Mindi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2008
- 3,523
- 4,991
Nimemsikiliza Dr. Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM, akiongea na Vyombo vya habari. Pamoja na kutumia usomi wake kutetea "sera" za CCM, ikiwa ni pamoja na zile za kupora viongozi wa upinzani, ametumia nafasi hiyo pia kujitutumua kwa kutumia mgongo wa Marehemu Profesa Samir Amin, Mungu amweke mahali pema peponi.
Dr. Bashiru alianza kwa "kutangaza" habari za kusikitisha za kifo cha nguli huyo wa siasa za kimapinduzi Afrika na Dunia nzima, na kupenyeza kwamba alipigiwa simu na Profesa Issa Shivji. habari hiyo fupi ilikuwa hasa na lengo la kujinasibisha na Msomi huyo, ambaye kwa bahati mbaya yale ambayo aliyasimamia ni tofauti kabisa na yale ambayo Dr. Bashiru anayasimamia kwa sasa. Profesa Samir amedumu na misimamo yake mpaka kifo kimemkuta, wakati Dr. Bashiru, ambaye alishiriki kumwalika Profesa Samir kuwa Kigoda cha mwalimu Nyerere mwaka 2010, akishirikiana na Profesa Issa Shivji, amesaliti kile alichokiamini, angalau hadharani, na kukimbilia kutumikia Chama ambacho kinasimamia ukandamizaji, uporaji wa haki, rushwa, utesaji na mengine maovu zaidi. Mchambuzi mmoja ana mweleza Profesa Samir kama ifuatavyo:
"Amin believed that the world capitalism – a rule of oligopolies based in the rich world – maintains its rule through five monopolies – control of technology, access to natural resources, finance, global media, and the means of mass destruction. Only by overturning these monopolies can real progress be made." [Rejea hapa]
Sasa CCM ndiyo inasimamia hayo hayo ambayo Profesa Samir alipinga na alihubiri yang'olewe ili kuleta maendeleo ya kweli ya wanyonge. CCM kupitia serikali yake inakandamiza vyombo vya habari, inakandamiza mitandao, Badala ya kutumia rasilimali za nchi kwa masilahi ya taifa zima, tunashuhudia watanzania wakiishi maisha magumu kutokana na mipango isiyoeleweka na isiyokuwa na vipaumbele vya kitaifa, bali kufuata matakwa ya mtu mmoja vile anavyojisikia. Kauli ya Rais Magufuli ndiyo sheria. Serikali ya CCM inasimamia uvunjaji wa sheria na katiba ya nchi, kwa kuvuruga mfumo wa vyama vingi.
Kimsingi CCM siyo tena chama cha siasa, kwa sababu haiwezi kusimama wala kufanya siasa bila kutumia Polisi, vyombo vya serikali, wateule wa Rais waliosambaa nchi nzima, ambao kwa kweli ni watumishi wa umma ambao hawatakiwi kuwa upande wa chama cha siasa
Kwa kumrejea Marehemu Profesa Samir Amin, Dkt Bashiru Ally anakusudia kuhalalisha usomi wake na hivyo kuutumia usomi huo kuhalalisha yale yanayoendelea hapa nchini.
Bashiru na wakubwa wake katika CCM wanajidanganya. Bashiru anajisahaulisha kwamba HUWEZI KUIDANGANYA HISTORIA.