Katiba Mpya: Clouds FM Wachochezi!

Katiba Mpya: Clouds FM Wachochezi!

Hao jamaa wamegeuka kuwa chombo cha habari na propaganda za CCM...kwenye Tv yao ndani ya King`amuzi cha Azam huwa napita nikiwa nashuka chini kutazama Sentanta Tv yangu.
Nikakuta wameanzisha kitu wanaita Uzalendo Kwanza sijui nini niniiiii....jamaa anaongea nyuma background ni bendera ya Tanzania,anasema rangi ya blue ktk bendera ni bahari inayotuunganisha Tz Bara na Visiwani ili kuuimarisha Muungano.(Upotoshaji mkubwa,anasahau hiyo blue hata ziwa Rukwa inawakilishwa nayo)
Wanatumika kubeba hoja ya Serikali mbili,wanatumika kuua hoja ya serikali tatu na Mamlaka kamili ya Znz,wanapotosha watu juu ya kuidai Tanganyika itambulike.
Huyo PJ ni mzee fulani anayetumika bila kujijua....wasamehe bure,hata shule zao vichwani ni za mashaka,ni lazma wajipendekeze ili wabaki mjini

Waandae tu disco zao haya mambo ya siasa hawayawezi, wamwulize mwenzao yule wa kasha sasa hivi anahenyeka na ICC
 
Hao jamaa wamegeuka kuwa chombo cha habari na propaganda za CCM...kwenye Tv yao ndani ya King`amuzi cha Azam huwa napita nikiwa nashuka chini kutazama Sentanta Tv yangu.
Nikakuta wameanzisha kitu wanaita Uzalendo Kwanza sijui nini niniiiii....jamaa anaongea nyuma background ni bendera ya Tanzania,anasema rangi ya blue ktk bendera ni bahari inayotuunganisha Tz Bara na Visiwani ili kuuimarisha Muungano.(Upotoshaji mkubwa,anasahau hiyo blue hata ziwa Rukwa inawakilishwa nayo)
Wanatumika kubeba hoja ya Serikali mbili,wanatumika kuua hoja ya serikali tatu na Mamlaka kamili ya Znz,wanapotosha watu juu ya kuidai Tanganyika itambulike.
Huyo PJ ni mzee fulani anayetumika bila kujijua....wasamehe bure,hata shule zao vichwani ni za mashaka,ni lazma wajipendekeze ili wabaki mjini

Waandae tu disco zao haya mambo ya siasa hawayawezi, wamwulize mwenzao yule wa kenya sasa hivi anahenyeka na ICC
 
Kwa kusema hivyo tayari anatakiwa kua mtuhumiwa namba moja.

Tatizo hivi vyeo vya ukuu wa wilaya na mikoa unawapumbaza sana wanahabari walio wengi hadi kusababisha msamiati wa ukanjanja uzidi kushamili bila kusahau bahasha za kaki.
 
Huyo pj, akae akijua kuwa the hague hakuna upendeleo na tutamsikia analialia oo mie sikusema! Amuulize Arap Sang wa kenya mwanahabari kama yeye leo anashinda huko badala ya kukaa na familia yake.tumewachoka hao mizoga
 
Amuulize Arap Sang wa kenya mwanahabari kama yeye leo anashinda huko badala ya kukaa na familia yake.
Una maanisha anashinda mamtoni, anakwea pipa kama anapanda daladala za mwenge posta vile.
 
Hakuna cha ajabu hapo. PJ ni kama wa ccm, alijitosa ubunge kura za maoni jimbo la Kawe, kura hazikutosha kwani alitanguliwa na Kina Kipi Warioba, Angela Kiziga, Adamjee na wengine. Pengine kwa kupotosha umma kupitia redio yao hiyo, anadhani 2015 kura za maoni zitamtosha.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Ni kweli mkuu, Lakini PJ anapata nguvu zaidi kutokana misimamo ya uongozi wa Clouds ambao wameamua kukamata fursa kupitia CCM.Hizi network zitakufa very soon na tutabaki na majeruhi wengi watakaokosa hata pa kuficha nyuso zao.
 
