Donyongijape
JF-Expert Member
- May 28, 2010
- 1,497
- 814
Habari za asubuhi wadau. Asubuhi ya Leo Nimesikia taarifa maalumu ya mtu anayeitwa PJ, wa Clouds FM, akiitoa kuhusu vikao vya bunge maalumu huko Dodoma. Taarifa ile ilikuwa ikiwaambia wananchi kile kinachoendelea huko na kuwapa taadhari kuwa kuna kikundi kimejiandaa kuvunja bunge hilo. Huku pia akisema kuwa kuna mjumbe mmoja ambaye ni kiongozi wa juu kabisa wa chama cha upinzani aliteuliwa kuingia kwenye kamati ya uongozi lakini kwa sababu 'anazozijua mwenyewe' akajitoa.
Tatizo langu hapa ni namna ya uwasilishaji wa taarifa hiyo. Haijafuata ueledi wa habari kwani haikuwa na FACTS kama taaluma ya habari inavyotaka. Ilikuwa haina vithibitisho vya hizo njama, au kuwapa wasikiliazi fursa ya kusikiliza kile kilichotokea katika bunge hilo.
Mimi naona huu ni UCHOCHEZI ambao ni hatari kwa taifa na unalenga kujenga chuki miongoni mwa jamii. Mamlaka inayohusika na vyombo vya habari inabidi kuingilia kati na kutoa adhabu stahiki kwa vyombo vya habari vya namna hii. La sivyo vitatufikisha katika hali mbaya na kuhatarisha amani ya nchi.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.