Katiba Mpya: Nitakuwa Tayari Kupokea Maoni Yako Kuanzia Leo!

Tatizo wengi wetu humu ndani JF hatukuamini kwa kuwa umekuwa MNAFIKI na MSALITI sana.
Hata maoni ya madaktari wakati wa migomo yao 2012 ulitumwa na Bunge kwenda kuyakusanya lakini ulichokwenda Kukiwalisha bungeni ni mashudu yako matupu na sio uhalisia.

Dr.Kigwangwalla wewe bado sana, unajaribu kufanya mambo kama Mwigulu Nchemba ili kudraw attention za watu tu lakini huna dhamira yoyote njema.

Kwa kuanzia tu, embu tupe msimamo wako ni upi kwenye bunge la Katiba na nini utafanya katika haya:
1/Mfumo wa serikali (Utafuata sera ya CCM serikali mbili au Msimamo wa Warioba na watanzania wengi(61%) serikali tatu au vinginevyo).

2/Posho ya shilingi 700000/= kwa siku kwa kila mjumbe wa bunge la katiba kwa siku 70.
Ndg nani sijui vile,
Naomba nianze kwa kukushangaa kwa hoja mfu uliyotoa.

1. kuhusu madaktari ni uongo, huna uhakika na unachoongea.

2. Mimi huwa siigi mtu anafanya ama anasimamia nini, hivyo kunifananisha na Mhe. Mwigulu si sahihi sana

3. Misimamo yangu.... kwa kuwa umeweka taarifa za uongo, siwezi kutoa msimamo. Tafuta ukweli kwanza ndiyo useme neno. Hakuna kitu kama posho ya laki saba, sera ya serikali 2 ama tatu, nitazungumza na waandishi wa habari kesho kuhusu hili.

wakatabahu,
HK.

1.
 
1. Ubunge wa viti maalum ukome mara moja kwani ni mzigo kwa walipa kodi

2. Wagombea binafsi katika chaguzi zote kuanzia ujumbe wa nyumba 10 hadi rais waruhusiwe. Kuna wengi tu hatuna itikadi ya vyama

3. Waziri asiwe mbunge. Akishateuliwa na rais jina lake lipelekwe bungeni kwaajili ya grilling na background check. Hii pia ifanyike kwa deputy ministers, Principal secs, Heads of state-owned corporations, agencies etc.

4. Vyeo vya Ukuu wa wilaya na mkoa vifutwe. Tuwe na counties tu na kila county wananchi wachague county commissioners wao na sio wabambikiwe na rais.

5. Idadi ya wizara ipunguzwe. Wizara kama michezo, utamaduni, Africa mashariki, Tawala bora, nk. zifutiliwe mbali kwani ni mzigo tu kwa walipa kodi

6. Ruzuku kwa vyama vyote vya siasa ifutwe.

7. Mishahara ya rais, PM, VC, County commissioners, MPs iwekwe wazi na ikatwe kodi.

8. Rais aondolewe immunity esp. akiondoka madarakani. Mtanzania yoyote awe na uwezo wa kumfungulia mashtaka rais

9. Baada ya cheo cha rais tuwe na aidha VP or PM lakini sio both. Kimojawapo kati ya VP ao PM kifutwe

10. Tume ya uchaguzi iwe tume huru. Rais asituchagulie mwenyekiti wa tume

11. Rais apendekeze majaji, majina yao yapelekwe bungeni kwaajili ya grilling na background check na upitishaji

Mengineyo yatafuata

Al umegusa mengi niliyokuwa nafikiria, ila nitaongezea machache kama ifuatavyo

12: Muundo wa serikali uwe katika katiba, yaani wizara za serikali ziwe ndani ya katiba ili raisi asijiundie baraza la mawaziri 100 ili kukidhi mahitaji ya marafiki zake.

