Katiba Mpya: Nitakuwa Tayari Kupokea Maoni Yako Kuanzia Leo!

Mawaziri wasitoke bungeni, wawe wanaomba kazi kama wafanyakazi wengine na wanafanyiwa udahili na uhakiki na bunge, na kazi na majukumu yao yaainishwe rasmi. Na wataingia bungeni kama mawaziri na si wabunge.

Wakuu wa mikoa wachaguliwe na wananchi kwa kura za kila mkoa, na mkuu wa mkoa ni lazima awe kaishi kwenye huo mkoa kwa muda usiopungua miaka 5. Na kazi na majukumu yao yaainishwe rasmi.

Wakuu wa wilaya wachaguliwe na wananchi, na mkuu wa wilaya ni lazima awe kaishi kwenye huo mkoa kwa muda usiopungua miaka 5. Na kazi na majukumu yao yaainishwe rasmi.

He! Kumbe na wewe hua unaweza kutoa Michango ya Kujenga namna hii.Sasa Mbona Wakati Mwingine unavaa Miwani ya Mbao yani Huwezi kuona vile!!!
 
Rais asiwekewe kikomo cha miaka 10, aweze kugombea awamu 4 na akichaguliwa zote maximum kufanya kazi ya Urais iwe miaka 20. Na Rais aweze kugombea hata akiangushwa awamu hii awamu ijayo ruksa kugombea mradi awe hajafanya kazi ya Urais zaidi ya Miaka 20.

Miaka ya kugombea Urais ishushwe hadi kufikia 28, tupate Marais vijana.

Umri wa mwisho wa kugombea Urais uwe ni miaka 61.

Mhhhhhh! makubwa tena!
 
1. Ubunge wa viti maalum ukome mara moja kwani ni mzigo kwa walipa kodi

2. Wagombea binafsi katika chaguzi zote kuanzia ujumbe wa nyumba 10 hadi rais waruhusiwe. Kuna wengi tu hatuna itikadi ya vyama

3. Waziri asiwe mbunge. Akishateuliwa na rais jina lake lipelekwe bungeni kwaajili ya grilling na background check. Hii pia ifanyike kwa deputy ministers, Principal secs, Heads of state-owned corporations, agencies etc.

4. Vyeo vya Ukuu wa wilaya na mkoa vifutwe. Tuwe na counties tu na kila county wananchi wachague county commissioners wao na sio wabambikiwe na rais.

5. Idadi ya wizara ipunguzwe. Wizara kama michezo, utamaduni, Africa mashariki, Tawala bora, nk. zifutiliwe mbali kwani ni mzigo tu kwa walipa kodi

6. Ruzuku kwa vyama vyote vya siasa ifutwe.

7. Mishahara ya rais, PM, VC, County commissioners, MPs iwekwe wazi na ikatwe kodi.

8. Rais aondolewe immunity esp. akiondoka madarakani. Mtanzania yoyote awe na uwezo wa kumfungulia mashtaka rais

9. Baada ya cheo cha rais tuwe na aidha VP or PM lakini sio both. Kimojawapo kati ya VP ao PM kifutwe

10. Tume ya uchaguzi iwe tume huru. Rais asituchagulie mwenyekiti wa tume

11. Rais apendekeze majaji, majina yao yapelekwe bungeni kwaajili ya grilling na background check na upitishaji

Mengineyo yatafuata

Naunga Mkono Hoja za Mjumbe isipokua hoja no. 5 Inahitaji Marekebisho.Hasa kufuta Wizara ya Michezo na Utamaduni!
 
Hongera sana mhe. Daktari kweli wewe ni muwakilishi wa wananchi. Mawazo yangu ni haya;
1. Mahakama, Huu ni muhili ambao unahitaji ujadiliwe kwa kina sana ili uweze kufanya kazi zake kwa uhuru bila woga, na hili litawezekana tu endapo nafasi ya Jaji mkuu itakuwa ni nafasi ya kuchaguliwa, Kama ilivyo kwa spika wa bunge anachaguliwa na wabunge kisha jina lake lina thibitishwa na rais. Jaji mkuu achaguliwa na wanamahakama wenyewe Kisha jina lake lithibitishwe na rais, maslahi ya mahakimu pia yatambuliwe ndani ya katiba kima ilivyo kwa majaji,hii itasaidia sana ktk kupunguza suala la rushwa, pia lugha rasmi ya mahakam pamoja na uwelaji wa kumbukumbu za mahakama ziwekwe kwa lugha ya kiswa, Hii itasaidia wananchi walio wengi kufahamu kwa wepesi jinsi ya kupata haki zao na pia kuelewa jinsi ilivyo tolewa.ni kwamahakama zote.
2. Ukomo wa majaji uwe miaka 50, hii itasaidia sana.
3.Tume ya mahakama kiwe chombo cha kujitegemea M.kiti wake afanye application asiteuliwe

4.
 
