Katiba Mpya: Nitakuwa Tayari Kupokea Maoni Yako Kuanzia Leo!

Hivi huu ni wakati kweli wa kupokea maoni? Tume ya warioba imefanya nini? Kama mpaka wakati huu rais amekuteua kwenda kupitia/ kujadilidi maoni ya wananchi kwa namna ya kuboresha halafu wewe unataka maoni tena kutoka kwetu..., haishangazi sana kuwa sisi tumebaki kuwa taifa la hovyo sana.
Kuna kila dalili kuwa hatutapata katiba mpya tuliyoitaka wananchi. Kumbuka hata raisi ameshawaambia kuwa mnaweza kubadili kabisa maoni yetu mkitaka (na mmeshaonyesha dalili hizo).
Nendeni Dodoma mkafanye kile chama chenu kinachowataka mkifanye...nendeni. Sisi tumekwisha malizana na Warioba. Historia itawahukumu kwa haki. Nendeni, msituchoshe!
 
Ndugu wanabodi,

Assalaam alaykum.

Siku nyingi sijaandika hapa na hata kusoma, nimekuwa bize sana na majukum mbalimbali ya kusongesha mbele maisha.

Leo nimeamka nikajifikiria niwataarifu waTanzania wenzangu kuhusu utayari nilionao wa kupokea maoni, michango yenu na ushauri utakaoniwezesha kupata mwangaza wa ni nini niseme Bungeni wakati tukipitia Rasimu ya Katiba Mpya. Nitakuwa nikirudi hapa kusoma na kujadili mambo mbali mbali yatakayohusu issues zitakazokuwa zikijitokeza kwenye mjadala wa Katiba.

Ninawakaribisheni kwa mjadala constructive hapa.

Kama kuna mambo tunapaswa kuwa serious nayo kama Taifa basi ni hili la kuandika Katiba Mpya ya nchi yetu. Yale matatizo ya kimfumo tunayoyaongelea miaka na miaka sasa huu ndiyo muda wa kuyashughulikia, hakuna muda mwingine.

Wakatabahu,
HK.

Mkuu, hapo kwenye bold, are you serious!!?? Ina maana hujui atakwenda kusema nini na unataka JF wakupe mwangaza ...........!!??
 
Katiba hii mpya haijatambua haki ya afya (right to health) kama ilivyotambua haki zingine mfano Elimu. Tanzania imeridhia mikataba ya africa na ya kimataifa ambayo inaitambua haki ya afya kama haki ya msingi ya binadamu. Kutokuweka haki hii katika katiba mpya ni kwenda kinyume na mikataba hii ambayo nchi imeridhia/imesaini.

Mkataba wa afrika (banjul) kuhusu utu na haki za binadamu (1981)

Ibara ya 16 (kwa nchi wanachama): (1)Kila mtu atakuwa na haki ya kufurahia hali ya kuwa na afya ya kimwili na kiakili. (2) Kila nchi ina jukumu la kuchukua hatua za lazima za kulinda afya za wananchi wake na kuhakikisha kuwa wanapata matibabu pindi wanapokuwa wagonjwa. Tanzania imeridhia mkataba huu.

Katiba ya Tanzania (iliyopo):Haki zote zimefafanuliwa katika ibara ya 12 - 28. Haki ya afya haikutajwa moja kwa moja kama haki ya elimu na zingine zilivyotajwa.

Ibara 14. Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka katika jamii hifadhi ya maisha yake kwa mujibu wa sheria.

Ibara 11(1): Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu unaofaa kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa;
haki ya mtu kufanyakazi, haki ya kujipatia elimu na haki ya kupata msaada kutoka kwa jamii wakati wa uzee, maradhi au hali ya ulemavu, na katika hali nyinginezo za mtu kuwa hajiwezi.

