Tatizo lako hapa ni nini?
Kwamba hukupenda Dkt. Bushiru kupigiwa simu na Profesa Issa Shivji au hukutaka aseme kuwa amepigiwa simu?
Swali zuri. Unajua ndugu, wataalamu wa kiwango cha juu katika kutoa hotuba, mhadhara au wasilisho, hutambua umuhimu wa kila kitu kinachofanyika, kila neno, kila "pause", kila "gesture". Haikuwa bahati mbaya kwamba Bashiru aliamua kuanza mkutano wake kwa kutoa heshima kwa Profesa Samir. Bashiru alipokuwa UDSM alijitambulisha kama Mwanamapinduzi, aliongelea uanamapinduzi, na alichangamana na watu aina ya akina Profesa Samir. Mara ya kwanza alipotajwa kwamba angeweza kuteuliwa ukatibu mkuu wa CCM, alikanusha vikali, akieleza kwamba yeye ni Mwanauzuoni, mtafiti, mwanaakademia, hawezi kuingia "mainstream politics".
Kama angekuwa bado UDSM, akawa katika kongamano fulani pale Nkrumah, na kutoa taarifa kama hiyo, wala isingekuwa tabu. Lakini hapo alipokuwa, Katibu Mkuu wa CCM, CCM hii ya Magufuli, ni jukwaa tofauti kabisa. Lakini pia hiyo isingekuwa shida kubwa kwangu kama ambaye angekuwa anaongea angekuwa Kinana. Kinana alijitofautisha na "Umagufuli" kwa namna iliyo wazi kabisa. Angalau amewahi kutoa kauli inayomkosoa Mwenyekiti wake moja kwa moja, pale Nkrumah, na hakuonesha kuendana na sera za sasa hivi za CCM.
Kumwongelea Profesa Samir pale ilikuwa ni kukumbushia wasikilizaji wake kwamba yeye ni yule mwanamapinduzi wa aina ya Samir, na anachokifanya kupigania yale yale ambayo amekuwa akiyapigania. Hali kwa sasa hivi siyo hiyo, na CCM ya sasa hivi siyo tena CHAMA CHA MAPINDUZI yale ambayo yalibainishwa mwaka 1977.
Suala la kupigiwa simu na Profesa Shivji pia, ni kama vile mtu anasema "Jana nilipigiwa simu na Rais Magufuli..." maana yake anataka kuonesha kwamba kuna mawasiano na Rais Magufuli. alitaka kusema kwamba bado anawasiliana vizuri na Profesa Shivji, na kwamba anakubaliana na yale ninayofanya hivi sasa. Bado ni mtu wangu wa karibu. Hilo halinisumbui kwa sababu Profesa Shivji naye anaelekea kukubaliana japo si sana na hali inayoendelea. lakini kwa kujibu swali lako, kuyasema yote hayo alikuwa na malengo yake ambayo ni kujipaka uhusika ambao hana kwa sasa
Nimecheka kidogo uliposema hii paragraph yako!
''Kimsingi CCM siyo tena chama cha siasa, kwa sababu haiwezi kusimama wala kufanya siasa bila kutumia Polisi, vyombo vya serikali, wateule wa Rais waliosambaa nchi nzima, ambao kwa kweli ni watumishi wa umma ambao hawatakiwi kuwa upande wa chama cha siasa''.
Naomba nikuulize swali, ni lini CCM haikuwa na haya uliyataja ambayo yaliifanya kuwa chama cha siasa nchini?
Mzazi wa CCM, TANU, alikuwa chama cha siasa kweli kweli, na mimi nilikuwa chipukizi wa TANU na mpaka leo naamini katika TANU. CCM ilirithi tunu za TANU, lakini imeziacha tunu za TANU. mfano mmoja ambao Dakt. Bashiru aliongelea katika kikao chake kile ni jinsi ambavyo majeshi yetu yalivyofanya kazi ya ukombozi katika nchi mbalimbali. alikuwa akijibu swali kuhusu majeshi hasa Polisi wanavyokiuka sheria na haki za binadamu.
Sasa kitu ambacho inabidi kumkumbusha Daktari Bashiru ni kwamba msingi wa majeshi yetu kwenda huko ni msingi wa TANU na baadaye CCM, kwamba BINADAMU WOTE NI NDUGU ZANGU NA AFRIKA NI MOJA. Msingi mwingine pacha na huo ni BINADAMU WOTE NI SAWA. Sasa CCM ya leo imeacha hayo yote. Nyerere aliamini katika UMAJUMUI - PAN AFRICANISM, na ndio msingi mkuu wa Kigoda cha Nyerere ambacho Bashiru amekihudumia kwa miaka mingi. CCM ya Nyerere iliheshimu hili, na ndio kisa cha kupokea wakimbizi toka nchi mbalimbali, na pia suala la URAIA halikupewa umuhimu kama wa siku hizi. Mipaka yetu iliwekwa na wakoloni ili kutugawa. Waafrika tunalo jukumu kuimarisha umoja wetu. Mwafrika toka Kenya, Uganda, Rwanda, anakaribishwa, na kama kuna tatizo la uraia linashughulikiwa kwa heshima ya binadamu huyu ndugu yetu.
CCM ya leo inatumia URAIA wa mtu kama fimbo ya kumnyamazisha. inashughulikia mambo ya WAKIMBIZI kama vile ni kero fulani tu. Umajumui ni kama umetupwa kando, na majeshi yetu yanapokwenda huko nje, ni suala hasa la kimaslahi tu. ule ushirikano na vyama vya ukombozi umewekwa kando. ndio maana tunaanzisha "uhusiano" na Morocco na Israel, ambazo bado zina makoloni, Sahara magharibi na Palestina. nimesema "uhusiano" kwa sababu Rais wetu hachelewi kupiga magoti kuomba omba kwa namna ambayo hatukuzoea huko nyuma. Tuliomba lakini na heshima ilikuwepo.
CCM ilianza kugeuka mwaka 1992, pale ilipotupa mbali kabisa AZIMIO LA ARUSHA. Hilo hata Nyerere mwenyewe alikiri kwamba CCM imeacha misingi yake. CCM ilipoteza dira, kadiri ya Katibu Mkuu wake wa tatu, Horace Kolimba (1990 -1995).
CCM kabla ya 1992 ilikuwa chama imara cha siasa, chenye misingi. leo, hata kama Magufuli anajinasibu kuirejesha CCM katika misingi, anachofanya ni kwanza kuibinafsisha iwe ya kwake. Ndiyo maana hata maamuzi yanayotakiwa kufanywa na vikao rasmi, anafanya mwenyewe tu. aliwahi kutishia kutimua wanachama waliosema "tuna imani na Lowasa" na juzi tu alitishia kutimua wabunge wa "Korosho". haya yote anayazungumza hadharani, bila kujali kwamba anachoongea ni udikteta katika chama chake mwenyewe. hata haya maamuzi kwamba wanaojiunga CCM toka upinzani, wabaki kugombea majimbo waliyokuwepo, aliamua Magufuli katika mkutano kule Arusha.
CCM ya sasa inafanya Rushwa ya kimfumo, kusimamia uporaji na wizi wa kura. siamini kama CCM ya Nyerere ilifanya hayo. kama unao ushahidi tuambie