Katiba inasemaje kuhusu uteuzi wa Bashiru Ally?

Kwani hizo teuzi haziwezi kuwa simultaneously?

Mbona kuna mawaziri ambao huwa wanateuliwa kuwa wabunge na kuwa mawaziri kwa wakati mmoja....au nakosea?
Wanateuliwa kwanza kuwa wabunge halagu wanateuliwa kuwa mawaziri, na siyo kinyume chake.
 
Mods naomba tuuache uzi huu ujitegemee ili tuweze kupata mwanga wa kikatiba na kisheria kuhusu uteuzi tajwa.Pamekuwa na kambi mbili katika uteuzi huu na msaada wa wadau wa katiba na sheria unaweza kutupa mwanga.
Najua kuna jukwaa la mambo ya sheria lakini uteuzi huu una athari za kisiasa ambazo inawezekana kwa sasa hazipo wazi.
Tusaidieni tujue ukweli ni upi?
Katiba tupa kule kwa sasa ni one man show tu
 
Huyu Nshomile kwa sound hajambo! Anachoongea na vitendo Ni vitu 2 tafauti....!!!CCM Ina watu wengi wako wapi???
Yaleyale ya Mr. Slowslow toka KATIBU MWENEZI kuwa Mbunge.....!!! Bashiru toka KM-CCM kuwa KMK....!!!Kwanini hakumshauri hajakataa uteusi huu na kunshauri Mwenyeki wake ateue watu wengine????
Anasema atakomesha watu kukalia vyeo na hatakubali UTEUZI mwingine wowote🤣 na hapohapo anasema unateuliwa kwa UWEZO WAKO NA UTII WAKO😁 Sasa ikitokea Magu akamteua kwene Ubunge na kumpa UWAZIRI atakataaje na YEYE NI MTIIFU KWA MAGUFULI😂😂😂
 
Hata kwa hii "katiba", bado haijavunjwa. Hasa ukisoma hicho kipengele cha 7 chote (kwenye hii attachment yako kimekatika).

Tuondolee 'utopolo' wako hapa. Afisa Mwandamizi anayeshika nafasi ya KATIBU MKUU maana yake siyo KATIBU MKUU WA CCM baali Ni KATIBU MKUU kwenye moja ya Wizara! Je, unataka kunambia CCM nayo ni Wizara??
 
Hapana. Weka hapa hicho kipengele cha 7 chote, ili kila mtu asome. Utaona kuwa si lazima mtu awe katibu mkuu bali hata wenye sifa za kuweza kuchaguliwa katibu mkuu. Lakini ukisoma katiba ya sasa, hakuna sehemu ilipovunjwa (tena yenyewe haiweki mipaka) na pia Public Services Act pia haijavunjwa.

Sikubaliani na JPM kwenye mambo mengi tu (soma posts zangu humu JF), lakini napenda kuwa objective.

In fact, hata kwenye huu uteuzi wa Bashiru nina reservations zangu nyingi tu, but sio katiba kuvunjwa.
 
Hicho kipengele chote cha 7 unachotumia kama kichaka kinasemaje? Kama kinatetea hoja yako ya Uteuzi wa KATIBU MKUU CCM si ukiweke basi??
 
Hicho kipengele chote cha 7 unachotumia kama kichaka kinasemaje? Kama kinatetea hoja yako ya Uteuzi wa KATIBU MKUU CCM si ukiweke basi??
Soma tu katiba ya sasa (katibu wa baraza la mawaziri). Hiyo ya katiba ya Warioba ambayo wajenga hoja humu wanaitumia haitumiki kwa sasa. Kwa hivyo nilikuwa tu najaribu kujenga hoja kuwa hata kwa kutumia hiyo Katiba ya Warioba bado haijavunjwa. Ndio kwenye post yangu nikamuomba aliyeweka nukuu, aweke hicho kipengele cha 7 chote kinachotoa tafsiri ya afisa mwandamizi...

"116(7) Kwa madhumuni ya Ibara hii, maneno “Afisa Mwandamizi aliye katika nafasi ya uteuzi” maana yake ni mtu anayeshika nafasi ya Katibu Mkuu au mwenye sifa ya kuwa Katibu Mkuu au cheo kingine kinachofanana na hicho."

Hapo vipi?
 
Mods naomba tuuache uzi huu ujitegemee ili tuweze kupata mwanga wa kikatiba na kisheria kuhusu uteuzi tajwa.Pamekuwa na kambi mbili katika uteuzi huu na msaada wa wadau wa katiba na sheria unaweza kutupa mwanga.
Najua kuna jukwaa la mambo ya sheria lakini uteuzi huu una athari za kisiasa ambazo inawezekana kwa sasa hazipo wazi.
Tusaidieni tujue ukweli ni upi?
We nae mamlaka za serikali zinatokana na siasa na mliruhusu mfumo wa vyama vingi,sasa unakuja na swali gani hili
 
Rais tuliye naye anajua yeye ndiye sheria na mnapoyajadili haya atakuwa anawashangaa sana mlivyochanganyikiwa akili.
 