Ibara ya tisa (9) ya katiba iliyopo sasa inasema; Lengo la katiba hii ni kuwezesha ujenzi wa Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar……….. …. kwa hiyo, mamlaka ya nchi na vyombo vyote vinawajibika kuelekeza sera zake zote katika lengo la kuhakikisha kwamba; (a) Utu na haki nyinginezo zote za binadamu zinaheshimiwa na kuthaminiwa. (f) Matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha umaskini, ujinga na maradhi.

Haki ya afya inatambuliwa na m ikataba ya kimataifa tuliyoiridhia. Ni muhimu tukaitambua haki hii na kwamba ni wajibu wa serikali kuhakikisha haki hii inapatikana kwa raia wake kama ibara hii ya tisa ya katiba ya sasa inavyosema.

Jukumu la dola ni kutoa huduma ipasavyo ili kufanikisha upatikanaji wa haki za msingi za watu wake ikiwemo haki ya afya.Kushindwa kuitambua ama kutoa huduma ikiwemo huduma ya afya ni uvunjaji wa haki za binadamu.

Mkataba wa Kimataifa kuhusu Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni (ICESCR - The international convenant for economical, social and cultural rights)ulisainiwa na nchi takribani 150 ikiwemo Tanzania. Unawataka waliotia saini kutoa huduma kwa dhana ya haki kwenye maeneo muhimu kwa kuzingatia rasilimali zilizopo. Baadhi ya haki zilizotajwa katika mkataba huu ni Afya, Elimu, Usalama kwa jamii, Kiwango cha maisha cha wastani (chakula, mavazi na malazi) na Kuendelea kuboresha hali ya maisha.

Mkuu Kingwalla, hakikisha unatetea haki ya afya kuingia katika katiba hii mpya!
 
Ninahitaji Serikali 3. Na kama vipi muungano wa Tanganyika na Zanzibar ufe. Kila nchi ichukue hamsini zake
 
Kwako HKigwangalla!
Maoni yangu ni haya: Nafasi za wakuu wa wilaya zifutwe, manake wamekaa kichamachama tu, katibu tawala wilaya anatosha kufanya kazi za wilaya akishirikiana na mkurugenzi, mawaziri wasiwe wabunge, serikali ya Tanganyika irudi, tunahitaji kujua mishahara ya viongozi wakuu wa serikali coz wanalipwa kutokana na kodi za wananchi. Posho zzenu wabunge zipunguzwe na zikatwe kodi kama ambavyo wengine tunalipa kodi. Mwisho nahitaji mtaji wa kuanzisha biashara so, ukinisaidia angalau posho yako ya siku 5 utakuwa umenisaidia sana (TSH 3,500,000).Mungu akubariki sana
 
Last edited by a moderator:
...ukomo ya kugombea ubunge iwe ni vipindi viwilii kama uraisi...

Na Mbunge asipofanya kwa "matakwa" ya wananchi basi aweze kupigiwa kura ya kutokuwa na imani ili aondoke hata kabla ya hiyo miaka mitano!!!!! Yaaaani afurushwe kama hafanyi kazi!!

Mawaziri wasiwe wabunge ili kupata serikali "strong" nje ya vyama vya siasa "moja kwa moja" ili ile executive power iwe independent na "party caucus"za adhoc kila mambo yanapoelekea upande wa wananchi!!!!!!
 
sina uhakika na nyie ukizingatia ni % 80 ya mliochaguliwa ni ccm

bac to topic
mi nasema wabunge viti maalumu vitolewe, vinamaliza pesa ya mlipa kodi, tunahitaji wabunge wa majimbo tu ht wanawake wakagombee full stop! !
pili, hivi kweli km mnathamini nchi na watz kweli mmekubali kulipwa hela yote hyo kwa cku? walati kuna watu wanafanya kazi kwa bidii hyo hela hawapati kwa mwezi! !

tatu, km kweli hamjali maslahi tunahitaji serikalo 3, yaani Tanganyika irudi.
 