13: Sifa pekee ya kuwania uraisi wa nchi iwe ni uraia wake: awe ni mtanzania aliyezaliwa Tanzania na wazazi ambao pia walizaliwa Tanzania. Elimu, umri na jinsia visiwe vigezo; vitu hivyo ama vitumike dhidi yake au kwa manufaa yake katika kampeini lakini visiwe vigezo vya kikatiba. Umri pekee unaotakiwa ni ule wa utu uzima yaani miaka 18.

14: Wateule wote wa Rais, majaji, mawaziri na mabalzoi wathibitishwe na bunge.

15: Kuwepo na tume huru ya utumishi wa umma ambayo haiingiliani na serikali. Watumishi wataalamu wote wa serikali wanakuwa chini ya tume hiyo na hawatachukua amri kutoka kwa wanasiasa.

16: Nafasi zote za kitaalamu serikalini ziwe za kuomba siyo za kuteuliwa au kupendekezwa. Kwa hiyo makatiibu wakuu, wakurugenzi na makamishna mbalimbali pamoja na wakuu wa vitengo mbalimbali wizarani waombe kazi hizo siyo wateuliwe na waziri au rais. Maombi yao yawe screened na tume ya taifa ya utumishi serikalini niliyotaja hapo juu.

17: Rais asiwe na mamlaka ya kumfukuza mtu yeyote wakati wowote hata kama ni mteule wake wa kisiasa, lazime kuwepo na due process.

.....
 
Ndugu wanabodi,

Assalaam alaykum.

Siku nyingi sijaandika hapa na hata kusoma, nimekuwa bize sana na majukum mbalimbali ya kusongesha mbele maisha.

Leo nimeamka nikajifikiria niwataarifu waTanzania wenzangu kuhusu utayari nilionao wa kupokea maoni, michango yenu na ushauri utakaoniwezesha kupata mwangaza wa ni nini niseme Bungeni wakati tukipitia Rasimu ya Katiba Mpya. Nitakuwa nikirudi hapa kusoma na kujadili mambo mbali mbali yatakayohusu issues zitakazokuwa zikijitokeza kwenye mjadala wa Katiba.

Ninawakaribisheni kwa mjadala constructive hapa.

Kama kuna mambo tunapaswa kuwa serious nayo kama Taifa basi ni hili la kuandika Katiba Mpya ya nchi yetu. Yale matatizo ya kimfumo tunayoyaongelea miaka na miaka sasa huu ndiyo muda wa kuyashughulikia, hakuna muda mwingine.

Wakatabahu,
HK.

Mi naomba hoja ya kiswahili kutumika kama lugha ya Taifa litazamwe vizuri na ikibidi libadilishwe. Katika Mazingira ya sasa siamini kuwa lugha ya kiswahili ina nafasi ya kutuvusha kutoka hapa tulipo kimaendeleo kwenda tunakotaka.Tuachane na Utaifa na Pride isiyokuwa ya msingi na tuseme kwa pamoja kwamba kiswahili kitaendelea kubaki kama lugha yetu mama inayotuunganisha wote lakini haiwezi kuwa official language kinaturudisha nyuma kwa sababu zifuatazo:

i)Watoto wa walalahoi kuwa victims: Wakati wanasiasa wanapitisha kiswahili kuwa lugha rasmi watoto wao wanawasomesha international schools na nje ya nchi, Ulaya na Marekani.Wakirudi kwenye soko la ajira mtoto wa mlala hoi hana nafasi,siku zote atakuwa chini sababu hawezi kuongea kingereza, chukulia mfano kazi za EAC community, AU, UN, Makampuni ya kigeni nk

ii)Kutengeneza makundi katika jamii; kama nilivyosema hapo juu, kundi la watoto wa makabwela waliosomea shule za kizalendo wasioweza kuimudu lugha ya Kiingereza who are looked down upon in the employment market vs watoto wa vigogo na matajiri waliosomeshwa nje ya nchi/English medium schools wanaoimudu kiingereza, hivyo wanaofikiriwa kwanza katika soko la ajira, wenye confidence, exposure