Soma tu katiba ya sasa (katibu wa baraza la mawaziri). Hiyo ya katiba ya Warioba ambayo wajenga hoja humu wanaitumia haitumiki kwa sasa. Kwa hivyo nilikuwa tu najaribu kujenga hoja kuwa hata kwa kutumia hiyo Katiba ya Warioba bado haijavunjwa. Ndio kwenye post yangu nikamuomba aliyeweka nukuu, aweke hicho kipengele cha 7 chote kinachotoa tafsiri ya afisa mwandamizi...

"116(7) Kwa madhumuni ya Ibara hii, maneno “Afisa Mwandamizi aliye katika nafasi ya uteuzi” maana yake ni mtu anayeshika nafasi ya Katibu Mkuu au mwenye sifa ya kuwa Katibu Mkuu au cheo kingine kinachofanana na hicho."

Hapo vipi?
Hapo siyo!
Nimeshakwambia maana ya mtu anayeshika nafasi ya KATIBU MKUU au mwenye sifa ya kuwa Katibu Mkuu siyo KATIBU MKUU WA CCM.
Sifa ya kuwa KATIBU MKUU wa BARAZA LA MAWAZIRI ni angalao awe alishawahi kuwa KATIBU MKUU WA WIZARA mojawapo(experience)!
Hebu fuatilia ujue utujuze kama Marehemu Kijazi alitokea CCM akiwa KM wa CCM.....!!
 
  • Thanks
Reactions: SMU

Sawa. Tuletee hivyo vipengele vya sheria. Ukishakuwa mhadhiri wa chuo kikuu cha umma na baadae kuteuliwa kuwa katibu mkuu wa ccm unapoteza sifa za kuteuliwa kuwa katibu mkuu wa wizara au katibu mkuu kiongozi?

Katiba yetu haina hilo zuio na hata hiyo ya Warioba haina hilo zuio.
 
..utumishi wa umma ni serikali kuu na taasisi zake.

..watumishi waandamizi ni manaibu katibu wakuu, makatibu wakuu, na wateule wa raisi ktk taasisi za serikali.
Unajua kama jamaa ni kutoka karibu na multi-choice Tanzania?

Na pia kabla hapo ameshateuliwa ubalozi au ulitaka utumishi wa uuma upi?

Ebu jaribu kusoma majukumu ya katibu mkuu kwanza.
 
Sawa. Tuletee hivyo vipengele vya sheria. Ukishakuwa mhadhiri wa chuo kikuu cha umma na baadae kuteuliwa kuwa katibu mkuu wa ccm unapoteza sifa za kuteuliwa kuwa katibu mkuu wa wizara au katibu mkuu kiongozi.
Katiba yetu haina hilo zuio na hata hiyo ya Warioba haina hilo zuio.

Mkuu in brief niseme hivi:
Hapa hakuna Katiba iliyofuatwa si ya Katiba hii tuliyo nayo Wala Katiba Pendekezwa ya Jaji Warioba!!!
Katiba inayotumika kwa sasa ni ya JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI..Yeye ndiye kila kitu: Yeye ndo Katiba, yeye ndo Serikali, Yeye ndiye Bunge,Yeye ndiye Mahakama na yeye ndiye Waziri wa Fedha.😎
 
Hapo sawa
 
Kwa kifupi JIWE kachemka sana na hakuna mtu wa kumwambia. Chief Secretary ilipaswa atoke miongoni mwa maafisa waandamizi wa serikali siyo mtumishi wa chama cha siasa.

Mbona kawaida tu, hujiulizi nafasi ya DEDs ambayo wanapaswa wateuliwe kati ya wakuu wa idara seniors ila awamu hii hata kama mtu yuko kitaa sio public servant anapewa

MIMI SIPANGIWI
 
..kwa hiyo kumtoa mtu ofisi ya chama na kumpeleka ofisi ya umma hamna makosa?
hakuna kosa lolote, kwa sababu sio dhambi kuwa mwanachama wa chama chochote kile cha siasa na wakati huo huo ukawa mtumisha wa uma, isipokuwa hauruhusiwi tu kuwa mwanasiasa wa majukwaani, pia hupaswi kujihusisha na shughuli za kisiasa,
Unajuwaje pia hata mtangulizi wake alikuwa mwanachama wa chama tawala? ila hakujihusisha wala kujionyesha hadharani au kwenye majukwaa.
na kinyumebchake pia inawezekana ilimradi tu uzingatie sheria na miiko iliyopo na ukaendelea na itikadi yako kimya kimya! maana wakati huo sasa unazuiwa na sheria na taratibu.
 
Soma 116(2) atakuwa katibu wa baraza wa usalama wa Taifa.

Unamjua Bashiru kijuu juu.
Wewe ata kuelewa uelewi...kua katibu wa bara za la usalama wa Taifa ni baada ya kua katibu kiongozi sio kabla ya apo.Tatizo ni lugha au?
 
Back
Top Bottom