Katiba Mpya haitakuja kwa Maneno Matupu

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,924
35,930
Kupata katiba mpya ni shughuli pevu dhidi ya walamba asali, vibaraka na chawa wao. Vipi kuwatemesha matonge midomoni?

Katiba mpya haitakuja kwa maneno Matupu mezani au mitandaoni.

Katiba mpya itakuja kwa mapambano yaliyoratibiwa vyema chini ya mikakati thabiti.

Kuganga yaliyopo na yajayo katika maana halisi kutatufikisha kunako katiba mpya.

Shuruti tutoke kokote tulipo tukutane Tahrir.

Shime waungwana katiba mpya haiwezi kuwa zao la wajinga wala waoga.

"Shikamoo Prof. Lwaitama, mshirika wa dhati katika mapambano."

Kwa hakika hauko peke yako.
 
Katiba Mpya inaratibiwa na wenye nchi hao ndio waliamua kikwete aanzishe mchakato ule!!

Sio takwa la CCM CHADEMA wala Mbowe ni la wenye NCHI! WENGINE ni chambo TU!!

Tozo na kauli za Mwigulu Ndio chambo cha katiba Mpya kupatikana!

Hakuna haja ya harakati wala vurugu katiba ipo njiani !!!

Tofauti ya kenya na huku ni kuwa mambo yanaratibiwa VIZURI na wenye ambao hata chama tawala wanawajibika kwao!

Tusubiri
 
Wenye nchi ni sisi. Uliowataja hapo ni ile timu pendwa ya walamba asali. Hao hawawezi kutupa sisi wenye nchi katiba tunayoitaka.

NInakazia:

"Shime waungwana katiba mpya haiwezi kuwa zao la wajinga wala waoga."
 
Nionavyo sasa hivi, ni kama vile vyama vya upinzani vimeiachia CCM iwaletee Katiba Mpya baada ya Kamati Kuu ya CCM kusema itaanzisha mchakato wake.

Wametulia wanasubiri Katiba Pendekezwa iletwe mezani, halafu ikishakuja washtuke usingizini waanze tena kupiga kelele za kuipinga, na hapa itakuwa too late kwasababu naamini 2024 ya uchaguzi wa SM itakuwa imekaribia kuelekea 2025.
 
Nionavyo kuna woga (playing safe) na kutegeana kukwepa gharama Ili kuja kujilia matunda kiulaini bila jasho.

Kwa hakika haya ndiyo yale ya ujinga sasa wayasemayo FAM na Jenerali ulimwengu:

IMG_20220914_180443_804.jpg

Woga (playing safe) na kutegeana yaone hata katika nyuzi bayana kama hizi uone tunavyopita juu kwa juu.

Niliwahi kuandika nyuzi kadhaa:

Upinzani - walio waoga (cowards) si Wafuasi

Muda wa mapinduzi vyamani ni sasa

Tusilaumiane: Wako wapi kina Nyerere, Maalim Seif, Mtikila, Julius Malema au kina Tutu

Ikumbukwe ukombozi ni wito kwa wachache waliochaguliwa na mola. Haiwezi kuwa kwa kila mtu na hasa kila mburula.
 
Huu ndio ukweli , Bila gharama za kutisha ccm haitokubali Katiba Mpya wala Tume Huru , kuna haja kubwa sana ya kulipia gharama hizi .

Jukumu takatifu (noble duty) hili haliwezi kuwa la kila aitwaye binadamu, hata mburula tu?

Ni muhimu kufahamu ma opportunists wapo na wataendelea kuwapo.

Tusikatishwe tamaa na wajinga.

Penye nia pana njia.
 
Nionavyo sasa hivi, ni kama vile vyama vya upinzani vimeiachia CCM iwaletee Katiba Mpya baada ya Kamati Kuu ya CCM kusema itaanzisha mchakato wake.

Wametulia wanasubiri Katiba Pendekezwa iletwe mezani, halafu ikishakuja washtuke usingizini waanze tena kupiga kelele za kuipinga, na hapa itakuwa too late kwasababu naamini 2024 ya uchaguzi wa SM itakuwa imekaribia kuelekea 2025.
Mkuu

TUSUBIRI

Muda wa kuipata umekaribia ni ile Rasimu lakini zitabaki mbili na sio TATU!

Ccm inafuata maelekezo KUHUSU hiyo katiba na upinzani TAYARI wameshamaliza KAZI yao!

Takwa la katiba ni la wananchi wenye nchi hakuna haja ya mvutano!

Tanzania ni Taifa teule halimwagi damu KWA ajili ya mageuzi bali maridhiano nadhani yameshapatikana na kitabu kitapatikana!!

Kumbuka hakukuwa na mgogoro wowote wakati tume ya Warioba inakusanya maoni na Sasa itakuwa shwari tutaipata bila mizengwe!ile mivutano kwenye Bunge la katiba ilipangwa kuwa vile!Sasa watakamilisha!!

Maoni huru!!
 
Katiba mpya huwa haipatikani bila kuchapana. TUCHAPANE KWANZA

Kuchapana haliwezi kuwa chaguo letu. Anayetaka kuchapana atatukuta Tahrir.

Kukusanyika kudai haki yetu popote ni haki yetu.
 
Kuchapana haliwezi kuwa chaguo letu. Anayetaka kuchapana atatukuta Tahrir.

Kukusanyika kudai haki yetu popote ni haki yetu.
Ni wazo zuri. Nami naitamani siku kama hiyo ifike. Lakini wasiwasi wangu hulka ya vikosi vya ulinzi na usalama kutokuheshimu haki hiyo
 
Ni wazo zuri. Nami naitamani siku kama hiyo ifike. Lakini wasiwasi wangu hulka ya vikosi vya ulinzi na usalama kutokuheshimu haki hiyo

Unahofia vikosi vya ulinzi na usalama? Ni nia yako usiumie? Mbona hata kufa imo mkuu?

Tutawaomba waoga wote kutupisha.

Hao ndiyo wamekuwa wakitugharimu muda wote.

Kwa hakika huu mchezo hautuhitaji wote bali wachache walio na wito kamili. Wengine hata mkikaa kimya mbona ni sawa tu.
 
Kifo kinatisha mkuu, siyo rahisi kwa mtanzania kujitolea kufa. Ujasiri huu upo nchi za wenzetu, lkn hapa kwetu, mmh!
 
Kifo kinatisha mkuu, siyo rahisi kwa mtanzania kujitolea kufa. Ujasiri huu upo nchi za wenzetu, lkn hapa kwetu, mmh!

Ileweke hivi mkuu. Usitusemee na wengine. Kwenu nyie waoga, tuwaombe kwa heshima na taadhima kukaa kimya kuhusu huu mpambano. Huu ninyi hauwahusu wala hamtasikia tukiwalaumu.
 
Back
Top Bottom