mIMI NATAKA IITISHWE KURA YAN MAONI JUU YA MUUNGANO. hAYA MAMBO YENU YA KUTUCHAGULIA AINA YA MUUNGANO TUMEYACHOKA
 
Kuna hii kitu inaitwa wawekezaji ambao si Watanzania na hawana uchungu na kuimarika kwa uchumi wa Tanzania zaidi ya kutafuta faida. Halafu kuna hii kitu inaitwa makampuni ya ukaguzi wa mahesabu ya kimataifa, mtamzamo hati ya ukaguzi (audit opinion) kwa makampuni ambayo zaidi 50% yanamilikiwa na wageni katiba isiruhusu hiyo hati kusaini na wakaguzi ambao si Watanzania.
 
[h=2]Mkuu.

Naomba wajumbe wa Bunge hilo pamoja na mambo mengine msisitize umuhimu wa lugha ya kiswahili kwa mustakabali wa taifa letu. Mnaweza kuendelea kupigia chapua matumizi ya lugha ya kiingereza kwa kadri mnavyoona inafaaa, lakini kiswahili kwanza mengine yafuate.

Ukifuatilia maandishi mengi katika mitandao ya kijamii, utabaini kuwa watanzania wana matatizo makubwa juu ya uelewa wao wa lugha hii kutokana na kukosekanha kwa misingi ya kuisimamia ipasavyo.

Katiba itamke kuwa kiswahili ndio lugha rasmi katika shughuli zote kiserikali na kupiga marufuku kuchanganya lugha iwe katika mazungumzo au maandishi.

Kigwangala, hata katika andiko lako hili linaonyesha kwa kiwango gani ambavyo tunatakiwa makini kwa kuweka katika katiba yetu msisitizo juu ya kiswahili.

Kwa kufanya hivyo , serikali itawajibika kuelekeza raslimali za kutosha kuwezesha kiswahili kinafundishwa na kutumika katika shughuli zote za serikali hali ambayo itawavutia watu wengi kupenda kukitumia inavyostahili.

Masuala mengine kama ya kuchanganya lugha sio lazima yawekwe ndani ya katiba, isipokuwa tunaweza kutunga kanuni kiatika taasisi zte kama inavyofanyika kwenye bunge la Kenya ambako mzungumzaji atatakiwa kuendelea kutumia lugha ambayo wakati anaanza kuchangia aliitumia. Ukianza kiswahili utaendelea kwa kiswahili.
Asante[/h]
 
Hivi huu ni wakati kweli wa kupokea maoni? Tume ya warioba imefanya nini? Kama mpaka wakati huu rais amekuteua kwenda kupitia/ kujadilidi maoni ya wananchi kwa namna ya kuboresha halafu wewe unataka maoni tena kutoka kwetu..., haishangazi sana kuwa sisi tumebaki kuwa taifa la hovyo sana.
Kuna kila dalili kuwa hatutapata katiba mpya tuliyoitaka wananchi. Kumbuka hata raisi ameshawaambia kuwa mnaweza kubadili kabisa maoni yetu mkitaka (na mmeshaonyesha dalili hizo).
Nendeni Dodoma mkafanye kile chama chenu kinachowataka mkifanye...nendeni. Sisi tumekwisha malizana na Warioba. Historia itawahukumu kwa haki. Nendeni, msituchoshe!
Kwa utawala uliopo sasa ni lazima katiba itakayopatikana ifanane nao. Kwa hiyo tegemea katiba ya kijanjajanja na isiyo na maamuzi.

 
Katiba itamke wazi kuwa Tume ya uchaguzi iwe taasisi huru isiyoingiliwa uhuru wake kisiasa.
Jeshi la polisi liwe taasisi huru bila kuingiliwa kisiasa
Mahakama iwe mhimili unaojitegemea usioingiliwa na siasa


nitakuja baadaye.
 
