Katiba mpya ipendekeze Raisi na Makamu wote wotekee Bara

themagnificient

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
988
3,318
Naskia kulikuwa na hatakati za Kuanzishwa kwa katiba mpya basi pendekezo langu ni hili

Kwa mustakabali wa maendeleo yetu na kulinda Rasilimali zetu ni lazma Katiba mpya iweke Sheria kuwa Raisi na makamu wake wote watokeee Bara, ni jambo la kushangaza Zanzibar tokea tuungane nao Maraisi wao wote hadi makam wanatoka Zanzibar yaani Asali ya Uongozi kwao ni Yao huku Bara tunagawana wao hata wabunge huwezi kuta mbunge au waziri ni mzawa wa Mwanza au Moshi wao Ajira hadi uongozi ni mali yao huku bara tunagawana hili halipo sawa

Mfano mwingine ni Namna Raisi Samia alivyoridhia kuingia mkataba wenye Utata na Waarabu yeye na Waziri Mbarawa mkataba ambao umepigiwa kelele na Nchi nzima kuwa una utata na unaweza kuja kuliingiza Taifa kwenye Hasara kubwa na cha kushangaza Wameingia mkataba kwa Bandari za Bara tu ila Bandari ya Zanzibar haijahusishwa

Yaani maana yake ni kuwa Raisi samia ameonyesha kuwa ana uchungu sana na uchumi Wa huku Bara ila Zanzibar hana?

Makataba umechukua vipi Bandari za Dar ukaacha Bandari za Zanzibar?
 
Kwa mustakabali wa maendeleo yetu na kulinda Rasilimali zetu ni lazma Katiba mpya iweke Sheria kuwa Raisi na makamu wake wote watokeee Bara
... hilo halina tofauti na kuvunja muungano wa serikali mbili maana kiungo mojawapo cha mfumo huu wa muungano (wa CCM) ni uongozi wa juu wa nchi. Hati za Muungano zinasema, endapo rais akitokea upande mmoja wa muungano, makamu wake atoke upande wa pili.

The best model ya muungano ni ama serikali moja au tatu; serikali mbili (muundo wa sasa wa muungano wa CCM), ni ndoto za alinacha zisizotekelezeka.
 
Back
Top Bottom