Nawashangaa waTanganyika hakuna anaesema hataki muungano .,., yupo ataeweza kutoka jibu ???
 
Ndg nani sijui vile,
Naomba nianze kwa kukushangaa kwa hoja mfu uliyotoa.

1. kuhusu madaktari ni uongo, huna uhakika na unachoongea.

2. Mimi huwa siigi mtu anafanya ama anasimamia nini, hivyo kunifananisha na Mhe. Mwigulu si sahihi sana

3. Misimamo yangu.... kwa kuwa umeweka taarifa za uongo, siwezi kutoa msimamo. Tafuta ukweli kwanza ndiyo useme neno. Hakuna kitu kama posho ya laki saba, sera ya serikali 2 ama tatu, nitazungumza na waandishi wa habari kesho kuhusu hili.

wakatabahu,
HK.

1.

Kwa nini usitaje hapa msimamo wako juu ya Muundo wa Muungano. Hao waandishi wa habari wa nini? By the way, kwa maoni ya wengi waliochangia humu, wengi wanataka serikali3, hivyo tunakuomba ukawaambie waheshimiwa wa Chama, kuwa kwa upepo ulivyo serikali mbili hazikubaliki tena, na kwamba wale wanaoitwa Watanzania Bara, wanaitka Tanganyika yao Huru. Kwa kuwa serikali 2 hazikubaliki, basi mwendo ni wa serikali1, ikishindikana basi ni serikali3.
 
Dhana ya muundo wa serikali ni dhana ya kisiasa tu.........kuna mengi ya kujikita kwayo
 
Baraza la sanaa la taifa linatosha kusimamia mambo ya Utamaduni

Laiti kama Vingozi wetu wangekua sikivu wakaendesha Nchi kwa Mawazo na Michango ya Watu,wataalamu na Wadau mbalimbali.Tanzania ya sasa ingekua mbali sana.Ila wao wakilala wakiamka bila ata kushirikisha wataalamu utasikia "tunaanzisha Physics with Chemistry,Div 5,Vipindi vya bunge havitarushwa hewani kulinda Heshima ya Bunge,Tunaanzisha Digitali na asiyetaka na aache kuangalia TV,e.t.c.... to mention but few...This is very shameful!
 
Nimefuatilia maoni yako nimeridhika isipokuwa sijapata maoni yako juu ya separation of powers na tume huru ya uchaguzi iweje
 
Though watch out with what we re getting from various sources about prep of political party of pushing out there agenda which it seems to be very contrally to what warioba presented which we believe its peolpes wish and ideas and allot of resources wasted who to be blamed if are to be sidelined
 
1. Mtanganyika + CCM = mtetezi wa Tanzania (No matter what Znz is doing)
2. Mzanzibar + CCM = mtetezi wa Zanzibar
3. Mzanzibar + CUF = mtetezi wa Zanzibar
Sub-total = 80%
Who will stand for Tanganyika?
 
Mheshimiwa ulikuwa wapi wakati sheria ya marekebisho ya katiba inapitishwa bungeni? Sheria hiyo inasema tume ya sasa ya uchaguzi ndiyo itaendesha kura ya maoni; rasimu ya katiba inasema iundwe tume HURU ya uchaguzi; ina maana ya sasa siyo huru yaani iondolewe, Je unafikiri tume ya sasa ya uchaguzi itaweza kusema kuwa wananchi wametaka iondolewe wakati yenyewe ndiyo inasimamia kura hiyo? Hakuna mtu anayeweza kujipiga nyundo mwenyewe, labda mwendawazimu tu. Kwa hiyo basi, maoni yote tutakayokupa hayatasaidia chochote, hasa pale yatakapopingana na hao waliounda tume hiyo. Nadhani umenielewa. Kesho nitakupa maoni yangu kwa matumaini kuwa ukiingia bungeni utatoa hoja ya kutaka kipengele hicho cha sheria ya katiba kibadirishwe na majukumu hayo yarudishwe kwa tume ya Warioba kama ilivyokuwa kwenye sheria ya mwanzo kabisa.
 
Back
Top Bottom