Kati ya Udaktari na Uinjinia taaluma ipi inalipa zaidi

Kati ya Udaktari na Uinjinia taaluma ipi inalipa zaidi

Achana na Dr we we unampelekea mkeo na unamuacha ndani wewe nje na akimaliza kumuona mkeo unamshukuru... Bado tu umuheshimu
 
mnajaribu tu kustuastua eti dr na eng yan hiyo taaluma ya udokta acheni kama ilivyo halafu ni kama fedhea me naona kumuweka dr na eng eti wachuane kwnza eng hafui dafu hata kwa mwalimu wa primary!!
 
wapo wengi mkuu kwa Mwanza ongezea na huyu Dr malietta mahendega
Kumbe unamjua huyo mmoja ambae anajulikana mwanza tu,ulizia makampun makubwa ya construction,land survey,electrical,civil engineering au architecture ujue balaa lao kwa hela wanazomiki kutokana na proffesional zao,but madaktar wanakua na hela ya kawaida tu maybe wajiingize kwenye biashara nyengine,..
 
Hapana DK.ndiyo anaheshimika hata kwenye scale ya mishahara daktari anamzidi mhandisi kwa mbali.Sehemu zingine kama kijijini ukiuliza mhandisi hawajui ni nani lakini daktari hata madongo paromoka wanamjua.

jama hujui ukiongeacho...ni sawa DK analipwa vizuri lakini ni kwa starting salary tu...Engineering akishspata experience analipwa si chini ya M3 na kuendelaea sio Dk kalipwa sana M2.5 haya achana na habari ya mshahara hivi unajua anakula malupulup kiasi gani...mfano ujenzi ni Billion 42 Architect analipwa noy less than 6% Qs 3% structural engineer 3%...contractor sasa anakula profit kwenye kili material anayonunua
 
Zote ni nzuri inategemea tu na uchapakazi wako. Tofauti kubwa ni kwamba, madaktari wanakubalika na kuheshimika kwa upana zaidi katika jamii kuliko wahandisi kwa sababu kazi yao inawakutanisha moja kwa moja na watu wa aina zote, wakati wahandisi kufahamika kwa kazi zao tu ni tabu. Watu wa kawaida hawafahamu kabisa kazi za wahandisi, wapo wanaomuona fundi anaepanga tofali kujenga ukuta ni bora zaidi kuliko mhandisi.

kufahamik ndio nini kikubwa ni ulaji kingn uhandisi sio matofalo tu ni pana sana wapo kweny kilimo wapo kweny mazingira wapo kweny migodi,umeme, uchukuzi, aisee ni pana sana
 
jama hujui ukiongeacho...ni sawa DK analipwa vizuri lakini ni kwa starting salary tu...Engineering akishspata experience analipwa si chini ya M3 na kuendelaea sio Dk kalipwa sana M2.5 haya achana na habari ya mshahara hivi unajua anakula malupulup kiasi gani...mfano ujenzi ni Billion 42 Architect analipwa noy less than 6% Qs 3% structural engineer 3%...contractor sasa anakula profit kwenye kili material anayonunua

Ninajua nikiongeacho nashukuru umekili DK.anamzidi mhandisi mshahara,hivyi hujui kuwa madaktari wana hospitari zao? unajua wanaingiza pesa kiasi gani, unajua faida anayopata kwa laparatomy au laparoscopy moja anayofanya kwenye hosp.yake? consultation wanazofanya kwenye mahosp.mengine unajua wanapata sh.ngapi?halafu anasaidiana na Mungu kumrudishia mwanadamu uhai! halafu heshima debe hehehehehe.Udaktari kitu kingine.
 
Ninachojua mimi hakuna daktari Tajiri but maengineer matajir wapo kibao hapa mjini, madaktar wanakua na hela yao ya kubadilishia mboga tu

Nadeclare interest kuwa nami ni mmoja wa wanataaluma wa engineering! Sasa mimi nawacha watu mufanye tathmini wenyewe! Mradi mmoja wa Mkapa bridge, National Stadium, JubileeTowers, Bank kuu twin towers, Umoja bridge, Udom, hii yote kila mmoja haupungui 50bn/- na kuendelea. Sasa ukichukua mifano ya miradi hiyo ambayo ni mult billion na kwa kuwa wasimamiz wakuu wa miradi hiyo ni Engineers, basi amua wenyewe nani yuko poa!
 
Lawyer/Advocate ndio kila kitu, heshima juu lakini taaluma nyingine hizo njaa tu kama mhandisi mpaka uibe misumali na chokaa, naye dokta mpaka uibe panadol na pamba za wagonjwa ndo upate hela.
 
kupata hela kutokana na udaktari au kutengeneza fedha kutokana na uhandisi sio problem.
Problem ni fedha hiyo unaifanyia nini?
Naona hunielewi!
Iko hivii
tatizo sio kupata pesa tatizo ni kuimiliki fedha.
Upo?
Mkulima anaweza kumiliki makampuni akamuajiri huyo dr & engineer.
 
Lawyer/Advocate ndio kila kitu, heshima juu lakini taaluma nyingine hizo njaa tu kama mhandisi mpaka uibe misumali na chokaa, naye dokta mpaka uibe panadol na pamba za wagonjwa ndo upate hela.
Wewe hukijui ukiongeacho,mtu akibishana na wewe ataonekana taahira tu,mm namjua lawyer mwenye hela ni nurdin mkono peke yake,nitajua 10 ma lawyer na Mimi nikutajie maengineer 20 famous sio wa mtaani kwetu
 
Engineering inalipa sana kwa suala la pesa, hilo liko wazi na ni kutokana na posho nyingi pia makampuni yanatofautiana. Mwanafunzi wa engineering akiwa PT anaweza lipwa hata 15000 per day ( mf mimi nimelipwa hivyo nilipokuwa PT1 enzi hizo). Tatizo ni kuwa engineer anajitafutia kazi bt daktari anapangwa na serikali. So tukizungumzia kulipa ni upatikanaji wa ajira bas hata ualimu ni dili sana.
 
Wewe hukijui ukiongeacho,mtu akibishana na wewe ataonekana taahira tu,mm namjua lawyer mwenye hela ni nurdin mkono peke yake,nitajua 10 ma lawyer na Mimi nikutajie maengineer 20 famous sio wa mtaani kwetu

Ngoja nikusanye data nirudi.
 
Engineering hakuna bahati mbaya, hakuna kukosea, ukikosea madhara yake ni makubwa sana na makosa yanaonekana. Udaktari kuna bahati mbaya, ukikosea watasema mpango wa Mungu au Mungu amempenda zaidi na makosa yanaweza yasionekane.
 
mnajaribu tu kustuastua eti dr na eng yan hiyo taaluma ya udokta acheni kama ilivyo halafu ni kama fedhea me naona kumuweka dr na eng eti wachuane kwnza eng hafui dafu hata kwa mwalimu wa primary!!

si unaona akili zako kama hao walimu
 
Back
Top Bottom