Katibu Mkuu Dk. Slaa atoa pole Msikiti wa Mtambani, ajionea athari

Dah, pole zao nyingi hakika hao wasomi wanaotarajia kuhitimu form 4 wanahitaji msaada wa karibu ili wahitimu kwa mafanikio wakiwa na matumaini ya kufahuru mitihani yao. Nakushukuru sana Dr Slaa kwa kuguswa na kuahidi kutoa mchango wako na chama kwa ujumla ili kuhakikisha wahitimu watarajiwa wanahitimu vyema.

Hakika leo nimetambua bila kupepesa kwamba kipaumbele cha kwanza cha Chadema ni Elimu cha pili Elimu na cha tatu ni Elimu..

Long live Dr Wilbroad .P. Slaa

BACK TANGANYIKA

Umenena Kamanda
 
Hivi katika uislamu kafiri anaruhusiwa kuingia na kuonmgozwa na mashehe kutembezwa msikitini akiwa amevaa viatu?

@East African Eagle

Kwa kudra za Mwenyezi Mungu, eneo la kuswalia katika jengo hilo la Msikiti wa Mtambani halikuathirika kabisa. Hivyo Shehe Katimba alimwambia Katibu Mkuu Dk. Slaa;

"Tunaendelea kuswali kama kawaida...hapo chini. Eneo la kufanyia dua halikuathirika hata kidogo. Ndiyo sababu ya kuwaambia mje saa 11 jioni ili msi- disturb shughuli za imani, na hivi sasa mkiondoka tu tunaingia kuswali," alisema Shehe Katimba.

attachment.php
 
Duh.....hasara kweli kweli.
At least maabara zimesalimika. Kujenga shule sio mchezo kwa fedha hizi za kudunduliza jamani.
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk. Slaa amefika Msikiti wa Mtambani kutoa pole kwa waumini na viongozi wa msikiti kwa niaba ya chama kutokana na tukio la moto lililotokea juzi jioni.

Katibu Mkuu ambaye aliambatana na Mwenyekiti wa Chama Kanda ya Pwani, Prof. Abdalah Safari mbali ya kutoa pole pia alipata fursa ya kuzunguka maeneo mbalimbali kujionea madhara ya ya moto huo ambao hadi sasa kwa mujibu wa Msemaji wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam unakadiriwa kusababisha uharibifu mkubwa wa mali zenye thamani ya Tshs. Mil. 600.

Baada ya kuambiwa na Shehe Katimba mahitaji ya dharura kwa wakati huu, Dk. Slaa aliguswa na suala la wanafunzi wa Seminari ya Mvumoni kukosa vitu muhimu kwa ajili ya masomo yao hasa walioko Kidato cha Nne ambao wanajiandaa na mitihani yao ya kuhitimu, ambapo aliomba apewe tathmini ya mahitaji kwa wanafunzi hao ili chama kiweze kushirikiana na shule na wadau wengine kuwasaidia waendelee na masomo!

Hapo lazima CCM wataanza kuweweseka kwani watawaza zaidi kisiasa kuliko kangalia janga lenyewe
 
Hongera dk.slaa kwa kuwaonyesha upendo na umoja wananchi wako utakao waongoza kuanzia 2015.
 
Umenena Kamanda

Pamooja sana kichondi77 Kwa bahati mbaya sana wenzetu wa ccm hatuwaoni hapo wakishirikiana na Dr ili kutoa support kwa wenzetu Waislam kwa janga hili walilolipata naamini tungeunganisha nguvu wenzetu tungewaondolea machungu angalau kidogo

Sasa wao wameamua kususia ila ingekuwa msikiti unaomilikiwa na Bakwata ungesikia wanachangia gharama zote za uharibifu uliotokea, Huu ubaguzi ni mbaya sana.

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
Vzr sana Dr. Kwa ulichofanya na pole iende kwa ndugu zetu waislam kwa janga hili lililo tokea.
 
Pamooja sana kichondi77 Kwa bahati mbaya sana wenzetu wa ccm hatuwaoni hapo wakishirikiana na Dr ili kutoa support kwa wenzetu Waislam kwa janga hili walilolipata naamini tungeunganisha nguvu wenzetu tungewaondolea machungu angalau kidogo

Sasa wao wameamua kususia ila ingekuwa msikiti unaomilikiwa na Bakwata ungesikia wanachangia gharama zote za uharibifu uliotokea, Huu ubaguzi ni mbaya sana.

BACK TANGANYIKA
Yawezekana maccm ndio yamefanya hujuma, tunaomba uchunguzi huru ufanyike.

Msikiti wa Mbambani una histotia yake ya mapinduz kwa waislam na ni waumini wanaojitambua.

Daima huwa hawaprlekeshwi na maccm kama BAKWATA.

pia mkuu, msikiti upo katibu sana naa makao makuu ya CHADEMA.

Naomba CHADEMA, ianzishe harambe "Jenga Msikiti okoa Elimu" Tupo tayari kuchangia.

Waratibu kwa njia za online donations ,

Dr. Slaa asante... maana maccm hayana huruma hata na wanafunzi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom