Katiba inasemaje kuhusu uteuzi wa Bashiru Ally?

Hapo siyo!
Nimeshakwambia maana ya mtu anayeshika nafasi ya KATIBU MKUU au mwenye sifa ya kuwa Katibu Mkuu siyo KATIBU MKUU WA CCM.
Sifa ya kuwa KATIBU MKUU wa BARAZA LA MAWAZIRI ni angalao awe alishawahi kuwa KATIBU MKUU WA WIZARA mojawapo(experience)!
Hebu fuatilia ujue utujuze kama Marehemu Kijazi alitokea CCM akiwa KM wa CCM.....!!
Habari uelewiki mwenye sifa lakini asiwe katibu mkuu wa CCM. Jee kwa hapo katiba Haito vunjwa kama atakuwa katibu mkuu kiongozi kutoka cha Upinzania?
 
Pamekuwa na kambi mbili katika uteuzi huu na msaada wa wadau wa katiba na sheria unaweza kutupa mwanga.

Najua kuna jukwaa la mambo ya sheria lakini uteuzi huu una athari za kisiasa ambazo inawezekana kwa sasa hazipo wazi.

Tusaidieni tujue ukweli ni upi?

Mkuu, imekaa hivi:

1. Neno "Katibu Mkuu Kiongozi" halijaandikwa mahali popote kwenye Katiba ya JMT, 1977 (as amended);

2. Ibara ya 36 (1) na (2) ya Katiba ya JMT, 1977, inampatia mamlaka Rais kufanya uteuzi wa nafasi mbalimbali za watendaji wakuu wa serikali ikiwemo "Katibu Mkuu Kiongozi ";

3. Kwa muktadha wa Ibara ya 36 (2) ya Katiba ya JMT, 1977, Bunge limetunga Sheria ya Utumishi wa Umma (marejeo ya mwaka 2019) ambapo Kifungu cha 4(1) cha Sheria kinamtaka wazi kuwa Rais atakuwa na mamlaka ya kumteua "Katibu Mkuu Kiongozi";

4. Labda kama kuna sheria au miongozo mingine ambayo sifahamu inayosimamia uteuzi wa "Katibu Mkuu Kiongozi", katika utafiti wangu mfupi nimegundua kuwa kifungu cha 4(1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, 2019, au hata Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma, 2009 (Toleo la Tatu), hazijaweka wazi sifa za mtu anayetakiwa kuteuliwa kushika wadhifa wa "Katibu Mkuu Kiongozi". Kwa msingi huu, Rais anayo nafasi ya kumteua mtu yeyote ambaye anaamini atamsaidia vema ktk kutekeleza majukumu yake katika nafasi ya "Katibu Mkuu Kiongozi"; na

5. Pamoja na wajibu mwingine, Katibu Mkuu Kiongozi aliyeteuliwa kwa mujibu wa Kifungu cha 4 (1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, 2019, ndiye anakuwa "Katibu wa Baraza la Mawaziri" kama ilivyotajwa katika Kifungu cha 4(2) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, 2019, na Ibara ya 60 ya Katiba ya JMT, 1977.

Kwa imani yangu thabiti, uteuzi wa Dr. Bashiru kuwa "Katibu Mkuu Kiongozi" ni sahihi na halali na hakuna Katiba au sheria iliyovunjwa.

Maandishi yanayosambaza mitandaoni kuhusu sifa za mtu anayetakiwa kuteuliwa kushika nafasi ya "Katibu Mkuu Kiongozi" ni mojawapo ya Ibara katika Katiba iliyopendekezwa na Jaji Warioba.

Katiba ya Jaji Warioba haikupitishwa na haitumiki popote. Kwa hiyo, sio sahihi kufanya marejeo katika sheria ambayo haipo.

By the way, Katiba ya Jaji Warioba iliweka utaratibu mzuri sana wa namna ya kumpata "Katibu Mkuu Kiongozi" na nafasi zingine ktk utumishi wa umma.

Nawasilisha.
 
Kitu ambacho nikiona ni watu kuamua kubisha tu bila evidence simply because wao wanataka kuwa wapinzani, hata ukiwa elimisha wana kuambia wewe ni ccm , huwezi jifunza bila kukubali maoni ya watu wengine.
 
Mtoa hoja anaongelea katiba gani?vipi tuna katiba au tuna no 1 ambaye kila kitu kinamzunguka yeye?nchi haina katiba ila tuna very very strong statesman.
Utakuwaje doctor mkuu na wakati hujawahi kuwa dr ?? Kuwa katibu mkuu kiongozi lazima ushawahi kuwa katibu mkuu wizara Fulani .
 
hakuna kosa lolote, kwa sababu sio dhambi kuwa mwanachama wa chama chochote kile cha siasa na wakati huo huo ukawa mtumisha wa uma, isipokuwa hauruhusiwi tu kuwa mwanasiasa wa majukwaani, pia hupaswi kujihusisha na shughuli za kisiasa,
Unajuwaje pia hata mtangulizi wake alikuwa mwanachama wa chama tawala? ila hakujihusisha wala kujionyesha hadharani au kwenye majukwaa.
na kinyumebchake pia inawezekana ilimradi tu uzingatie sheria na miiko iliyopo na ukaendelea na itikadi yako kimya kimya! maana wakati huo sasa unazuiwa na sheria na taratibu.

..unadhani kwanini watumishi wa serikali hawatakiwa kujionyesha hadharani kisiasa, na kushiriki siasa za majukwaani?
 
Unajua kama jamaa ni kutoka karibu na multi-choice Tanzania?

Na pia kabla hapo ameshateuliwa ubalozi au ulitaka utumishi wa uuma upi?

Ebu jaribu kusoma majukumu ya katibu mkuu kwanza.
..Balozi huwa anawakilisha nchi, au anaongoza idara ya wizara ya mambo ya nje.

..Je, alikuwa balozi alituwakilisha nchi gani? Au, aliteuliwa balozi ktk idara gani ya wizara ya mambo ya nje?

..Huu uteuzi umefanyika kwa kufukia-fukia ili uteuzi upate nguvu za kisheria na kikatiba.

..Njia zilizotumika kumteua Dr.Bashiru kwa maoni yangu siyo sahihi, na hazileti ushawishi kwamba katiba yetu na sheria zinazingatiwa.

..Raisi kama ana mtu anataka kumteua, lakini hana sifa za kikatiba na kisheria, anachotakiwa ni kumuingiza kwanza ktk utumishi wa serikali, halafu ana-accelerate his/her promotions, mpaka anafikia ngazi ya nafasi ambayo amelengwa kuteuliwa.

..Kwa mfano, Raisi anaweza kuwa anataka kumteua mtu fulani[labda ana PhD, mwanasheria mahiri] kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufaa. Kitu cha kwanza atakachofanya ni kumteua kwenda mahakama kuu. Baada ya muda anaweza kum-promote kuwa Jaji Kiongozi, au kuwa Jaji Mahakama ya Rufaa. Baada ya hapo ndio amteue kuwa Jaji Mkuu.

..Hiki kilichotokea Wamakonde wana msemo wao wanasema, " the means justify the ends. "
 
..Hiki kilichotokea Wamakonde wana msemo wao wanasema, " the means justifies the end. "
Labda tueleze huyu alichaguliwa/kuteuliwa kwa kazi gani? Then alipewa kazi gani? Waswahili wanasema jambo usilolijua ni kama usiku wa kiza.
 
Habari uelewiki mwenye sifa lakini asiwe katibu mkuu wa CCM. Jee kwa hapo katiba Haito vunjwa kama atakuwa katibu mkuu kiongozi kutoka cha Upinzania?

..kwenye uteuzi huu Magufuli katoa boko.

..haileti picha nzuri kuteua mwanasiasa kuwa katibu mkuu kiongozi.

..katibu mkuu kiongozi anakwenda kusimamia nidhamu na maadili ya watumishi wa serikali.

..moja ya makatazo ktk utumishi wa serikali ni kushiriki siasa za vyama na majukwaani.

..sasa mtu ambaye anajulikana waziwazi ushiriki wake ktk siasa ataaminika vipi kuwasimamia watumishi wa serikali?

..uteuzi unaweza kuwa wa kisheria, maana wamelazimisha awe balozi kwanza, lakini nadhani hauleti picha nzuri.

..naamini Tanzania ina watu wengi sana wenye sifa na vigezo vya kuwa Katibu Kiongozi, na wasiokuwa na makando-kando ya kisiasa kama Dr.Bashiru. Hakukuwa na ulazima wa kulazimisha uteuzi huu.

NB:

..Hakuna katiba ambayo ni perfect imeeleze kila kitu. wakati mwingine kunahitajika busara na uungwana.

..Wamarekani wana katiba nzuri, lakini walipata matatizo walipochagua Raisi Trump ambaye hakuwa na busara, na si muungwana.
 
Mkuu MIGNON, nimeshawishika nami kujiunga katika mjadala huu wa 'kuelimishana' juu ya katiba na sheria.

Sijaona ukipewa jibu la kukuelimisha/kutuelimisha.

Lakini, pengine iwe ni kutumia tu fursa kuelimika, na sio kwamba hicho kilichomo kwenye sheria/Katiba kinamanufaa yoyote kwa wakati huu tuliomo; kwani Katiba na sheria hata kama zipo zinazozungumzia uteuzi huu, mteuzi kama ujuavyo hadi sasa hazuiwi na Katiba au sheria yoyote kufanya anayoona yeye yanafaa.

Kuna mifano mingi inayoonyesha kuwa kiongozi huyu hazuiwi na sheria wala katiba. Kwa hiyo pengine kuhoji/kuelimishwa unakotafuta hapa kutokana na uteuzi huu, pengine ni kujiridhisha tu kuwa Katiba na sheria zipo zinazohusu aina ya uteuzi huu, hata kama hazifuatwi.

Nami pia ningependa kuelimika tu juu ya hili, hata kama sihoji chochote juu yake, kwa kujua kuwa ni utaratibu wa kawaida wa mteuzi.
Naomba ni Mimi niulize,Kama haheshimu katiba na Sheria,hicho cheo chake Cha urais anakipata wapi ?
 
Eeenh, hili swali kweli umeliwazia vizuri mkuuu 'sijijui?

Hivi uchaguzi uliofanyika ulikuwepo hapa, au uliusikia tu?

Huo 'uchafuzi' ulifuata taratibu za kikatiba; kiasi kwamba hata matokeo yake yataiheshimu katiba?

Kwani 'Katiba' haiogopi bunduki na mabomu ya machozi?

Nimekujibu kadri nilivyoelewa swali lako.
 
Mkuu MIGNON, nimeshawishika nami kujiunga katika mjadala huu wa 'kuelimishana' juu ya katiba na sheria.

Sijaona ukipewa jibu la kukuelimisha/kutuelimisha.

Lakini, pengine iwe ni kutumia tu fursa kuelimika, na sio kwamba hicho kilichomo kwenye sheria/Katiba kinamanufaa yoyote kwa wakati huu tuliomo; kwani Katiba na sheria hata kama zipo zinazozungumzia uteuzi huu, mteuzi kama ujuavyo hadi sasa hazuiwi na Katiba au sheria yoyote kufanya anayoona yeye yanafaa.

Kuna mifano mingi inayoonyesha kuwa kiongozi huyu hazuiwi na sheria wala katiba. Kwa hiyo pengine kuhoji/kuelimishwa unakotafuta hapa kutokana na uteuzi huu, pengine ni kujiridhisha tu kuwa Katiba na sheria zipo zinazohusu aina ya uteuzi huu, hata kama hazifuatwi.

Nami pia ningependa kuelimika tu juu ya hili, hata kama sihoji chochote juu yake, kwa kujua kuwa ni utaratibu wa kawaida wa mteuzi.
Kupitia mijadala ndiyo raia wanaweza kuonyeshana kama kweli katiba na sheria zinakiukwa. Hata mijadala hii haitasaidia kubatilisha ukiukwaji huu basi angalau kumbukumbu zitawekwa kwa ajili ya vizazi vijavyo na historia ya taifa letu. Kama kweli ukiukwaji wa katiba na sheria utadhihirika bila shaka huko mbele ya safari hali hiyo itataxamwa kikatiba.
 
Eeenh, hili swali kweli umeliwazia vizuri mkuuu 'sijijui?

Hivi uchaguzi uliofanyika ulikuwepo hapa, au uliusikia tu?

Huo 'uchafuzi' ulifuata taratibu za kikatiba; kiasi kwamba hata matokeo yake yataiheshimu katiba?

Kwani 'Katiba' haiogopi bunduki na mabomu ya machozi?

Nimekujibu kadri nilivyoelewa swali lako.
Kama nimekuelewa ,unachotaka kusema ni kuwa, kwa Sasa nchi yetu haina rais kwa mujibu wa katiba yetu,siyo?
 
Back
Top Bottom