iii)Matumizi mabaya ya rasilimali:Nasema ni matumizi mabaya ya rasimilimali kufikiria kubadilisha mfumo kuwa wa kiswahili, mfumo ambao umetushinda kubadilisha tokea miaka 50 tulipopata uhuru ni kujidangaya kufikria kuwa tutaubadilisha leo.Kwa maana nyingine ni kutanguliza uzalendo upofu(blind patriotism) au Utaifa upofu(blind nationalism) Usiokuwa wa msingi.Hii tulitakiwa tufanye na tufanikishe right after independence kama walivyofanya nchi za asia, china,korea, japan nk lakini sio sasa.Huu ni muda wa kufocus on global integration so as to match the technological pace the world is today.We need to abandon Swahili very quick and fast in order to focus on English as a national language and medium of communication.That is the only way we can match up the pace, kiswahili is a big backwardness towards those goals.

iv)Low Self esteem problem:Ni ukweli usiopingika kuwa kutokumudu kiingereza vizuri kinachangia sana katika hili sana sana katika soko la ajira la dunia.Tumeona jinsi ambavyo watanzania wanapewa second priority kwenye makampuni ya kigeni kulinganisha na wakenya, waganda, wagana nk. Simaanishi kuwa hakuna wataanzania wanaobahatika kupata ajira nzuri katika makampuni ya kigheni lakini ni wachache na kikwazo kikubwa ni very low self esteem we posses due to our inability to express our-self well in English.Let's say enough with politics and pride,let's be realistic. English is the solution!!...Kusisitiza matumizi ya kiswahilili wakati watoto wao wanasoma ulaya na marekani ni ufisadi mwingine wa kimfumo.Be ware!!
 
Mimi nakushauri tu wewe na wengine wa CCM,katiba ni ya Watanzania si wanasiasa!watanzania tulishatoa maoni na 61% kwa mujib wa Tume tunaitaji serikali tatu!neno serikali mbili kama CCM wanalipenda basi liandikwe katika Katiba ya CCM sio katika katiba Nchi!naamin kila chama kilikua na maoni na sisi wananchi pia ila sio yote yameandikwa
 
Tatzo wewe mahaba ya ccm yamekujaa

sisi wananch tumependekeza serkali tatu

mkienda bungen mnfanya kaz ya kuwasalit wananchi
tena kwa kutumia vigezo vya uongo

subir waje wtt wa lumumba mtaelewana labda
 
Ndugu wanabodi,

Assalaam alaykum.

Siku nyingi sijaandika hapa na hata kusoma, nimekuwa bize sana na majukum mbalimbali ya kusongesha mbele maisha.

Leo nimeamka nikajifikiria niwataarifu waTanzania wenzangu kuhusu utayari nilionao wa kupokea maoni, michango yenu na ushauri utakaoniwezesha kupata mwangaza wa ni nini niseme Bungeni wakati tukipitia Rasimu ya Katiba Mpya. Nitakuwa nikirudi hapa kusoma na kujadili mambo mbali mbali yatakayohusu issues zitakazokuwa zikijitokeza kwenye mjadala wa Katiba.

Ninawakaribisheni kwa mjadala constructive hapa.

Kama kuna mambo tunapaswa kuwa serious nayo kama Taifa basi ni hili la kuandika Katiba Mpya ya nchi yetu. Yale matatizo ya kimfumo tunayoyaongelea miaka na miaka sasa huu ndiyo muda wa kuyashughulikia, hakuna muda mwingine.

Wakatabahu,
HK.

Hivi nyie mlio kwenye bunge la katiba mnalipwa shilingi ngapi kwa siku? Je unadhani hicho kiwango sio UFISADI? Mchango wangu ni kwamba anzeni na posho zenu kuzijadili maana hizi posho zenu ni dalili ya UFISADI!!
 
jamani huu muda siyo wa kurumbana na kumtafuta mchawi wa katiba mpya, cha msingi, wazo analolitoa mtu kama lina manufaa kwa maendeleo ya Taifa letu basi tulipitishe na tuangalie matokeo yake,katiba ni yetu sote yaani watanzania wote.
 