Hivi huu ni wakati kweli wa kupokea maoni? Tume ya warioba imefanya nini? Kama mpaka wakati huu rais amekuteua kwenda kupitia/ kujadilidi maoni ya wananchi kwa namna ya kuboresha halafu wewe unataka maoni tena kutoka kwetu..., haishangazi sana kuwa sisi tumebaki kuwa taifa la hovyo sana.
Kuna kila dalili kuwa hatutapata katiba mpya tuliyoitaka wananchi. Kumbuka hata raisi ameshawaambia kuwa mnaweza kubadili kabisa maoni yetu mkitaka (na mmeshaonyesha dalili hizo).
Nendeni Dodoma mkafanye kile chama chenu kinachowataka mkifanye...nendeni. Sisi tumekwisha malizana na Warioba. Historia itawahukumu kwa haki. Nendeni, msituchoshe!

yaaa waende tu hata wakisema ndiyooooooooooooo sawa tu, wagonge meza wao tu, lakini wakumbuke iko siku Mungu atawaleta hukumuni.
 
1. Serikali 3, au la kila nchi iende kivyake. (tutakutana EAC, kama bado itakuwepo!)

2.Kila raia wa Tanzania alipe kodi with no exception!!! (rais, wanasiasa wote inclusive)!!

3. Kundi la watu wasiwe na mamlaka ya kubadilisha au kutunga sheria itakayowanufaisha wao wakati wakiwa madarakani, sheria kama hiyo ikitungwa iwanufaishe watakaoingia madarakani baada ya walioitunga kumaliza kipindi chao.
- hii itaondoa uroho wa wanasiasa kujiongezea mafao kila kukicha!


Nitarudi tena!
 
Wee CCM uache kutuzuga, hautoweza kupingana na serikali mbili kama chama chako kinavyotaka! Na vile hauwezi kupingana na laki 7 kwa kazi ya kusema ndio, hapana na kusinzia!
...
Usichezee akili zetu, kama mpaka leo haujui huko ukaongee nini, katetetee sera za chama chako!
Si ndivyo miccm mlivyo, badala ya kutetea wananchi eti mnatetea chama!
Kwendaaaaaaaaaaaaa!
 
1. Ubunge wa viti maalum ukome mara moja kwani ni mzigo kwa walipa kodi

2. Wagombea binafsi katika chaguzi zote kuanzia ujumbe wa nyumba 10 hadi rais waruhusiwe. Kuna wengi tu hatuna itikadi ya vyama

3. Waziri asiwe mbunge. Akishateuliwa na rais jina lake lipelekwe bungeni kwaajili ya grilling na background check. Hii pia ifanyike kwa deputy ministers, Principal secs, Heads of state-owned corporations, agencies etc.

4. Vyeo vya Ukuu wa wilaya na mkoa vifutwe. Tuwe na counties tu na kila county wananchi wachague county commissioners wao na sio wabambikiwe na rais.

5. Idadi ya wizara ipunguzwe. Wizara kama michezo, utamaduni, Africa mashariki, Tawala bora, nk. zifutiliwe mbali kwani ni mzigo tu kwa walipa kodi

6. Ruzuku kwa vyama vyote vya siasa ifutwe.

7. Mishahara ya rais, PM, VC, County commissioners, MPs iwekwe wazi na ikatwe kodi.

8. Rais aondolewe immunity esp. akiondoka madarakani. Mtanzania yoyote awe na uwezo wa kumfungulia mashtaka rais

9. Baada ya cheo cha rais tuwe na aidha VP or PM lakini sio both. Kimojawapo kati ya VP ao PM kifutwe

10. Tume ya uchaguzi iwe tume huru. Rais asituchagulie mwenyekiti wa tume

11. Rais apendekeze majaji, majina yao yapelekwe bungeni kwaajili ya grilling na background check na upitishaji

Mengineyo yatafuata
 
Back
Top Bottom