bidii, weledi na uwajibikaji wa Pamoja ili kuleta matokeo mazuri kwa Shirika na maslahi mapana ya Taifa

Hayo ameyasema leo tarehe 20 Julai, 2021 wakati wa kikao na Menejimenti ta Shirika la Posta Tanzania, katika Makao Makuu ya Shirika hilo, jijini Dar es Salaam.

Dkt Chaula alisisitiza uwajibikaji na kujituma kwa viongozi hao na kuwaasa kuacha Kufanya kazi kwa mazoea, bali waongeze ubunifu na washirikiane “Team Work” katika kutimiza majukumu yao ili kuyafikia malengo yaliyowekwa Shirika.

“Lazima tuwajibike tumsaidie Postamasta Mkuu, hii kazi sio yake peke yake mshirikiane kulipeleka Shirika mbele na tuyafikie malengo tuliyowekewa”. Alisema Dkt. Chaula.

Aidha, Dk Chaula alisema kuwa Shirika la Posta lina rasilimali nyingi ambazo zikitumika vizuri zinaweza kuleta tija na kuongeza mapato ya Shirika na hata kuchangia kwa kiasi kikubwa pato la Taifa, hivyo alisistiza Uwepo wa usimamizi wa kutosha na kuimarisha mifumo ya udhibiti wa uendeshaji wa rasilimali hizo kila mwananchi na Taifa wote wanufaike.

“Wasiwepo wachache wanaonufaika na rasilimali za Shirika letu halafu wengi wanakosa, simamieni rasilimali hizi na mhakikishe mnaweka mifumo ya udhibiti na miongozo itakayowezesha kila mtu kunufaika na rasilimali zetu”. Alisema Dkt. Chaula.

Kwa upande wake Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Macrice Daniel Mbodo alihitimisha kwa kusema kuwa amefurahishwa na ujio wa Katibu Mkuu Dkt Zainab Chaula na kuahidi kufanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa ili Kuongeza uzalishaji na mapato ya Shirika kwa maslahi ya Taifa.

“Kwa niaba ya Menejimenti ya Shirika la Posta tumeyapokea maelekezo yote uliyotupa na kwa kuwa tumeweka nia ya kuleta mabadiliko katika Shirika letu tunakuahidi kuanza utekeleza wa maagizo hayo mara moja, hata hivyo tunakushukuru mno kwa kutenga muda wako kufika hapa leo”. Alisema Mbodo.

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano;
Shirika la Posta Tanzania.
20 Julai, 2021.


IMG_20210720_230006_640.jpg
 
Back
Top Bottom