Mawaziri wasitoke bungeni, wawe wanaomba kazi kama wafanyakazi wengine na wanafanyiwa udahili na uhakiki na bunge, na kazi na majukumu yao yaainishwe rasmi. Na wataingia bungeni kama mawaziri na si wabunge.

Wakuu wa mikoa wachaguliwe na wananchi kwa kura za kila mkoa, na mkuu wa mkoa ni lazima awe kaishi kwenye huo mkoa kwa muda usiopungua miaka 5. Na kazi na majukumu yao yaainishwe rasmi.

Wakuu wa wilaya wachaguliwe na wananchi, na mkuu wa wilaya ni lazima awe kaishi kwenye huo mkoa kwa muda usiopungua miaka 5. Na kazi na majukumu yao yaainishwe rasmi.
 
Rais asiwekewe kikomo cha miaka 10, aweze kugombea awamu 4 na akichaguliwa zote maximum kufanya kazi ya Urais iwe miaka 20. Na Rais aweze kugombea hata akiangushwa awamu hii awamu ijayo ruksa kugombea mradi awe hajafanya kazi ya Urais zaidi ya Miaka 20.

Miaka ya kugombea Urais ishushwe hadi kufikia 28, tupate Marais vijana.

Umri wa mwisho wa kugombea Urais uwe ni miaka 61.
 
Mimi nakushauri kama mjumbe wa bunge la kutengeneza katiba ya watanzania, jitahidi sana kuwashauri wana ccm kutoweka maslahi ya chama mbele, bali wayaweke maslahi ya taifa kwanza. Chama baadaye. Hii ni kwasababu katiba inayokwenda kutengenezwa Bungeni ni katiba ya vizazi vijavyo na hasa wakiwepo na watoto wako. sijui kama bunge hilo lisipoangalia maslahi ya taifa watakimbilia nchi gani? ok, yawezekana watatorokea nje ya nchi, lakini Taifa kama Taifa watadaiwa popote waendapo. Toa maoni ya Watamzania na siyo ya ccm, na nini watanzania wanataka hasa kiwekwe kwenye katiba. ya kwanu leo ya wewe kuipeleka bungeni ni kwamba naungana na Watanganika wenzangu kudai Jamhuri ya Watanganyika kama walivyo Wanzanzibari.
nakutakia uwakilishi mwema kada!
 
simamia serikali 3, zanzibar na tanganyika ziwe na mawaziri wakuu watakao kuwa wenye mamlaka na kusimamia serikali , mawaziri hao wawe ni wajumbe wabaraza la jamhuri yamuungano wasio na kura. pia katiba ipitishe tume huru ya uchaguzi na ndiyo itakayosimamia kuboresha daftari la wapiga kura kila uchaguzi unapoitishwa
 
(18) Kikomo cha urais kibaki miaka 10 lakini pia kuwe na kikomo cha ubunge kuwa miaka 15.

(19) Adhabu ya kifo iwekwe rasmi katika Katiba kama adhabu pekee kwa makosa mawili ya kudhamiria: Kosa la kuua kwa kudhamiria, na kosa la kuubia umma wa watanzania kwa kudhamiria.

(20) ...
 
Katiba ipunguze kinga ya polisi raia awe na haki ya kuwashitaki polisi kama ataona hakutendewa haki kama kesi haikupelekwa mahakamani. Uteuzi wowote utakaofanywa na rais sharti uidhinishwe na bunge kuepuka kuteua watu wasiokuwa na sifa kwa kigezo cha kujuana. Safari za rais nje ya nchi zidhibitiwe kuepuka matumizi ovyo ya kodi zetu. Katiba itamke wazi kupiga marufuku ya matumizi ya vyombo vya kifahari kama magari kwa matumizi ya shughuli za serikali. Napendekeza muungano wa kweli yaani serikali moja kama hiyo haiwezekani basi tutengane mazima.
 
Back
Top Bottom