Kati ya prof. Lipumba, James Mbatia na dk Slaa nani anafaa kupeperusha bendera ya UKAWA

Poll: Kati ya prof. Lipumba,James Mbatia na dk Slaa nani anafaa kupeperusha bendera ya UKAWA

  • Dr. Slaa

    Votes: 49 87.5%
  • Prof. Ibrahim Lipumba

    Votes: 6 10.7%
  • James Mbatia

    Votes: 1 1.8%
  • Emmanuel Makaidi

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    56
  • Poll closed .
Umesema mengi mazuri ila DR.SLAA atosha sn. Tulishamwamin. Tunamwamini . Tutazidi kumuamini 2015
 
Mzee slaa kwasasa anamiaka 79 akiwa rais hataweza kumudu kazi zake hata kampeni hawezi kumudu kwanza uadilifu wake ni mbovu kweli hana sifa za kuwa kiongozi wa kitaifa kama rais wa twiga star hapo sawa.

Wewe acha,sisi tutamchagua kwa sababu tumemuona huyo kijana kazi anayemaliza kaziyake ilikuwa nikuzurula nakuomba omba nje tu! Kwahiyo tunahitaji Rais atakayekuwa hapa nasisi,atakayetibiwa Mhimbiri nasisi sio hao wa Ccm
 
Dr. Slaa ndiye nembo ya upinzani nchini - hilo halina ubishi. Na kama atachaguliwa na UKAWA kupeperusa bendera ya umoja huu kwa kiti cha URASI (tunaomba iwe hivyo), Basi ndugu zangu tukae mkao wa kula, mkao wa watawala wapya kwa mara ya kwanza katika nchi yetu.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki UKAWA -Tunaomba na Kushukuru kwa rehema zako kuu wewe uketiye mahapa pa juu ili uwezeshe tendo hili litimie kuinusuru nchi yetu na vizazi vijavyo.
 
Mimi naamini, mtu akishindwa kuongoza familia yake, hawezi kuongoza Nchi.

Uongozi huanzia kwenye familia.
 
Sioni sababu ya kumuacha Slaa kugombea urais kupitia Ukawa.Sitaki kukubali eti kauli yake kuhusu Bifu la JK na PK ndio sababu ya kumuona Slaa hafai.

Naamini Dr Slaa mwenyewe atampendekeza Tundu Lissu kupeperusha bendera ya Ukawa.

Hatuhitaji kusikia ubaya wa Dr Slaa ili tumjenge Mgombea mwingine.
 
Jamaa anatoa hoja nyepesinyepesi sana kuhusu masuala ya Watanzania. Ni wazi Kikwete ni tatizo anapenda kujipendekeza kwa watoto wa kufikia kwa sababu ya interest binafsi. Hana cha kuwasaidia Wanyarwanda ila ni kulinda business interest zake na akina Kabila kuanzia kule Kigamboni, mambo ya mafuta, madini ya kule Congo, sembe, nk. Hoja ya kuhamasisha insurgency ni ya kawaida tu katika mapambano. Mbona kikwete alimwita Salim muuaji, Hizbu na matusi mengine mengi, lakini mwandishi anaona ni sawa tu. Ama kweli nyani aoni kundule. Kuna suala la internationalism of the downtrodden regardless of colonially determined territorial boundaries, hivyo sio hoja wapenda haki wa nchi moja ku - rub shoulders na walalahoi wenzao wa nchi nyingine dhidi ya Kikwete na mafisadi wenzao kama Chenge, Madabida, Sita, Lowasa, Makinda, Joseph Kabila nk. Kwamba eti wabunge wakiwa wachache Slaa atashindwa kutawala. Ukweli ni kwamba hii hoja ni nyepesi pia kwa sababu katiba ya Tanzania inampa rais kuwa sehemu ya bunge ndio maana mswada hauwi sheria hadi rais assent. Lakini pia katiba imempa rais mamlaka ya kuvunja bunge endapo watashindana. Kama bunge likikataa kupitisha hoja zake anaweza kuvunja bunge na kuitisha fresh election. Hiyo itakuwa ni nafasi mwafaka kuingiza wabunge wengi wa UKAWA kwa vile katiba kupitia tume isiyo huru ya uchaguzi inaruhusu aliye madarakani kujipendelea. Kuna wabunge wangapi wa CCM watakuwa tayari kurudi kwa wananchi? Mwisho ya yote wewe huwezi kuwapangia UKAWA mgombea kwani hata huko CCM mzee Kingunge (katumwa na kikwete) ameshasema wote waliojitokeza hamna hata mmoja anayefaa. Kwa hiyo kabla hujaanza kuongelea UKAWA ni vizuri ukaangalia matatizo ya ndani mwako badala ya kujifanya unawahurumia UKAWA. Ukweli ni kwamba Slaa ni tishio kwa uhai wa CCM kuendelea kuwa madarakani ndio maana unadhani ni vema ukadhoofisha UKAWA kwanza. Jiandae kisaikologia kuwa kwenye upinzani.
 