Kuna watu hawana haibu hapa duniani na miongoni mwao ni wale wanaojiita 'ccm damu' ambao hii radio nayo ni kitengo chao cha propaganda.
Nia yao ni kuwa kuliko mawazo ya wananchi walio wengi kutekelezwa ni bora sote tukose, na kinara wao keshasema kuwa hii kitu haitawezekana labda mpaka aondoke madarakani! Tambua hili
 
Nilishangaa , halafu hata hawajamuhoji Lipumba akasema sababu za kujitoa wao wanamnaga tu . hawa jamaa ni Mungiki kabisa
 
Hakuna cha ajabu hapo. PJ ni kama wa ccm, alijitosa ubunge kura za maoni jimbo la Kawe, kura hazikutosha kwani alitanguliwa na Kina Kipi Warioba, Angela Kiziga, Adamjee na wengine. Pengine kwa kupotosha umma kupitia redio yao hiyo, anadhani 2015 kura za maoni zitamtosha.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
Kumbe amewahi kujitosa kugombea ubunge....!!
Basi ndio maana huwa anaongea vile redioni.....!
 
Una maanisha anashinda mamtoni, anakwea pipa kama anapanda daladala za mwenge posta vile.

Ee si unasikia kaka kesi ikisikilizwa leo wanaambiwa baada ya siku 7 mwenzake anarudi yeye anabaki kule.
 
Naamin kama TCRA wapo makin watawahoji,moja ya mistari ya PJ ile inayosema kuna njama za kuifanya tanzania isitawalike baada ya kuvuruga mchakato wa katiba,,,,kumepangwa kufanyika machafuko pande zote za nchi hii,binafsi nilishtuka

Hao achaneni nao bali muda muafaka ukifika watakuwa Historia na kuwajibika kwa matendo yao binafsi na sio Radio Clouds
 
Ni sera ya hii Radio kupumbaza watanzania na si ajabu kusikia habari zisizo na weledi ili mradi tu ziwe upande wa magamba!Hata mimi naamini iko siku watalazimika kuwajibika kwa maneno yao!

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Watafanya nn jamani na wanataka kuishi vizuri mjin? Yani hao jamaa kila kitu wanajua wao na wanacho amini wao ndo wanataka watu wote tukikubali, kwao wao jd ni mbaya basi na ss wote tukubali hvyo
 
Habari za asubuhi wadau. Asubuhi ya Leo Nimesikia taarifa maalumu ya mtu anayeitwa PJ, wa Clouds FM, akiitoa kuhusu vikao vya bunge maalumu huko Dodoma. Taarifa ile ilikuwa ikiwaambia wananchi kile kinachoendelea huko na kuwapa taadhari kuwa kuna kikundi kimejiandaa kuvunja bunge hilo. Huku pia akisema kuwa kuna mjumbe mmoja ambaye ni kiongozi wa juu kabisa wa chama cha upinzani aliteuliwa kuingia kwenye kamati ya uongozi lakini kwa sababu 'anazozijua mwenyewe' akajitoa.

Tatizo langu hapa ni namna ya uwasilishaji wa taarifa hiyo. Haijafuata uelewe wa habari kwani haikuwa na FACTS kama taaluma ya habari inavyotaka. Ilikuwa haina vithibitisho vya hizo njama, au kuwapa wasikiliazi fursa ya kusikiliza kile kilichotokea katika bunge hilo.

Mimi naona huu ni UCHOCHEZI ambao ni hatari kwa taifa na unalenga kujenga chuki miongoni mwa jamii. Mamlaka inayohusika na vyombo vya habari inabidi kuingilia kati na kutoa adhabu stahiki kwa vyombo vya habari vya namna hii. La sivyo vitatufikisha katika hali mbaya na kuhatarisha amani ya nchi.
God bless us
 
Jifunzeni kusikia hoja mbadala wa zile mnazopenda kusikia. Sio kila mtu aliye na mawazo tofauti na yale mnayoyapenda, hana akili.
Hoja ipi inayopingwa hapa. Watu wanajadili usahihi wa taarifa na jinsi ilivyowasilishwa
 
Back
Top Bottom