Sioni sababu ya kumuacha Slaa kugombea urais kupitia Ukawa.Sitaki kukubali eti kauli yake kuhusu Bifu la JK na PK ndio sababu ya kumuona Slaa hafai.

Naamini Dr Slaa mwenyewe atampendekeza Tundu Lissu kupeperusha bendera ya Ukawa.

Hatuhitaji kusikia ubaya wa Dr Slaa ili tumjenge Mgombea mwingine.
 
hivi Wasira na DK Slaa nini mzee? hebu waangalie hata sura zao!

Afadhari kidogo Wasira mwili wake uko ki mazoezi sasa huyu babu viungo vinaanza kufa kimoja kimoja tutampoteza ktk kampeni na mjukuu wakw atabaki yatima, mwacheni alee familia yake, Lipumba na Mbowe si wapo?
 
Tunahitaji kiongozi mwenye msimamo kama Dk slaa. CCM hawana kiongozi makini kwa muda huu! watanzania wenzangu tuwaombe Ukawa wampitishe babu.
 
Afadhari kidogo Wasira mwili wake uko ki mazoezi sasa huyu babu viungo vinaanza kufa kimoja kimoja tutampoteza ktk kampeni na mjukuu wakw atabaki yatima, mwacheni alee familia yake, Lipumba na Mbowe si wapo?

hapana! macho yako hana ushirikiano! Wassira hataukimwangari kapinda. ulimuona alipoenda kukukagua maendeleo ya chama kigoma? mwenye picha hizo atupie hapa iliuone. slaa bado ananguvu.
 
hapana! macho yako hana ushirikiano! Wassira hataukimwangari kapinda. ulimuona alipoenda kukukagua maendeleo ya chama kigoma? mwenye picha hizo atupie hapa iliuone. slaa bado ananguvu.

Haya ila mtaniambia hapa!
Hata hivyo sioni mtu wa kumzuia Mbowe asigombee urais kutoka ukawa! Maana amedhamilia haswa.
 
Ukitaka tz ya neema.dr slaa ndye pekee atakayeweza kuwazibiti hawa mnaoita mapapa wa mafisadi ambao kna pm wamewashnda
 
Miccm ipo km mizukule eti nyie miccm mmerogwa au ? Kikwete umri wake 65 years Slaa 65 years. Lowasa 64 years Membe 65 years sijui ya. Baba yako ni mingapi ? haki ya kugombea kwa mujibu wa katiba ya nchi yetu kuanzia miaka 40 lkn katiba aijaelekeza kikomo cha. Uzee
 
Nianze kwa kumpongeza mtoa mada, amejipinda na ameonyesha dhamira ya kweli kutetea anachoamini ni sahihi. Kwa urefu wa andiko lake ni dhahiri anajua anachokisema na hakika kimetoka moyoni. Hawa ndio wantanzania tunaoweza kuwaita "great thinkers". Ninampogenza kwa ujenzi wa hoja yake na hisia zake kama Mtanzania.

Pamoja na maelezo yangu hapo juu, ninapingana naye vikali kabisa. Najua Dr. Slaa ni binadamu wa kawaida na ana mapungufu yake, sio mkamilifu kwa asilimia mia moja. Dr.Slaa hajatangaza kuwa atagombea au la! Kama amabavyo hata mwaka 2010 hakutangaza ila aliombwa na chama chake( CHADEMA) na dio maana wanachadema na watanzania wengine walimuamini na kumpigania hadi nguvu zao zilipoishia. Na kusema ukweli matokeo ya uchaguzi hayakuwasilisha maoni ya wapiga kura. Matokeo yalichezewa.

Hata hivyo alizuia umwagikaji wa damu kwa kukaa kimya hadi muda ukapita na wala hakuwataka wananchi wasiokubali matokeo waingie mitaani kupinga matokeo hayo. Hapo ndipo thamani ya Daktari huyu ilipodhihiri. Ni mpenda amani na anaona mbele sana. Anapashwa kupongenzwa na sio kumbeza.

Kama UKAWA wataona anafaa watampigania hadi mwisho nami nitakuwa miongoni ya wale watakao muunga mkono. Jambo moja ambalo nalo ni dhahiri ni kwamba mtoa mada anaona uwezekano wa Dr. Slaa kupendekezwa kwa kuwa anaaminika na anakubalika.

Dr. Slaa na kuomba ukiombwa na UKAWA au hata na CHAMA CHAKO kugombea nafasi hiyo usituangushe. Kubali.
 
Pole sana ndugu mleta mada naona Dr Slaa aakusumbua sana wewe Pamoja na Migamba wenzio kiasi cha kuamua kuzusha mambo ambayo katu Dr hajawahi kuongea ili tu upate kusherehesha nafsi yako kwa kujiaminisha eti umempaka matope Dr Slaa....

Ili upate kuwaokota wajinga wenzio hapa jukwaani umeona uanze kwanza na kumpamba kwa sifa unazodhani watavutiwa na hadithi zako then uje utupe mashambulizi yako, kitu ambacho kwa wajinga umefanikiwa lakini kwa watu waelewa wanakuona ni mwanafunzi wa chakechea kwa propaganda...!! Ili uweze kufaulu hilo darasa la propaganda itakuchukua zaidi ya miaka 50 kitu ambacho ninauhakika nacho kwa umri ulionao kama Mungu atakuacha hai basi utakuwa Kipofu,huoni tena kutokana na umri kukuelemea. Ni ushauri wa bure ukatafuta shughuri nyingine ya kufanya Dr Slaa humuwezi siyo Size yako wewe wala wakubwa wa chama chako. Alianza Kikwete akaja Nape,Mwigulu mpaka mzee Gombe hakuna aliyefanikiwa kufifisha nyota ya Dr kwa Watanzania hususani Watanganyika.

Ngoja nikuonyesha ujinga wako....

Unadai Dr Slaa alisema nchi haitatawalika kwasababu ya kuibiwa kura na Miccm... umedanganya watu mchana kweupe huku sura yako ikiwa imejaa matongotongo... Dr alidai inchi inaweza isitawalike endapo watawala hawatatenda haki kwa Watawaliwa si kutokana na kuibiwa kura kwenye uchaguzi bali kutokana na kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji kwa Watanzania vikitekelezwa na jeshi la Police kwa maelekezo ya Watawala.... hiyo kauli yako kampelekee aliyekutuma, mwambie akupe nyingine hii tumekushitukia.!!!

Unadai Dr Slaa Aliwahimiza watu kwenda kuwatoa Mbowe na Lema ndani ya kituo cha police huko Arusha...huu ni uongo meingine ukiwadnganya kadamnasi ya wajumbe wa Jf mchana kweupe ukiwa na matongotongo usoni... Siku hiyo ni kweli kulikuwa na Maandamano ya Amani nayo hayakuhusiana na Mgogoro wa Meya wa Arusha na Chadema, bali ni kudai haki baada ya Mbunge Lema kupewa Dhamana na Kituo cha police na MKUU WA MKOA WA ARUSHA KUZUIA KWA MATAKWA YAKE BINAFSI. Wananchi wa Arusha walikubaliana kuandamana kwa Amani na kukesha pale uwanjani kwaajili ya Mbunge wao mpaka siku atakayo tolewa Mahabusu..!!!! Na kwa kuthibitisha hilo Maandamano yalifanyika kwa Amani kabisa (Mbowe hakuwepo wala Lema) na yalipokelewa na Dr Slaa na kuyahutubia. Mpaka kufika saa moja kulikuwa na Amani ya kudumu, Police kwa maelekezo waliyoyapata kutoka wanakokujua wao wenyewe wakawatangazia watu watawanyike (Ajabu na kweli) watu walikuwa haawajafanya fujo yoyote wala kumjeruhi yeyote. Kuona hivyo Dr Slaa akawa anawahimiza watu kwamba wafanye kile walichokubaliana mpka kuandaa Maandamano hayo (Kukesha kwaajili ya Mbunge wao) Police kuona hivyo wakaanza kufyatua risasi hovyo (Kamwe hawakumjeruhi wala kumuua mtu yeyote siku hiyo) wale waliouwawa ni siku Chadema wamefanya Maandamano kwaajili ya kudai haki ya Uchaguzi wa Meya na siku hiyo hakukamatwa Mbowe wala Dr Slaa wala Lema (Isipokuwa walijipeleka wenyewe baada ya kuwa wanatafutwa na Police) kamwe haya Matukio hayahusiani ni mawili tofauti..

Uongo wako kamdanyanye mwanao anayenyonya na sio sisi watu wazima na ndevu.zetu zikiwa zinaeelkea kugeuka rangi....!!!

Kwahayo machache sina haja ya kuendelea kuonyesha ni namna gani umuongo kwenye hiyo mistari ya Rwanda na kikwete kwani ninaimani wati.washakujua wewe pamoja na aliyekutuma.. Tena mwambie hayo matango akawauzie wazee wake kule .......

Fillipo Mungi Crashwise Molemo Tumaini Makene etc.

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
Wasiwasi wangu ni kwamba atapora sana wake za watu kwani akimtamani mke wa mtu zake ni kuvu tu.
 
Back
Top Bottom